Wewe naona umejiunga na JF wakati huu wa uelewa mdogo wa polisi kuhusu PGO je na wewe unauelewa mdogo kiasi chao
mkuu unapoteza muda kumjibu mtu kajiunga JF juzi?????
Screenshot_2021-09-29-11-29-35-73.jpg
 
Hii ndio taarifa iliyotufikia , kwamba leo Mke wa Mshitakiwa aliyeteswa kinyama komando Adam kasekwa leo atapanda kizimbani akiwa ni shahidi wa tatu wa upande wa utetezi katika kesi ndogo ndani ya kesi kubwa inayomkabili Freeman Mbowe na Wenzake watatu

Endelea kufuatilia

========

Saa 3 na Dakika 11 Tupo Chumba Cha Mahakama Tayari, Kwa Mawakili wa Utetezi wapo tayari Mahakamani ila Mshitaka bado wapo Nje

Jaji: ameshaingia Sasa Mahakamani

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021, Jamuhuri dhidi ya Halfan Bwire,Adam Hassana Kasekwa (Adamoo), Mohammed Abdalah Ling'wenya na Freeman Aikael Mbowe

Kesi inatajwa

Jaji: Habarini za Asubuhi, Tuendeleeni ni Siku Nyingine

Jaji: sawa

Wakili wa Serikali: naomba Radhi tumeingia wakati umeshaingia

Jaji: Wakili wa Serikali

Wakili wa Serikali: Kidando anatambulisha wenzake
Robert Kidando
2. Nassoro Katuga
3. Ignas Mwanuka
4. Esther Martin
5. Tulimanywa Majigo


Jaji: Utetezi

Kibatala: anatambulisha Wenzake

Advocate Peter Kibatala
Advocate Jonathan Mndeme
Advocate Fredrick Kiwhelo
Advocate John Malya
Advocate Sisty Aloyce
Advocate Alex Masaba
Advocate Idd Msawanga
Advocate Gaston Garubindi
Advocate Evaresta Kisanga
Advocate Faraj Mangula
Advocate Maria Mushi
Advocate Bonifasia Mapunda

Wakili Dickson Matata anaombewa Ruhusa Mdogo wake anafanyiwa Operesheni Hospitali ya Lugalo

Jaji: Wakili wa Serikali

Jaji: John Mallya

Wakili wa Serikali: Tumekuja kwa ajili ya kesi Ndogo ambapo Shahidi wa tatu yupo tayari kuendelea Kutoa Ushahidi wake

Mallya: Tunaye Shahidi, Na Shahidi yupo tayari kutoa Ushahidi

Shahidi: Mdada anatokea Nyuma kabisa ya Chumba Cha Mahakama anaenda Kizimbani

Jaji: Shahidi wa tatu upande wa Utetezi ambaye ameandaliwa Tafadhali anaweza Kuja

Jaji: anaandika Kidogo na Ukimya wa Mahakama

Jaji: Shahidi unaitwa nani

Jaji: Shahidi upo Mahakamani ondoa Hofu, nitakuuliza Majina yako na Nitakuapisha, Wakili wa Utetezi atakuongoza na Mawakili wengine watakuuliza Swali na Mawakili wa Serikali watakuuliza Maswali pia huna Haja ya Kuogopa, tupo hapa kutafuta Haki

Shahidi: Lilian Kibona
Dini Mkristo

Jaji: wakili Mallya endelea

Jaji: Liliani utachagua Kukaa au Kusimama,Hata Ukikaaa nitakuona

Shahidi: Naapa Mbele ya Mahakama hii kuwa Ushahidi nitakao toa utakuwa Ukweli na Ukweli Mtupu , Mungu ni Saidie

Mallya: Shahidi Unaishi wapi

Shahidi: Chalinze Mkoa wa Pwani

Shahidi: Ramboni

Mallya: sehemu gani huko Chalinze,

Jaji: ni Mtaa.?

Mallya: Unaishi na nani..?

Shahidi: Ndiyo

Shahidi: Na mmewangu na Watoto ambaye kwa Sasa Mme wangu ameshikiliwa

Shahidi: Ndiyo

Jaji: ni Miongoni Mwa washitakiwa ??

Mallya: Mme wako anaitwa nani.?

Mallya: hapa kila nikiwa namuita Mshitakiwa wa Pili nitakuwa namaanisha pia ni yeye
]
Shahidi: ndiyo

Shahidi: Adamu Khalfani Kasekwa

Mallya: Ndoa Ya Kiserikali

Mallya: Mmeona lini 05 08 2016

Shahidi: Ndiyo

Shahidi: Palepale Chalinze

Mallya: Mlikuwa mnaishi wapi

Mallya: unaweza Kukumbuka Mmewako alikuwa anafanya kazi gani wakati huo

Mallya: alikuwa anafanya kazi gani Nyingine

Shahidi: Askari jeshi wa JWTZ kikosi cha 92 Ngerengere

Shahidi: alikuwa hana kazi Nyingine zaidi ya hiyo ya Serikali

Mallya: naruka nakuja 2020 Mme wako alikuwa anafanya kazi gani

Shahidi: alikuwa anafanya shughuli zake za Biashara

Mallya: Kabla ya Kwenda Moshi mlikuwana Hali gani kati yako na Mme wako

Mallya: Mwanzoni Mwa Mwezi wa Nane Mwaka 2020 unakumbuka Kilitokea Kitu gani kati yako na Mme wako

Shahidi: Mme wangu alikuwa Moshi, tulikuwa tunawasiliana naye Vizuri

Shahidi: Palikuwa na Mawasiliano

Shahidi: Rafiki yake Ling'wenya waliwasiliana kuwa kuna Kazi imepatikana Moshi

Mallya: kabla ajaenda Moshi kitu gani kilitokea

Shahidi: Hapana sikumbuki

Mallya: Unaweza Kukumbuka Siku na Saa ya hayo mawasiliano

Jaji: unasema palikiwa na Mawasiliano Kati ya Mme wako na Ling'wenya .?

Jaji: Ndiyo

Shahidi: Ndiyo Kwamba Ling'wenya alimpigia Simu kuwa kuna kazi Imepatikana Moshi

Mallya: Simu zilikuwa zinapigwa kati ya Ling'wenya na Mme wako wewe ulijuaje

Mallya: Jambo gani lilifanyika, kabla ya Mme wako kwenda Moshi

Mimi kama Mke nilimruhusu

Shahidi: Mimi Kama Mke wake alinishirikisha

Mallya: Hali ya Mme wako ki Afya Wakati anaenda Moshi hali yake ilikuwaje

Shahidi: Nakumbuka walikutana na Ling'wenya wakaemda Kwanza Morogoro, Wakarudi, Waliporudi wakajiandaa Wakaenda Moshi

Shahidi: aumwi na Kwamba anaweza Kwenda Moshi

Shahidi: Ilikuwa Nzuri inamruhusu kwenda Kufanya kazi

Mallya: Hali Nzuri unamaanisha nini , Mwambie Mheshimiwa Jaji

Mallya: mlikuwa mnatumia Njia gani kufanya mazungumzo

Shahidi: alinitaarifu kuwa amefika Moshi

Mallya: kitu gani kilifuata baada ya Kwenda Moshi

Mallya: Siku ya Tarehe 05 08 2020 kitu gani kilitokea

Shahidi: alinipigia na akaongea na watoto, tulipokuwa tunaongea akasema Hebu subiri nikamsubiri

Shahidi: kwa Njia ya Simu

Mallya: kitu gani Kilifuata

Mallya: ilikuwa Saa ngapi Kama Saa Moja

Mallya: alipokwambia Subiri kidogo nitakupigia Kidogo

Shahidi: Sikumbuki Kichwani lakini ipo kwenye Simu yangu

Shahidi: Nilipoona Muda umeenda ilipofika Saa 10 ilibidi nimpigie,Simu iliita ikawa imepokelewa lakini Kina nikisema Hallo Sisikii Mtu akiongea

Mallya: Unaweza Kukumbuka namba ya Simu uliyopiga ambayo ulipiga Ikapokelewa.?

Mallya: Baadae kilifuata nini baada ya Simu kutokupelewa

Mallya: kitu gani Kilifuata

Shahidi: baadae Ikawa haipatikani

Mallya: baada ya Kumpigia Ling'wenya.?

Shahidi: kwakuwa nilikuwa na namba ya Mwenzake Ling'wenya nikampigia Ling'wenya

Mallya: Sasa wewe ilipata hisia gani baada ya kuona Inaita hadi Kesho yake haipokelewi

Shahidi: niliona labda ni Mambo ya Kazi, sikuwa na wasiwasi wowote

Shahidi: Ikawa ainaita Mpaka jioni ,Mpaka Usiku ,Mpaka Kesho yake inaita haipokelewi

Shahidi: Wewe ulichukua hatua gani..?

Shahidi: Sikuwa na mtu Mwingine yoyote wa akumuuliza Zaidi ya Ling'wenya

Mallya: Baada ya hapo Kitu gani Kilifuata baada ya kuhisi ni Mambo ya kazi

Shahidi: Miaka 3 na Miezi 9

Shahidi: Sikuwa na namna yoyote zaidi ya Kusubiri simu kutoka kwao

Mallya: Una mtoto unesema anaumri gani?

Shahidi: nakumbuka ilikuwa 09 08 Mwaka 2020 niliamka Asubuhi ikiwa siku ya Jumapili, Mtoto alikuwa anasumbuliwa na tumbo

Jaji: Mtoto wa Jinsia gani

Mallya: Nataka kukupeleka Tarehe 09 Mwezi 08 kitu gani Kilitokea

Mallya: kwanini Unakumbuka kuwa ilikuwa Siku ya Jumapili

Shahidi: Wakike

Shahidi: Sababu ilikuwa Siku ya Ibada

Shahidi: Sikwenda Ibadani badala yake nikaenda Hospitali

Mallya: ikawaje huko Hospitali

Mallya: Ikawaje

Shahidi: Nilipokelewa

Mallya: Hospitali gani

Shahidi: Hospitali ya Serikali palepale Chalinze

Mallya: baada ya Kupokelewa Hospitali

Shahidi: nilipatiwa Huduma nikarudi Nyumbani

Mallya: Ule Mlango ulikuwa katika hali gani

Mallya: baada ya Kurudi Nyumbani niliona Miguu ya watu kama Imekanyaga, Wakati natoka Nyumbani nilifunga Mlango lakini niliporudi nikakuta Milango ipo wazi

Shahidi: Mlango ulikuwa wazi na Kitasa nikakuta kimevunjwa

Shahidi: kwa akili ya harakaharaka nilijua Wezi, Cha ajabu kila kitu nilikuta Vipo, Kitu kama Tv lakini vipo

Mallya: enheeee ikawaje

Mallya: kitu gani kikatokea

Jaji: Za Mme wako

Shahidi: zote zimemwaga,na Mabegi yamefunguliwa

Shahidi: Nikaingia Chumbani nikakuta Nguo za zimemwagwa Chini

Shahidi: Alinunua Congo Begi lenye Mabaka Mabaka ya Jeshi

Shahidi: Kuna begi alinunua Congo nilipokuja kikakuta halipo

Mallya: Jirani yako anaitwa nani.?

Mallya: Kitu gani kilifuata

Shahidi: Nilienda Kuuliza Majirani zangu

Shahidi: niliemda Kuuliza kama Mme wangu amekuja Nyumbani? wamemuona.? kwamba kunakitu huenda alikuja Kukitafuta kwa haraka haraka

Shahidi: Judith Charles

Mallya: lengo la kwenda kwa Jirani lilikuwa nini

Mallya: Jirani alikwambiaje

Jaji: Ndiyo

Shahidi: Kuna Magari yalikuja hapa Ya Kipolisi, Moja walikuwa wamevaa Sare na Wengine walikuwa Wamevaa Kiraia

Mallya: Taarifa Nyingine alikupa Jirani yako ni Ipi

Mallya: baada ya hapo Mapolisi walishuka kwenye gari wakaingia Ndani

Shahidi: kwamba Mapolisi walimuita kwa lengo la Kuniulizia Mimi

Mallya: yeye Jirani alikuwa anafanya nini wakati huo

Mallya: Kitu gani kingine walikufahamisha au Kumpatia

Shahidi: alikuwa anashuhudia wakati wanaingia ndani ya Nyumba yako

Walichukua Hati ya Uwanja

Shahidi: walisema walichukua Begi, Vyeti vyake vya Kijeshi vya Adamu walichukua Kadi ya pikipiki

Shahidi: aliongozana na Mkuu wa Upelelezi wa Chalinze

Mallya: Kitu gani Kingine alikwambia

Mallya: aliyeongozana na Mkuu wa Upelelezi wa Chalinze alikuwa ni ameongozana na akina nani

Shahidi: Jirani yangu aliongozana na Mkuu wa Upelelezi na aliacha namba ya Simu kwa Jirani,

Jaji: kwa ajili ya Nini

Shahidi: alisema Kama Kuna Lolote ambalo hajalielewa ampigie

Mallya: Siku ya Jumapili 08 Mwezi 09 Jumapili, Nyumba imesachiwa na Umekuta namba ya simu ya Mkuu wa Upelelezi Chalinze kitu gani Kilifuata baada ya hapo

Mallya:
alikufahamisha kuwa alipigiwa Simu na nani..?

Shahidi:
nilimpigia Simu,yeye aliniambia kuwa alipigiwa tuh simu kuwa inabidi waongozane kwenda Kusachi kwenye Nyumba ya Adamu Kasekwa

Jaji: labda nisikilize Mawakili

Mallya: Mheshimiwa Jaji naomba tubreak Kidogo kwa Sababu Shahidi akitumia Sana Nguvu anaweza akupoteza Energy na huenda akawa na siku Ndefu

Jaji: Mnasikia au Mvua inasababisha Kupoteza Usikivu tuhairishe kidogo.?

Jaji: upande wa Serikali

Jaji: kama Mvua imeacha Kidogo, Hebu tuendelee Kidogo ,Ikirudi na tukashindwa ,Tutaharishi

Wakili wa Serikali
: hatuna Pingamizi

Jaji: uliishia Kuhusu kumpigia simu Mkuu wa Upelelezi Chalinze

Mallya:
nilimuuliza Mkuu wa Upelelezi alijibu Kitu gani

Shahidi: alisema amepigiwa simu Kutoka Moshi

Jaji: naona Mvua haituoi Muda wa kuendelea,siwezi Kukadiria kwa muda gani, Kwa muda Mchache nahairisha Shauri


Jaji anatoka Nje



Kesi namba 16 ya Mwaka 2021,Jamuhuri dhidi ya Halfan Bwire,Adam Hassana Kasekwa (Adamoo), Mohammed Abdalah Ling'wenya na Freeman Aikael Mbowe

Kesi inatajwa

Jaji amerejea Mvua Imekatika Sasa



Jaji: wakili John Mallya tuendelee

Mallya: Baada ya Kuwa ameshakwambia kuwa alipigiwa simu Kutoka Moshi kitu gani kilifuata

Jaji: Tunasikilizana, kama Mvua Inanisubiri Mimi, (Imeanza Kunyesha)

Mallya: Kesho yake ikawaje?

Shahidi:
Muda ulikuwa umeshaenda, nikasema itabidi Kesho yake niende kwa sababu sikuamini alichoniambia

Mallya:
Ulisema Ulienda Kituoni kesho yake wapi

Shahidi
: Kituo cha Chalinze

Jaji: sasa ilikuwa Jumatatu

Shahidi: Nikaomba Kuonana na Mpelelezi,Nilipo muina nikajitambulisha Kuwa Mimi ni Yule Dada qmbaye Mmekuja Nyumbani Kusachi

Mallya: akakwambiaje?

Mallya: tarehe 05 Umepigia Umemkosa, Tarehe 09 ukakuta umesachiwa, Kitu gani kilitokea Tarehe 10 Ya Jumatatu pale Kituoni?

Mallya:
Wewe ulikuwa unafanya Jitaihada gani zingine

Sina ninachokujua Zaidi

Shahidi:
akasema kama nilivyokueleza sina ambacho nakijua zaidi ya Kuchukuliwa na kuwasindikiza Kwenda Nyumbani Kwako

Shahidi: nilianza kutafuta namba za Mke wa Ling'wenya

Mallya: awali ulituambia namba za Ling'wenya ulikuwa nazo na Ukampigia, za Mke wake unazitafuta, Za Ling'wenya ulitoa wapi

Shahidi: ni Mtu wa Karibu wa Mme wangu, Rafiki yake tuseme siku wanaondoka walikuwa naye

Mallya: ulitumia Njia gani za Kupata namba za Mke wa Ling'wenya?

Jaji: Mwenzao Kwamba alikuwa Askari Jeshi

Shahidi: nilimtafuta Mwenzao SHIKUNZI aliyekuwa anaishi nao Kimara

Mallya: alikuwa kimara aanakaa na nani

Shahidi: Ndiyo

Shahidi: alikuwa anakaa karibu na Ling'wenya

Shahidi: Nilitaka kumuuliza Mke wa Ling'wenya ili Kumuuliza huko kwake ni nini kilikuwa kinaendelea.?

Mallya: kikichokufanya Umtafute SHIKUNZI ili umtafute Mke wa Ling'wenya ni nini.?

Jaji: Kwanini ukimtafuta SHIKUNZI?

Mallya:
SHIKUNZI akafanyeje..?

Shahidi: walikuwa ni Majirani

Shahidi: alinipatia namba ya Mke wa Ling'wenya

Shahidi: nilimpigia Mke wa Ling'wenya

Mallya: ulifanya hatua gani?

Mallya: nini kilifuata baada ya hapo

Shahidi:
akaniambia baada ya hapo walienda Kwa Mwingine anaitwa Bwire, tumtafute Mke wa Bwire

Iliku ya siku ya Jumatatu, na yeye akaniambia Siku ya Jumapili ambayo ni Jana yake walienda Nyumbani Kwake wakafanya Upekuzi

Nikamwambia wewe huko Jirani huko Mtafute Mke wa Bwire

Shahidi: kwamba nilitaka Kujua kama kwake walienda kusachi akaniambia Wameenda kusachi, akaniambia pia tutafute Mke wa Bwire

Mallya: Kitu gani alikueleza Mke wa Ling'wenya

Shahidi:
Mke wa Bwire anaitwa mama Itham na Mke wa Ling'wenya anaitwa Mama Somoye

Mallya: ulipata namba ya Mke wa Bwire na Unaweza kukumbuka Majina yao

Mallya: nini Kinafuata

Shahidi
: Mke wa Bwire alikuwa Dar es salaam anakasema Inabidi nitoke Chalinze nije Dar es salaam

Jaji: alisema utoke wapi?

Mallya:
hii sintofahamu yote ilitokana na nini

Shahidi: Kutokana na kuto kujua Mwenza wangu yupo wapi,namtafuta simpati alafu Nyumbani wamekuja Kusachi

Shahidi:
Chalinze ni Dar es salaam

Mallya: ilikuwa lini.?

Shahidi: Nilitafuta Nauli nikaja Dar es salaam

Mallya: baada ya Kushauriwa Ulichukua hatua gani

Shahidi: Sikumbuki

Mallya: Baada ya Kufika Dar es salaam nini Kilifuata

Mallya:
unaweza Kujua Nyumbani Kwake Bwire

Shahidi: Maeneo ya Temeke

Shahidi:
tulishauriana tuanze Kutafuta Vituo Vyote vya Polisi

Mallya
: Ndiyo

Mallya: Unaweza kukumbuka mlianzia Wapi

Shahidi: Kituo cha Polisi CHANG'OMBE

Shahidi: Polisi wa zamu

Mallya:
mlikumkuta Polisi gani?

Shahidi: Tukajitambulisha kuwa sisi Wame zetu Wamekamatwa hatujui wamepelekwa Kituo gani

Mallya:
Mkajitambulishaje?

Shahidi:
Kwa Majina yetu na Waume zetu

Mallya: baada ya hapo yule Askari alifanyeje?

Shahidi?
akaanza kupekua Kitabu kwa kuangalia yale Majina ya waume zetu hatukuyaona
Kesi hii si mchezo asee
 
Ndo maana hukuwa jaji..... uwiano utaujua wapi na wewe kazi kuimba CCM mbele kwa mbele!!!
Mimi sio mtumwa wa chama chochote humu wala sio mtumwa wa kiongozi wa chama chochote nachangia mada kadri ninavyoona inanipendeza,fuatilia coments zangu utaona.
Maswali na majibu haviendani labda huenda mwandishi anashindwa kuendana na kasi ya mazungumzo ya mahakamani.
 
Pamoja na awareness yooooteeee hii kuhus PGO bado unauliza swali rubbish kama hili au unadhani PGO ni kwa ajili ya kukandamizia ukiwa unaamwandikisha maelezo mtuhumiwa? Mungu tusaidie!!!
Usiwe unakurupuka kudandia vitu ambavyo hujui vimeanzia wapi!
 
aisee kumbe Majaji na Mahakimu wanakazi sana!
nauliza tu haya maneno yote wanarekodi kwa mkono au mashine?
na yanaandikwa kwa lugha ya kiswahili au kizungu?!
kama ni kwa kizungu inamaana wanatafsiri muda gani?! yaani wanatafasiri wenyewe au wanatafasiriwa?!
hii kazi yote ya nini, kwani haiwezekani kuandikwa kwa lugha ya Taifa?
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom