Maamuzi ya Mahakama: Shule Bora Kwa Wapenda Sheria

George Dalali

Member
May 3, 2014
37
150
Wakuu, wasalaam.

Malengo ya uzi:

1. Kusoma na kujifunza toka kwenye maamuzi mbalimbali ya Mahakama.

2. Kushiriki kuibua mijadala ya kifikra kuhusu tafsiri mbali mbali za Sheria zilizotolewa kwenye maamuzi mbalimbali ya Mahakama.

3. Kushirikiana ufahamu na kuiishi Sheria.

Muongozo:

1. Kutochanganya mihemuko ya kisiasa na Sheria.

2. Kujadiliana kwa lugha ya staha na kuheshimu mawazo tofauti tofauti.

3. Kujadili hoja na si mtu.

4. Kuzingatia malengo ya uzi.

Vikwazo/changamoto:

Kukiuka Malengo na Muongozo tajwa.

Chimbuko la wazo hili (kwa tafsiri yangu):

1. Kujaribu kuitekeleza topic husika kwa vitendo.

2. Kuongeza chachu kwenye Jukwaa hili.

Ahadi yangu:

Uvumilivu wa kadri.

Kuhusu utaratibu:

Mtu yeyote (pamoja na mimi) anaweza kupost hapa uamuzi wa Mahakama na kuandika jinsi alivyo uelewa.

Nukuu: tafadhali, uelezaji wa uelewa wa mtu husika kuhusu uamuzi wa Mahakama usiwe wa kuikashifu au kuidhalilisha Mahakama husika. Lengo ni kuielewa Sheria kupitia maamuzi ya Mahakama.

Tahadhari:

Baadhi ya maandiko yanaweza kuwa si katika lugha nyepesi kihivyo. Hatahivyo mwandishi anashauriwa kurahisisha uandishi wake kiasi kwamba audience imuelewe au angalau ipate picha.

Faraja:

Kama wachangiaji wa uzi huu watazingatia maelezo hapo juu, ipo faraja kwamba uzi huu utafungua ukurasa Mpya katika segment hii ya Jukwaa la Sheria, aidha upo uwezekano wa uzi huu kuwa endelevu.

Karibuni.
 

George Dalali

Member
May 3, 2014
37
150
Binafsi the Court imenichanganya kwenye uamuzi huu.

Ukiusoma uamuzi Appellant alifile petition of Appeal High Court dhidi ya uamuzi wa Assistant Registrar of title of Dodoma (rejea quotation ya petition of appeal).

Katika ground za Appeal alieleza kwamba Registrar huyo hakuzingatia kwamba maamuzi ya District court hayakuwa sahihi.

The Court ika nullify maamuzi ya High Court, maamuzi ya District Court na maamuzi ya pili ya Primary court.

Mambo yaliyovutia fikra zangu:

1. Title: je rufaa kwenda High Court, ilikuwa sahihi kwa hoja ya ku title document kama 'petition of Appeal' au ilipaswa kuwa 'memorandum of appeal'?

2. Maamuzi yaliyokatiwa rufaa High Court yalihusu uamuzi wa Assistant Registrar of title wa Dodoma.

Je ilikuwa sahihi kwa the Court kutoa amri dhidi ya uamuzi wa District Court na Primary Court?

Kwa maneno mengine:

Je ukikata rufaa dhidi ya maamuzi ya A, rufaa hiyo inaweza kutafsirika kwamba umekata rufaa dhidi ya maamuzi ya B na C kwakuwa tu vina uhusiano?

Note: mlologo ruhusiwa wa kukata rufaa unataja mamlaka ya kiserikali kuwa na mlolongo tofauti na wa mamlaka za Judiciary.

Kwa maneno mengine tena:

Je mamlaka za kiserikali zikitoa maamuzi yasiyo sahihi, venue ni rufaa? Kama Sheria imeelekeza hivyo kwenye issue ya Assistant Registrar of title (sijasoma Sheria husika), je ni kusema:

Maamuzi ya Serikali yaliyotokana na maamuzi ya Judiciary yakikatiwa rufaa rufaa hiyo inahusisha maamuzi husika ya Judiciary?

Tafadhali nukuu kwamba rufaa to the Court ilihusu maamuzi ya High Court. Jionye kwamba katika maamuzi hayo ya the Court maamuzi yote ya chini ya Serikali na Judiciary yalitolewa uamuzi.

Kuhusu kupunguza stress: story ya uamuzi ni ipi?

1. Mtu A ilijitahidi akajenga nyumba. Akampangisha mtu B.

2. Mtu A akafariki dunia. Tumtakie heri.

Mtu C akateuliwa kuwa msimamizi wa mirathi. Mtu C akajichanganya akashindwa kugawa mirathi ndani ya muda wa kisheria, aidha hakuomba extension of time ya kugawa mirathi.

3. Mtu D kwa namna isiyo elezewa vyema akafanikiwa kupata order ya Mahakama ya kutengua usimamizi wa mirathi wa mtu C na yeye mtu D akateuliwa kuwa msimamizi wa mirathi.

4. Kwa mbwembwe na ndani ya muda mfupi, mtu D akamuuzia mtu B nyumba bishaniwa (mpangaji) na Assistant Registrar of title akabadilisha umiliki kwenda kwa mtu B.

5. Mtu C hakuridhika akaomba revision District Court. Akapigwa chini, akaamua kufile Appeal High Court lakini akasema anachokatia rufaa ni maamuzi ya Assistant Registrar of title wa Dodoma.


Asante kwa kusoma.
 

George Dalali

Member
May 3, 2014
37
150
Tafadhali ridhia tuvuruge kidogo break yako kidogo:

Madhara ya makosa ya mchapaji wa hukumu and Mahakama.

Pata saga ya story:

Mh Judge wa High Court aliamua kwamba Appellant hana hatia na anatakiwa kuachiwa huru.

Appellant hakuachiwa huru na aliendelea kutumikia kifungo. Sababu?

(let the Court speaks itself at page 5 of this decision):

"... we think the confusion was brought by the inclusion in the typed script of a text which is not part of the decision of the High Court.

Kwa namna yeyote, Mh Jaji asingeweza kufanya kosa hili. Tafadhali jionye, ukijakuwa Mh. Jaji. Usiwaamini wachapaji.

Kuhusu farijiko:

The Court ilifanya yafuatayo kama sehemu ya kushare hisia za maumivu:

1. Baada ya kusikiliza rufaa, the Court iliamuru accused awe released hata kabla ya kutoa uamuzi wa mwisho wenye sababu za maamuzi husika.

2. The Court imetoa onyo kwa mamlaka husika kutorudia kosa elezewa.

3. The Court, iliamua kwa uchungu mkubwa ku scan kile kilicho andikwa na Hon. Jaji wa High Court kwenye proceedings (toka kwenye file la kesi) ambacho ni tofauti maamuzi yaliyochapwa.

Huu ni mmoja wa uamuzi ambao huhitaji darubini kuona hasira za Mahakama ya Rufaa.

Asante kwa kusoma. View attachment emmanuel-ngunja-vs-republic-criminal-appeal-no254-2012-new.pdf
 

George Dalali

Member
May 3, 2014
37
150
Uamuzi huu unahusu admission and authenticity of electronic evidence.

Ubora wa uamuzi huu:

1. His Lordship Mwambegele J amejitahidi mno. Uamuzi umekuwa very authoritative kutokana na Utafiti mkubwa alio ufanya yeye mwenyewe kama Jaji na Mahakama.

No wonder, alirusha ka kijembe kadogo kwa Counsels wa parties kwamba si sahihi kwa wao kulalamikia upya wa hoja hii kama sababu ya ukosefu wa authorities. Walitakiwa kutumia technology kufanya research kuhusu suala hili kama lilivyo kwenye nchi nyingine.

2. Jaji ametoa a comprehensive lecture on the history of admissibility of electronic evidence.

Historia hii, itakuwezesha kufahamu kwa kina jinsi judiciary ilivyo changia kwenye mchakato huu, jinsi Sheria zilivyo badilishwa hatua kwa hatua, position ilivyo kwa nchi nyingine, tafsiri ya ujio wa Electronic Transactions Act, 2015 nk.

3. Jaji amejitahidi mno, tena kwa ku demostrate kuonesha inns, gist, intention, scope and applicability ya section 18 (2) (a), (b) and (c) of the Electronic Transactions Act, 2015.

Kimsingi, kwa wale wapenda PO hoja karibu nyingi dhidi ya admission ya electronic evidence zinatokana na tafsiri ya yardsticks zilizowekwa na section hii.

Jaji amejitahidi mno kuelezea bayana kila criteria na inavyo fanya kazi na amekwenda mbali kiasi cha kutumia criteria moja moja kuamua matter iliyokuwa mbele yake.

Kwa kufanya hivi Jaji amepunguza mno ambiguities zinazojitokeza katika kutafsiri section tajwa.

4. Ukisoma vyema uamuzi huu utagundua kwamba mbali na section tajwa au Sheria elezewa, yardsticks nyingine zinatoka kwenye Evidence Act.

Moja ya kigezo kilichoibua maswali mengi ni "originality ya electronic evidence" inayotarajiwa kuwa admitted.

Jaji amejitahidi kadri alivyo weza kuielezea hoja hii.

Hoja hii ni ya kihistoria, ilikuwepo hata kabla ya ujio wa Electronic Transactions Act. Lakini pamoja na uzamani wake, bado ni hoja tata mno. Ni wazi kwamba Marekebisho ya Sheria na hata Sheria mpya zilizofuata hazijafaulu vizuri ku deal na changamoto zinazo jitokeza kwenye hoja hii.

Note: Kwenye uamuzi huu Jaji amejadili pia vipimo vingine kama relevancy, Chain of Custody nk.

Maoni yangu:

Safari ya admission of electronic evidence ni ndefu. Hatua tuliyofikia ni njema. Tunashukuru.

Hata hivyo nachelea kusema kwamba ukikutana na Makamanda wapenda PO na wanaoweza kutembea na beat za PO kwa roho ngumu hatua kwa hatua, unaweza kujenga dhana kwamba vigezo vilivyo wekwa hasa na section 18 havitimiliziki.

Kinacho tokea mara nyingi ni kwamba ukivuka vipimo vipya vya Electronic Transactions Act, unaanza kukabiliana na filter ya zamani ya provisions za Evidence Act. Kazi inakuwepo!.

Ni kama Sheria hizi zimekubali hoja ya admission of electronic evidence kwa kufungua mlango mmoja na wakati huo huo kuikataa hoja hiyo kwa kufunga mlango mwingine (hasa section 18 ya Sheria tajwa).

Asante kwa kusoma. View attachment electronic evidence case.pdf View attachment 1520889
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom