nundaz
JF-Expert Member
- Jun 8, 2012
- 273
- 191
mkuu unapoteza muda kumjibu mtu kajiunga JF juzi?????Wewe naona umejiunga na JF wakati huu wa uelewa mdogo wa polisi kuhusu PGO je na wewe unauelewa mdogo kiasi chao
mkuu unapoteza muda kumjibu mtu kajiunga JF juzi?????Wewe naona umejiunga na JF wakati huu wa uelewa mdogo wa polisi kuhusu PGO je na wewe unauelewa mdogo kiasi chao
Memeo hajapasha kiporo leo!!?Huyo gaidi wanamchelewesha tu kama alifikia hatua ya kutapeli familia yake kwa kujimilikisha mali zote za urithi wampige haraka mvua 50
Hili ni jukwaa kwaajili ya watu wenye akili timamu. Wewe ungetafuta jukwaa lenye kukufaa.Huyo gaidi wanamchelewesha tu kama alifikia hatua ya kutapeli familia yake kwa kujimilikisha mali zote za urithi wampige haraka mvua 50
Mkuu cheki mtiririko naona hauko sawa....Ngoja tuone mwisho wake
Kesi hii si mchezo aseeHii ndio taarifa iliyotufikia , kwamba leo Mke wa Mshitakiwa aliyeteswa kinyama komando Adam kasekwa leo atapanda kizimbani akiwa ni shahidi wa tatu wa upande wa utetezi katika kesi ndogo ndani ya kesi kubwa inayomkabili Freeman Mbowe na Wenzake watatu
Endelea kufuatilia
========
Saa 3 na Dakika 11 Tupo Chumba Cha Mahakama Tayari, Kwa Mawakili wa Utetezi wapo tayari Mahakamani ila Mshitaka bado wapo Nje
Jaji: ameshaingia Sasa Mahakamani
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021, Jamuhuri dhidi ya Halfan Bwire,Adam Hassana Kasekwa (Adamoo), Mohammed Abdalah Ling'wenya na Freeman Aikael Mbowe
Kesi inatajwa
Jaji: Habarini za Asubuhi, Tuendeleeni ni Siku Nyingine
Jaji: sawa
Wakili wa Serikali: naomba Radhi tumeingia wakati umeshaingia
Jaji: Wakili wa Serikali
Wakili wa Serikali: Kidando anatambulisha wenzake
Robert Kidando
2. Nassoro Katuga
3. Ignas Mwanuka
4. Esther Martin
5. Tulimanywa Majigo
Jaji: Utetezi
Kibatala: anatambulisha Wenzake
Advocate Peter Kibatala
Advocate Jonathan Mndeme
Advocate Fredrick Kiwhelo
Advocate John Malya
Advocate Sisty Aloyce
Advocate Alex Masaba
Advocate Idd Msawanga
Advocate Gaston Garubindi
Advocate Evaresta Kisanga
Advocate Faraj Mangula
Advocate Maria Mushi
Advocate Bonifasia Mapunda
Wakili Dickson Matata anaombewa Ruhusa Mdogo wake anafanyiwa Operesheni Hospitali ya Lugalo
Jaji: Wakili wa Serikali
Jaji: John Mallya
Wakili wa Serikali: Tumekuja kwa ajili ya kesi Ndogo ambapo Shahidi wa tatu yupo tayari kuendelea Kutoa Ushahidi wake
Mallya: Tunaye Shahidi, Na Shahidi yupo tayari kutoa Ushahidi
Shahidi: Mdada anatokea Nyuma kabisa ya Chumba Cha Mahakama anaenda Kizimbani
Jaji: Shahidi wa tatu upande wa Utetezi ambaye ameandaliwa Tafadhali anaweza Kuja
Jaji: anaandika Kidogo na Ukimya wa Mahakama
Jaji: Shahidi unaitwa nani
Jaji: Shahidi upo Mahakamani ondoa Hofu, nitakuuliza Majina yako na Nitakuapisha, Wakili wa Utetezi atakuongoza na Mawakili wengine watakuuliza Swali na Mawakili wa Serikali watakuuliza Maswali pia huna Haja ya Kuogopa, tupo hapa kutafuta Haki
Shahidi: Lilian Kibona
Dini Mkristo
Jaji: wakili Mallya endelea
Jaji: Liliani utachagua Kukaa au Kusimama,Hata Ukikaaa nitakuona
Shahidi: Naapa Mbele ya Mahakama hii kuwa Ushahidi nitakao toa utakuwa Ukweli na Ukweli Mtupu , Mungu ni Saidie
Mallya: Shahidi Unaishi wapi
Shahidi: Chalinze Mkoa wa Pwani
Shahidi: Ramboni
Mallya: sehemu gani huko Chalinze,
Jaji: ni Mtaa.?
Mallya: Unaishi na nani..?
Shahidi: Ndiyo
Shahidi: Na mmewangu na Watoto ambaye kwa Sasa Mme wangu ameshikiliwa
Shahidi: Ndiyo
Jaji: ni Miongoni Mwa washitakiwa ??
Mallya: Mme wako anaitwa nani.?
Mallya: hapa kila nikiwa namuita Mshitakiwa wa Pili nitakuwa namaanisha pia ni yeye
]
Shahidi: ndiyo
Shahidi: Adamu Khalfani Kasekwa
Mallya: Ndoa Ya Kiserikali
Mallya: Mmeona lini 05 08 2016
Shahidi: Ndiyo
Shahidi: Palepale Chalinze
Mallya: Mlikuwa mnaishi wapi
Mallya: unaweza Kukumbuka Mmewako alikuwa anafanya kazi gani wakati huo
Mallya: alikuwa anafanya kazi gani Nyingine
Shahidi: Askari jeshi wa JWTZ kikosi cha 92 Ngerengere
Shahidi: alikuwa hana kazi Nyingine zaidi ya hiyo ya Serikali
Mallya: naruka nakuja 2020 Mme wako alikuwa anafanya kazi gani
Shahidi: alikuwa anafanya shughuli zake za Biashara
Mallya: Kabla ya Kwenda Moshi mlikuwana Hali gani kati yako na Mme wako
Mallya: Mwanzoni Mwa Mwezi wa Nane Mwaka 2020 unakumbuka Kilitokea Kitu gani kati yako na Mme wako
Shahidi: Mme wangu alikuwa Moshi, tulikuwa tunawasiliana naye Vizuri
Shahidi: Palikuwa na Mawasiliano
Shahidi: Rafiki yake Ling'wenya waliwasiliana kuwa kuna Kazi imepatikana Moshi
Mallya: kabla ajaenda Moshi kitu gani kilitokea
Shahidi: Hapana sikumbuki
Mallya: Unaweza Kukumbuka Siku na Saa ya hayo mawasiliano
Jaji: unasema palikiwa na Mawasiliano Kati ya Mme wako na Ling'wenya .?
Jaji: Ndiyo
Shahidi: Ndiyo Kwamba Ling'wenya alimpigia Simu kuwa kuna kazi Imepatikana Moshi
Mallya: Simu zilikuwa zinapigwa kati ya Ling'wenya na Mme wako wewe ulijuaje
Mallya: Jambo gani lilifanyika, kabla ya Mme wako kwenda Moshi
Mimi kama Mke nilimruhusu
Shahidi: Mimi Kama Mke wake alinishirikisha
Mallya: Hali ya Mme wako ki Afya Wakati anaenda Moshi hali yake ilikuwaje
Shahidi: Nakumbuka walikutana na Ling'wenya wakaemda Kwanza Morogoro, Wakarudi, Waliporudi wakajiandaa Wakaenda Moshi
Shahidi: aumwi na Kwamba anaweza Kwenda Moshi
Shahidi: Ilikuwa Nzuri inamruhusu kwenda Kufanya kazi
Mallya: Hali Nzuri unamaanisha nini , Mwambie Mheshimiwa Jaji
Mallya: mlikuwa mnatumia Njia gani kufanya mazungumzo
Shahidi: alinitaarifu kuwa amefika Moshi
Mallya: kitu gani kilifuata baada ya Kwenda Moshi
Mallya: Siku ya Tarehe 05 08 2020 kitu gani kilitokea
Shahidi: alinipigia na akaongea na watoto, tulipokuwa tunaongea akasema Hebu subiri nikamsubiri
Shahidi: kwa Njia ya Simu
Mallya: kitu gani Kilifuata
Mallya: ilikuwa Saa ngapi Kama Saa Moja
Mallya: alipokwambia Subiri kidogo nitakupigia Kidogo
Shahidi: Sikumbuki Kichwani lakini ipo kwenye Simu yangu
Shahidi: Nilipoona Muda umeenda ilipofika Saa 10 ilibidi nimpigie,Simu iliita ikawa imepokelewa lakini Kina nikisema Hallo Sisikii Mtu akiongea
Mallya: Unaweza Kukumbuka namba ya Simu uliyopiga ambayo ulipiga Ikapokelewa.?
Mallya: Baadae kilifuata nini baada ya Simu kutokupelewa
Mallya: kitu gani Kilifuata
Shahidi: baadae Ikawa haipatikani
Mallya: baada ya Kumpigia Ling'wenya.?
Shahidi: kwakuwa nilikuwa na namba ya Mwenzake Ling'wenya nikampigia Ling'wenya
Mallya: Sasa wewe ilipata hisia gani baada ya kuona Inaita hadi Kesho yake haipokelewi
Shahidi: niliona labda ni Mambo ya Kazi, sikuwa na wasiwasi wowote
Shahidi: Ikawa ainaita Mpaka jioni ,Mpaka Usiku ,Mpaka Kesho yake inaita haipokelewi
Shahidi: Wewe ulichukua hatua gani..?
Shahidi: Sikuwa na mtu Mwingine yoyote wa akumuuliza Zaidi ya Ling'wenya
Mallya: Baada ya hapo Kitu gani Kilifuata baada ya kuhisi ni Mambo ya kazi
Shahidi: Miaka 3 na Miezi 9
Shahidi: Sikuwa na namna yoyote zaidi ya Kusubiri simu kutoka kwao
Mallya: Una mtoto unesema anaumri gani?
Shahidi: nakumbuka ilikuwa 09 08 Mwaka 2020 niliamka Asubuhi ikiwa siku ya Jumapili, Mtoto alikuwa anasumbuliwa na tumbo
Jaji: Mtoto wa Jinsia gani
Mallya: Nataka kukupeleka Tarehe 09 Mwezi 08 kitu gani Kilitokea
Mallya: kwanini Unakumbuka kuwa ilikuwa Siku ya Jumapili
Shahidi: Wakike
Shahidi: Sababu ilikuwa Siku ya Ibada
Shahidi: Sikwenda Ibadani badala yake nikaenda Hospitali
Mallya: ikawaje huko Hospitali
Mallya: Ikawaje
Shahidi: Nilipokelewa
Mallya: Hospitali gani
Shahidi: Hospitali ya Serikali palepale Chalinze
Mallya: baada ya Kupokelewa Hospitali
Shahidi: nilipatiwa Huduma nikarudi Nyumbani
Mallya: Ule Mlango ulikuwa katika hali gani
Mallya: baada ya Kurudi Nyumbani niliona Miguu ya watu kama Imekanyaga, Wakati natoka Nyumbani nilifunga Mlango lakini niliporudi nikakuta Milango ipo wazi
Shahidi: Mlango ulikuwa wazi na Kitasa nikakuta kimevunjwa
Shahidi: kwa akili ya harakaharaka nilijua Wezi, Cha ajabu kila kitu nilikuta Vipo, Kitu kama Tv lakini vipo
Mallya: enheeee ikawaje
Mallya: kitu gani kikatokea
Jaji: Za Mme wako
Shahidi: zote zimemwaga,na Mabegi yamefunguliwa
Shahidi: Nikaingia Chumbani nikakuta Nguo za zimemwagwa Chini
Shahidi: Alinunua Congo Begi lenye Mabaka Mabaka ya Jeshi
Shahidi: Kuna begi alinunua Congo nilipokuja kikakuta halipo
Mallya: Jirani yako anaitwa nani.?
Mallya: Kitu gani kilifuata
Shahidi: Nilienda Kuuliza Majirani zangu
Shahidi: niliemda Kuuliza kama Mme wangu amekuja Nyumbani? wamemuona.? kwamba kunakitu huenda alikuja Kukitafuta kwa haraka haraka
Shahidi: Judith Charles
Mallya: lengo la kwenda kwa Jirani lilikuwa nini
Mallya: Jirani alikwambiaje
Jaji: Ndiyo
Shahidi: Kuna Magari yalikuja hapa Ya Kipolisi, Moja walikuwa wamevaa Sare na Wengine walikuwa Wamevaa Kiraia
Mallya: Taarifa Nyingine alikupa Jirani yako ni Ipi
Mallya: baada ya hapo Mapolisi walishuka kwenye gari wakaingia Ndani
Shahidi: kwamba Mapolisi walimuita kwa lengo la Kuniulizia Mimi
Mallya: yeye Jirani alikuwa anafanya nini wakati huo
Mallya: Kitu gani kingine walikufahamisha au Kumpatia
Shahidi: alikuwa anashuhudia wakati wanaingia ndani ya Nyumba yako
Walichukua Hati ya Uwanja
Shahidi: walisema walichukua Begi, Vyeti vyake vya Kijeshi vya Adamu walichukua Kadi ya pikipiki
Shahidi: aliongozana na Mkuu wa Upelelezi wa Chalinze
Mallya: Kitu gani Kingine alikwambia
Mallya: aliyeongozana na Mkuu wa Upelelezi wa Chalinze alikuwa ni ameongozana na akina nani
Shahidi: Jirani yangu aliongozana na Mkuu wa Upelelezi na aliacha namba ya Simu kwa Jirani,
Jaji: kwa ajili ya Nini
Shahidi: alisema Kama Kuna Lolote ambalo hajalielewa ampigie
Mallya: Siku ya Jumapili 08 Mwezi 09 Jumapili, Nyumba imesachiwa na Umekuta namba ya simu ya Mkuu wa Upelelezi Chalinze kitu gani Kilifuata baada ya hapo
Mallya: alikufahamisha kuwa alipigiwa Simu na nani..?
Shahidi: nilimpigia Simu,yeye aliniambia kuwa alipigiwa tuh simu kuwa inabidi waongozane kwenda Kusachi kwenye Nyumba ya Adamu Kasekwa
Jaji: labda nisikilize Mawakili
Mallya: Mheshimiwa Jaji naomba tubreak Kidogo kwa Sababu Shahidi akitumia Sana Nguvu anaweza akupoteza Energy na huenda akawa na siku Ndefu
Jaji: Mnasikia au Mvua inasababisha Kupoteza Usikivu tuhairishe kidogo.?
Jaji: upande wa Serikali
Jaji: kama Mvua imeacha Kidogo, Hebu tuendelee Kidogo ,Ikirudi na tukashindwa ,Tutaharishi
Wakili wa Serikali: hatuna Pingamizi
Jaji: uliishia Kuhusu kumpigia simu Mkuu wa Upelelezi Chalinze
Mallya: nilimuuliza Mkuu wa Upelelezi alijibu Kitu gani
Shahidi: alisema amepigiwa simu Kutoka Moshi
Jaji: naona Mvua haituoi Muda wa kuendelea,siwezi Kukadiria kwa muda gani, Kwa muda Mchache nahairisha Shauri
Jaji anatoka Nje
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021,Jamuhuri dhidi ya Halfan Bwire,Adam Hassana Kasekwa (Adamoo), Mohammed Abdalah Ling'wenya na Freeman Aikael Mbowe
Kesi inatajwa
Jaji amerejea Mvua Imekatika Sasa
Jaji: wakili John Mallya tuendelee
Mallya: Baada ya Kuwa ameshakwambia kuwa alipigiwa simu Kutoka Moshi kitu gani kilifuata
Jaji: Tunasikilizana, kama Mvua Inanisubiri Mimi, (Imeanza Kunyesha)
Mallya: Kesho yake ikawaje?
Shahidi: Muda ulikuwa umeshaenda, nikasema itabidi Kesho yake niende kwa sababu sikuamini alichoniambia
Mallya: Ulisema Ulienda Kituoni kesho yake wapi
Shahidi: Kituo cha Chalinze
Jaji: sasa ilikuwa Jumatatu
Shahidi: Nikaomba Kuonana na Mpelelezi,Nilipo muina nikajitambulisha Kuwa Mimi ni Yule Dada qmbaye Mmekuja Nyumbani Kusachi
Mallya: akakwambiaje?
Mallya: tarehe 05 Umepigia Umemkosa, Tarehe 09 ukakuta umesachiwa, Kitu gani kilitokea Tarehe 10 Ya Jumatatu pale Kituoni?
Mallya: Wewe ulikuwa unafanya Jitaihada gani zingine
Sina ninachokujua Zaidi
Shahidi: akasema kama nilivyokueleza sina ambacho nakijua zaidi ya Kuchukuliwa na kuwasindikiza Kwenda Nyumbani Kwako
Shahidi: nilianza kutafuta namba za Mke wa Ling'wenya
Mallya: awali ulituambia namba za Ling'wenya ulikuwa nazo na Ukampigia, za Mke wake unazitafuta, Za Ling'wenya ulitoa wapi
Shahidi: ni Mtu wa Karibu wa Mme wangu, Rafiki yake tuseme siku wanaondoka walikuwa naye
Mallya: ulitumia Njia gani za Kupata namba za Mke wa Ling'wenya?
Jaji: Mwenzao Kwamba alikuwa Askari Jeshi
Shahidi: nilimtafuta Mwenzao SHIKUNZI aliyekuwa anaishi nao Kimara
Mallya: alikuwa kimara aanakaa na nani
Shahidi: Ndiyo
Shahidi: alikuwa anakaa karibu na Ling'wenya
Shahidi: Nilitaka kumuuliza Mke wa Ling'wenya ili Kumuuliza huko kwake ni nini kilikuwa kinaendelea.?
Mallya: kikichokufanya Umtafute SHIKUNZI ili umtafute Mke wa Ling'wenya ni nini.?
Jaji: Kwanini ukimtafuta SHIKUNZI?
Mallya: SHIKUNZI akafanyeje..?
Shahidi: walikuwa ni Majirani
Shahidi: alinipatia namba ya Mke wa Ling'wenya
Shahidi: nilimpigia Mke wa Ling'wenya
Mallya: ulifanya hatua gani?
Mallya: nini kilifuata baada ya hapo
Shahidi: akaniambia baada ya hapo walienda Kwa Mwingine anaitwa Bwire, tumtafute Mke wa Bwire
Iliku ya siku ya Jumatatu, na yeye akaniambia Siku ya Jumapili ambayo ni Jana yake walienda Nyumbani Kwake wakafanya Upekuzi
Nikamwambia wewe huko Jirani huko Mtafute Mke wa Bwire
Shahidi: kwamba nilitaka Kujua kama kwake walienda kusachi akaniambia Wameenda kusachi, akaniambia pia tutafute Mke wa Bwire
Mallya: Kitu gani alikueleza Mke wa Ling'wenya
Shahidi: Mke wa Bwire anaitwa mama Itham na Mke wa Ling'wenya anaitwa Mama Somoye
Mallya: ulipata namba ya Mke wa Bwire na Unaweza kukumbuka Majina yao
Mallya: nini Kinafuata
Shahidi: Mke wa Bwire alikuwa Dar es salaam anakasema Inabidi nitoke Chalinze nije Dar es salaam
Jaji: alisema utoke wapi?
Mallya: hii sintofahamu yote ilitokana na nini
Shahidi: Kutokana na kuto kujua Mwenza wangu yupo wapi,namtafuta simpati alafu Nyumbani wamekuja Kusachi
Shahidi: Chalinze ni Dar es salaam
Mallya: ilikuwa lini.?
Shahidi: Nilitafuta Nauli nikaja Dar es salaam
Mallya: baada ya Kushauriwa Ulichukua hatua gani
Shahidi: Sikumbuki
Mallya: Baada ya Kufika Dar es salaam nini Kilifuata
Mallya: unaweza Kujua Nyumbani Kwake Bwire
Shahidi: Maeneo ya Temeke
Shahidi: tulishauriana tuanze Kutafuta Vituo Vyote vya Polisi
Mallya: Ndiyo
Mallya: Unaweza kukumbuka mlianzia Wapi
Shahidi: Kituo cha Polisi CHANG'OMBE
Shahidi: Polisi wa zamu
Mallya: mlikumkuta Polisi gani?
Shahidi: Tukajitambulisha kuwa sisi Wame zetu Wamekamatwa hatujui wamepelekwa Kituo gani
Mallya: Mkajitambulishaje?
Shahidi: Kwa Majina yetu na Waume zetu
Mallya: baada ya hapo yule Askari alifanyeje?
Shahidi? akaanza kupekua Kitabu kwa kuangalia yale Majina ya waume zetu hatukuyaona
Ndo maana hukuwa jaji..... uwiano utaujua wapi na wewe kazi kuimba CCM mbele kwa mbele!!!Maswali na majibu hayana uwiano.
Mimi sio mtumwa wa chama chochote humu wala sio mtumwa wa kiongozi wa chama chochote nachangia mada kadri ninavyoona inanipendeza,fuatilia coments zangu utaona.Ndo maana hukuwa jaji..... uwiano utaujua wapi na wewe kazi kuimba CCM mbele kwa mbele!!!
Usiwe unakurupuka kudandia vitu ambavyo hujui vimeanzia wapi!Pamoja na awareness yooooteeee hii kuhus PGO bado unauliza swali rubbish kama hili au unadhani PGO ni kwa ajili ya kukandamizia ukiwa unaamwandikisha maelezo mtuhumiwa? Mungu tusaidie!!!
Walishajikoroga. Walidai waliwapeleka vituo vya polisi wakati Detention Registry zote hawapo. Sasa watapachikaje majina hiyo tar 5/8/2020 Ilishapita??Kesi Hii Ni Kimeo Kwa Jamhuri Mbona Wanashupuza tu Shingo!!!! Hawajagundua Wako Uchi...time will tell ebu tuwe wapole.
Mkuu huelewi nini sasa hapo. Kuandika papo kwa papo kitu kinachozungum$wa na watu wengine kunahitaji speed kali na kichwani pia ziwe zinachaji. Sisi tunaelewa vizuri tu.Maswali na majibu hayana uwiano.
kwanza hata ivo anajitahidi,tushukuru hata kwa hicho kidogo kinachopatikanaMkuu huelewi nini sasa hapo. Kuandika papo kwa papo kitu kinachozungum$wa na watu wengine kunahitaji speed kali na kichwani pia ziwe zinachaji. Sisi tunaelewa vizuri tu.