Maamuzi ya rufaa ya Lema na uhuru wa Lulu baada ya kubadilishiwa mashitaka

Lyimo

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,824
1,225
Ushindiwa G. Lema ulikuwa dhahiri tangu awali. Licha ya kubadilisha majaji, kuhamisha mahakama kutoka Arusha kwenda Dar na kupeleka mbele siku ya kutoa maamuzi licha ya shauri kusikilizwa siku nyingi. Hili la kulipeleka mbele hadi leo ambapo pia Lulu amebadilishiwa mashitaka na sasa anaweza kuwa huru mtaani huku akiendelea na aina nyingine ya mashitaka na si ya kuuwa kwa kukusudia.

Kutokea kwa mambo haya mawili wengi tunatafasiri kuwa serikali ipo nyuma ya maamuzi ya kesi ya Lulu. Imemrudishia Lema ushindi wake ambao umechukua attension kubwa ya wananchi hasa wa Dar na Arusha.

Kwa jinsi watanzania tulivyo hatutaona tena issue ya Lulu, na hatutahoji kulikoni. Siingilii maamuzi ya mahakama, bali najiuliza maswali mengi kutokana na obvious coincidence zinazotokeaga Tanzanaia. Coincidences zinaweza kupangwa na zikafanikisha madhumuni yake katika nchi hii tu.
 
qaymo

Member
Dec 14, 2012
16
0
Naungana na msemaji , kuwa Serikali ya Tanzania inafanya mambo kwa kuangalia ni jambo gani kwa wakati huo ni serious na inaleta hofu kwake , na inafahamu kuwa Watanzania maamuzi yao ni ya matukio . Tunakumbuka vema Babu wa Loliondo jinsi alivyokuzwa wakati serikali ilikuwa kwenye migogoro kibao na Wananchi wake lakini wakasahau yale muhimu , robo ya Watanzania ni Loliondo! matokeo yake yakasababisha vifo visivyo vya lazima ! Mfano wagonnjwa wa Kisukari na Ukimwi unawanywesha kikombo cha miti shamba na kuaminisha kuwa wamepona ! wapi na wapi. Hongera Lema kwa kuwa Mbunge wa Arusha - Chapa kazi .
 
JF-MBUNGE

JF-Expert Member
May 1, 2012
421
0
Ndio maana nilisema juzi ukishaona kesi inapigwa kalenda ovyo ovyo na mara kuhamishwa mikoa hamna kesi hapo bali ni mipango tuu...hongera kwa kuliona hili we una akili.
 
Sarya

Senior Member
Nov 6, 2009
151
225
Mimi naona ni kama wanafunika habari ya Lema kushinda kwa kutafuta vijihabari kama ya Lulu na ku diversify attention ya watanzania maana hata kesho baadhi ya vyombo vya habari vitajielekeza zaidi kwa Lulu badala ya hukumu ya Lema.
Watu wa namna hii huwa hawashindwi.........wanaweza hata wakamua kutega bomu kwenye maeneo muhimu leo na ilipuke leo hii hii ilimradi kudhoofisha taarifa za hukumu ya Lema.
 
tutaweza

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
634
500
Naunga mkono kuhusu hoja ya kesi ya Lema.

Ila suala la Lulu lipo wazi sana, huyu mtoto alitakiwa kuwa mtaani kitambo kwani mazingira yanaonyesha hakuua kwa kukusudia. Nadhani kubadilishiwa mashtaka kulicheleweshwa pia kwa sababu ya usalama wake (maana wale binadamu waliomhukumu kwa mauaji wangemsumbua sana mtaani, afadhali ya sasa wameshaanza kusahau)
 
chadog

Member
Aug 11, 2012
64
70
Ndivyo ilivyo..kwanza Ile ya kunasana ilipikwa kupoteza wabongo..mpaka Leo Hanna proof..picks Zote Kent magazeti ya udaku zilikuwa tofauti tofauti..
 
zeus

JF-Expert Member
Aug 13, 2009
213
0
Ushindiwa G. Lema ulikuwa dhahiri tangu awali. Licha ya kubadilisha majaji, kuhamisha mahakama kutoka Arusha kwenda Dar na kupeleka mbele siku ya kutoa maamuzi licha ya shauri kusikilizwa siku nyingi. Hili la kulipeleka mbele hadi leo ambapo pia Lulu amebadilishiwa mashitaka na sasa anaweza kuwa huru mtaani huku akiendelea na aina nyingine ya mashitaka na si ya kuuwa kwa kukusudia.

Kutokea kwa mambo haya mawili wengi tunatafasiri kuwa serikali ipo nyuma ya maamuzi ya kesi ya Lulu. Imemrudishia Lema ushindi wake ambao umechukua attension kubwa ya wananchi hasa wa Dar na Arusha.

Kwa jinsi watanzania tulivyo hatutaona tena issue ya Lulu, na hatutahoji kulikoni. Siingilii maamuzi ya mahakama, bali najiuliza maswali mengi kutokana na obvious coincidence zinazotokeaga Tanzanaia. Coincidences zinaweza kupangwa na zikafanikisha madhumuni yake katika nchi hii tu.

In effect, ushindi wa lema OVERSHADOWS the irregularities katika suala la llulu, if any.
hivi ni coincidence au ni "ushirikiano" ?
 
Lyimo

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,824
1,225
Nafikiri hili la Lema limeachiwa ili kuleta imani kwa MAJAJI feki wa JK. Watu hawatakaa wahoji hilo tena.
 
HASSAN SHEN

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
428
170
Wakati watu wakifurahia ushindi rufaa ya Lema wamesahau kauli kuwa Raisi/Ikulu kuingilia maamuzi ya mahakama, leo sijui mnasemaje?!! Tuhuma za msanii Lulu zimebadilishwa kutoka kuua kwa kukusudia mpaka kuua bila kukusudia na kupatiwa dhamana, jambo la ajabu DPP bado anamshikilia mtuhumiwa wa wizi wa kokoto Sheikh Ponda kwa kutompa dhamana. My take: Huu ni ubaguzi na DPP anatufanyia dhihaka. Tatizo la nchi hii akili ndogo huongoza akili kubwa, aibu
 
kiparah

JF-Expert Member
Sep 7, 2010
1,173
0
Una uhakika kwamba Lulu kapewa dhamana au umekurupuka tu? Kwa taarifa yako tu, Lulu hajapewa dhamana ila kesi yake imehamishiwa mahakama kuu. Kuwa makini na vyanzo vyako.
 
CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
12,367
2,000
wakati watu wakifurahia ushindi rufaa ya lema wamesahau kauli kuwa raisi/ikulu kuingilia maamuzi ya mahakama, leo sijui mnasemaje?!! Tuhuma za msanii lulu zimebadilishwa kutoka kuua kwa kukusudia mpaka kuua bila kukusudia na kupatiwa dhamana, jambo la ajabu dpp bado anamshikilia mtuhumiwa wa wizi wa kokoto sheikh ponda kwa kutompa dhamana. My take: Huu ni ubaguzi na dpp anatufanyia dhihaka. Tatizo la nchi hii akili ndogo huongoza akili kubwa, aibu

dpp, na ponda ameiba kokoto, kuchochea ghasia bila kukusudia apewe dhamana. Takbir!!!!!!!!!!!!!!!!!!allah!!!!!!!!!!!!
 
Ronn M

JF-Expert Member
May 2, 2012
1,279
0
Ushindiwa G. Lema ulikuwa dhahiri tangu awali. Licha ya kubadilisha majaji, kuhamisha mahakama kutoka Arusha kwenda Dar na kupeleka mbele siku ya kutoa maamuzi licha ya shauri kusikilizwa siku nyingi. Hili la kulipeleka mbele hadi leo ambapo pia Lulu amebadilishiwa mashitaka na sasa anaweza kuwa huru mtaani huku akiendelea na aina nyingine ya mashitaka na si ya kuuwa kwa kukusudia.

Kutokea kwa mambo haya mawili wengi tunatafasiri kuwa serikali ipo nyuma ya maamuzi ya kesi ya Lulu. Imemrudishia Lema ushindi wake ambao umechukua attension kubwa ya wananchi hasa wa Dar na Arusha.

Kwa jinsi watanzania tulivyo hatutaona tena issue ya Lulu, na hatutahoji kulikoni. Siingilii maamuzi ya mahakama, bali najiuliza maswali mengi kutokana na obvious coincidence zinazotokeaga Tanzanaia. Coincidences zinaweza kupangwa na zikafanikisha madhumuni yake katika nchi hii tu.

Ndugu, Mkurugenzi wa mashata ya jinai anaouwezo kikatiba wa kubadilisha au kufuta mashtaka yanayomkabili mtuhumiwa. Sababu kubwa ya kubadilisha mashtaka huwa ni pale ambapo upelelezi uliofanya haujapelekea ushahidi kwa kosa alilotuhumiwa nalo lakini unaweza kupelekea kutiwa hatiani kwa kosa jingine dogo. Ieleweke kwa kosa la mauaji lazima kuwepo na tendo lenyewe (actus reus) na nia ya kumwuua mhusika (mensrea). Sasa ni dhahiri ingelikuwa ngumu kumtia Lulu hatiani kwa kosa la mauaji. Ila kwa kosa la kuua bila kukusudia, hata tendo la uzembe (mfano kurusha kitu bila kuwa na nia ya kumdhuru mtu ila kwa bahati mbaya akadhurika na kufa) inapelekea hatia! Sasa kubadilisha mashtaka kunaiweka prosecution katika nafasi nzuri zaidi ya kuthibitisha kuwa Lulu aliua bila kukusudi, na ukichukulia kuwa 'alimsukuma tuu', uwezekano wa kuachiwa huru either kwa murder au maslaugher ni mkubwa sana
 
zenmoster

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
952
250
Wakati watu wakifurahia ushindi rufaa ya Lema wamesahau kauli kuwa Raisi/Ikulu kuingilia maamuzi ya mahakama, leo sijui mnasemaje?!! Tuhuma za msanii Lulu zimebadilishwa kutoka kuua kwa kukusudia mpaka kuua bila kukusudia na kupatiwa dhamana, jambo la ajabu DPP bado anamshikilia mtuhumiwa wa wizi wa kokoto Sheikh Ponda kwa kutompa dhamana. My take: Huu ni ubaguzi na DPP anatufanyia dhihaka. Tatizo la nchi hii akili ndogo huongoza akili kubwa, aibu
sijakupata mkuu.. unamaana raisi wako ana akili ndogo? ila yawezekana uko sahihi na GPA ya 2.1 yawezekana ulisemalo lina ukweli
 
Kamanda Kazi

JF-Expert Member
Dec 15, 2012
2,613
1,225
yap mkuu huenda kuna namna hapo! japo ushindi wa Kamanda Lema ni dhahili. hebu tukumbuke hili. kabla Babu Loliondo hajainuliwa na serikali kwa kupigiwa debe kulikuwa na malalamiko makubwa sana juu ya malipo ya DOWANS dhidi ya TANESCO. vyama vya siasa na wanaharakati walitishia kufanya maandamano nchi nzima kupinga malipo hayo. serikali ikaona hapo imekuwa nongwa so ili kuwapoteza watanzania ikapiga debe sana juu ya Babu Loliondo. tena viongozi wake wakuu wakaenda huko Loliondo na tukaoneshwa wakipata vikombe. serikali ikaweka taratibu za usafiri kwenda huko. ikatangaza kukarabati barabara. ikafanikiwa kuteka fahamu za watanzania! hata leo tumesahau DOWANS na malipo yake! nani anajua kesi ya DOWANS dhidi ya TANESCO inaigharimu serikali mapesa mangapi????
:shut-mouth:
 
Jallen

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
516
225
Ushindiwa G. Lema ulikuwa dhahiri tangu awali. Licha ya kubadilisha majaji, kuhamisha mahakama kutoka Arusha kwenda Dar na kupeleka mbele siku ya kutoa maamuzi licha ya shauri kusikilizwa siku nyingi. Hili la kulipeleka mbele hadi leo ambapo pia Lulu amebadilishiwa mashitaka na sasa anaweza kuwa huru mtaani huku akiendelea na aina nyingine ya mashitaka na si ya kuuwa kwa kukusudia.

Kutokea kwa mambo haya mawili wengi tunatafasiri kuwa serikali ipo nyuma ya maamuzi ya kesi ya Lulu. Imemrudishia Lema ushindi wake ambao umechukua attension kubwa ya wananchi hasa wa Dar na Arusha.

Kwa jinsi watanzania tulivyo hatutaona tena issue ya Lulu, na hatutahoji kulikoni. Siingilii maamuzi ya mahakama, bali najiuliza maswali mengi kutokana na obvious coincidence zinazotokeaga Tanzanaia. Coincidences zinaweza kupangwa na zikafanikisha madhumuni yake katika nchi hii tu.
Who is Lulu, yaani kweli huyu binti anaweza kuondoa tension ya lema kwa umma
 
nice 2

JF-Expert Member
Aug 10, 2011
747
0
Watu mnapenda kushobokea majungu! Nani kawaambia kwamba Lulu kapata dhamana?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom