Dah..aisee wake zetu hawa wanatupenda sana (sio wote).huyo dada anavyoeleza kampelekea jamaa shuka na chakula na sabun aisee nimehis kulengwa machozi nikakumbuka 2019 nimeugua ghafla nikiwa kwenye mishe zangu town nikaingizwa emergency Temeke hospital wife kaja na na nguo sijui hata alijuaje maana nilizovaa nilichafua chufua kwa kutapika.Mungu wabariki wanawake
 
Karibuni hapa kwa updates kutoka mahakama ya uhujumu uchumi kwenye kesi namba 16 ya mwaka 2021 inayomuhusu mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu...

Watuhumiwa tayari wamefikishwa mahakamani, leo shahidi wa tatu upande wa utetezi ataanza kutoa ushahidi wake.

View attachment 1956923

Mawakili upande wa Utetezi tayari wapo katika ukumbi wa Mahakama. Mawakili upande wa Mashtaka bado wapo Nje.

-------------------------------------------------------------------------​

Jaji ameshaingia Sasa Mahakamani, kesi inatajwa.

Wakili wa Serikali: naomba radhi tumeingia wakati umeshaingia

Jaji: sawa

Wakili wa Serikali: Kidando Wakili wa Serikali anatambulisha wenzake
1. Robert Kidando​
2. Nassoro Katuga​
3. Ignas Mwanuka​
4. Esther Martin​
5. Tulimanywa Majigo​

Kibatala: anatambulisha Wenzake
Adv. Peter Kibatala​
Adv. Jonathan Mndeme​
Adv. Fredrick Kiwhelo​
Adv. John Malya​
Adv. Sisty Aloyce​
Adv. Alex Masaba​
Adv. Idd Msawanga​
Adv. Gaston Garubindi​
Adv. Evaresta Kisanga​
Adv. Faraj Mangula​
Adv. Maria Mushi​
Adv. Bonifasia Mapunda​

Wakili Dickson Matata: anaombewa Ruhusa Mdogo wake anafanyiwa Operesheni Hospitali ya Lugalo

Jaji: Wakili wa Serikali

Wakili wa serikali: Tumekuja kwa ajili ya kesi ndogo ambapo Shahidi wa tatu yupo tayari kuendelea Kutoa Ushahidi wake

Jaji: John Mallya

Mallya: Tunaye, na Shahidi yupo tayari kutoa Ushahidi

Jaji: anaandika Kidogo na Ukimya wa Mahakama

Jaji: Shahidi wa 3 upande wa Utetezi ambaye ameandaliwa Tafadhali anaweza Kuja

Shahidi Mdada anatokea Nyuma kabisa ya Chumba Cha Mahakama anaenda Kizimbani

Jaji: Shahidi upo Mahakamani ondoa Hofu, nitakuuliza Majina yako na Nitakuapisha, Wakili wa Utetezi atakuongoza na Mawakili wengine watakuuliza Swali na Mawakili wa Serikali watakuuliza Maswali, pia huna Haja ya Kuogopa, tupo hapa kutafuta Haki.

Jaji: Shahidi unaitwa nani

Shahidi: Lilian Kibona, Dini Mkristo Shahidi Naapa Mbele ya Mahakama hii kuwa Ushahidi nitakao toa utakuwa Ukweli na Ukweli Mtupu, Mungu ni Saidie.

Jaji: Liliani utachagua Kukaa au Kusimama, Hata Ukikaaa nitakuona.

Jaji: wakili Mallya endelea

Mallya: Shahidi Unaishi wapi

Shahidi: Chalinze Mkoa wa Pwani

Mallya: sehemu gani huko Chalinze

Shahidi: Ramboni

Jaji: ni Mtaa.?

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Unaishi na nani..?

Shahidi: Na mme wangu na Watoto ambaye kwa Sasa Mme wangu ameshikiliwa.

Jaji: ni Miongoni Mwa washitakiwa?

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Mme wako anaitwa nani?

Shahidi: Adamu Khalfani Kasekwa

Mallya: hapa nitakuwa namuita Mshitakiwa wa Pili nitakuwa namaanisha pia ni yeye

Shahidi: ndiyo

Mallya: Mmeoana lini, 05/08/2016, Ndoa Ya Kiserikali

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Mlikuwa mnaishi wapi

Shahidi: Pale pale Chalinze

Mallya: unaweza Kukumbuka Mme wako alikuwa anafanya kazi gani wakati huo

Shahidi: Askari Jeshi la JWTZ, kikosi cha 92 Ngerengere

Mallya: alikuwa anafanya kazi gani Nyingine

Shahidi: alikuwa hana kazi Nyingine zaidi ya hiyo ya Serikali

Mallya: naruka nakuja 2020 Mme wako alikuwa anafanya kazi gani

Shahidi: alikuwa anafanya shughuli zake za Biashara

Mallya: Mwanzoni Mwa Mwezi wa Nane Mwaka 2020 unakumbuka Kilitokea Kitu gani kati yako na Mme wako

Shahidi: Mme wangu alikuwa Moshi, tulikuwa tunawasiliana naye Vizuri

Mallya: Kabla ya Kwenda Moshi mlikuwa na Hali gani kati yako na Mme wako

Shahidi: Palikuwa na Mawasiliano

Mallya: kabla hajaenda Moshi kitu gani kilitokea

Shahidi: Rafiki yake Ling'wenya waliwasiliana kuwa kuna Kazi imepatikana Moshi

Mallya: Unaweza Kukumbuka Siku na Saa ya hayo mawasiliano

Shahidi: Hapana sikumbuki

Jaji: unasema palikiwa na Mawasiliano Kati ya Mme wako na Ling'wenya .?

Shahidi: Ndiyo Kwamba Ling'wenya alimpigia Simu kuwa kuna kazi Imepatikana Moshi

Jaji: Ndiyo

Mallya: Simu zilikuwa zinapigwa kati ya Ling'wenya na Mme wako, wewe ulijuaje

Shahidi: Mimi Kama Mke wake alinishirikisha, Mimi kama Mke nilimruhusu

Mallya: Jambo gani lilifanyika, kabla ya Mme wako kwenda Moshi

Shahidi: Nakumbuka walikutana na Ling'wenya wakaenda Kwanza Morogoro, Wakarudi, Waliporudi wakajiandaa Wakaenda Moshi

Mallya: Hali ya Mme wako kiAfya Wakati anaenda Moshi hali yake ilikuwaje

Shahidi: Ilikuwa Nzuri inamruhusu kwenda Kufanya kazi

Mallya: Hali Nzuri unamaanisha nini ,Mwambie Mheshimiwa Jaji

Shahidi: haumwi na Kwamba anaweza Kwenda Moshi

Mallya: kitu gani kilifuata baada ya Kwenda Moshi

Shahidi: alinitaarifu kuwa amefika Moshi

Mallya: mlikuwa mnatumia Njia gani kufanya mazungumzo

Shahidi: kwa Njia ya Simu

Mallya: Siku ya Tarehe 05/08/2020 kitu gani kilitokea

Shahidi: alinipigia na akaongea na watoto, tulipokuwa tunaongea akasema Hebu subiri nikamsubiri

Mallya: ilikuwa Saa ngapi

Shahidi: Kama Saa Moja

Mallya: alipokwambia Subiri kidogo nitakupigia Kidogo kitu gani Kilifuata

Shahidi: Nilipoona Muda umeenda ilipofika Saa 10 ilibidi nimpigie, Simu iliita ikawa imepokelewa lakini Kila nikisema Hallo Sisikii Mtu akiongea

Mallya: Unaweza Kukumbuka namba ya Simu uliyopiga, ambayo ulipiga Ikapokelewa.?

Shahidi: Sikumbuki Kichwani lakini ipo kwenye Simu yangu

Mallya: Baadae kilifuata nini baada ya Simu kutokupokelewa

Shahidi: baadae Ikawa haipatikani

Mallya: kitu gani Kilifuata

Shahidi: kwa kuwa nilikuwa na namba ya Mwenzake Ling'wenya nikampigia Ling'wenya

Mallya: baada ya Kumpigia Ling'wenya.?

Shahidi: Ikawa inaita Mpaka jioni, Mpaka Usiku, Mpaka Kesho yake inaita haipokelewi

Mallya: Sasa wewe ulipata hisia gani baada ya kuona Inaita hadi Kesho yake haipokelewi

Shahidi: niliona labda ni Mambo ya Kazi, sikuwa na wasiwasi wowote

Mallya: Wewe ulichukua hatua gani..?

Shahidi: Sikuwa na namna yoyote zaidi ya Kusubiri simu kutoka kwao

Mallya: umesema una mtoto, anaumri gani

Shahidi: Miaka 3 na Miezi 9

Mallya: Nataka kukupeleka Tarehe 09 Mwezi 08 kitu gani Kilitokea

Shahidi: nakumbuka ilikuwa tarehe 09 mwezi 08 Mwaka 2020 niliamka Asubuhi ikiwa siku ya Jumapili, Mtoto alikuwa anasumbuliwa na tumbo

Jaji: Mtoto wa Jinsia gani

Shahidi: Wa kike

Mallya: kwanini Unakumbuka kuwa ilikuwa Siku ya Jumapili

Shahidi: Sababu ilikuwa Siku ya Ibada

Mallya: Ikawaje

Shahidi: Sikwenda Ibadani badala yake nikaenda Hospitali

Mallya: ikawaje huko Hospitali

Shahidi: Nilipokelewa

Mallya: Hospitali gani

Shahidi: Hospitali ya Serikali pale pale Chalinze

Mallya: baada ya Kupokelewa Hospitali

Shahidi: nilipatiwa Huduma nikarudi Nyumbani

Mallya: baada ya Kurudi Nyumbani

Shahidi: niliona Miguu ya watu kama Imekanyaga, Wakati natoka Nyumbani nilifunga Mlango lakini niliporudi nikakuta Milango ipo wazi

Mallya: Ule Mlango ulikuwa katika hali gani

Shahidi: Mlango ulikuwa wazi na Kitasa nikakuta kimevunjwa

Mallya: kitu gani kikatokea

Shahidi: kwa akili ya haraka haraka nilijua Wezi, Cha ajabu kila kitu nilikuta Vipo, Kitu kama Tv lakini vipo

Mallya: enheeee ikawaje

Shahidi: Nikaingia Chumbani nikakuta Nguo zimemwagwa Chini

Jaji: Za Mme wako

Shahidi: zote zimemwaga,na Mabegi yamefunguliwa

Shahidi: Kuna begi la jeshi alinunua Congo nilipokuja nikakuta halipo

Jaji: ukisema begi la jeshi alinunua Congo unamaanisha nini

Shahidi: Alinunua Congo Begi lenye Mabaka Mabaka ya Jeshi

Mallya: Kitu gani kilifuata

Shahidi: Nilienda Kuuliza Majirani zangu

Mallya: Jirani yako anaitwa nani.?

Shahidi: Judith Charles

Mallya: lengo la kwenda kwa Jirani lilikuwa nini

Shahidi: nilienda Kuuliza kama Mme wangu amekuja Nyumbani.? wamemuona.? kwamba kuna kitu huenda alikuja Kukitafuta kwa haraka haraka

Mallya: Jirani alikwambiaje

Shahidi: Kuna Magari yalikuja hapa Ya Kipolisi, Moja walikuwa wamevaa Sare na Wengine walikuwa Wamevaa Kiraia

Mallya: Taarifa Nyingine alikupa Jirani yako ni Ipi

Shahidi: kwamba Mapolisi walimuita kwa lengo la Kuniulizia Mimi. baada ya hapo Mapolisi walishuka kwenye gari wakaingia Ndani

Mallya: yeye Jirani alikuwa anafanya nini wakati huo

Shahidi: alikuwa anashuhudia wakati wanaingia ndani ya Nyumba yako

Mallya: Kitu gani kingine walikufahamisha au Kumpatia

Shahidi: walisema walichukua Begi, Vyeti vyake vya Kijeshi vya Adamu, Walichukua Hati ya Uwanja, Kadi ya pikipiki

Mallya: Kitu gani Kingine alikwambia

Shahidi: aliongozana na Mkuu wa Upelelezi wa Chalinze

Mallya: aliyeongozana na Mkuu wa Upelelezi wa Chalinze alikuwa ameongozana na akina nani

Shahidi: Jirani yangu aliongozana na Mkuu wa Upelelezi na aliacha namba ya Simu kwa Jirani.

Jaji: kwa ajili ya Nini

Shahidi: alisema Kama Kuna Lolote ambalo hajalielewa ampigie

Mallya: Siku ya Jumapili 08 Mwezi 09 Nyumba imesachiwa na Umekuta namba ya simu ya Mkuu wa Upelelezi Chalinze, kitu gani Kilifuata baada ya hapo

Shahidi: nilimpigia Simu,yeye aliniambia kuwa alipigiwa tu simu kuwa inabidi waongozane kwenda Kusachi kwenye Nyumba ya Adamu Kasekwa

Mallya: alikufahamisha kuwa alipigiwa Simu na nani..?

Jaji: Mnasikia au Mvua inasababisha Kupoteza Usikivu tuhairishe kidogo.?

Jaji: labda nisikilize Mawakili

Mallya: Mheshimiwa Jaji naomba tubreak Kidogo kwa Sababu Shahidi akitumia Sana Nguvu anaweza kupoteza Energy na huenda akawa na siku Ndefu

Jaji: upande wa Serikali

Wakili wa Serikali: hatuna Pingamizi

Jaji: kama Mvua imeacha Kidogo, Hebu tuendelee Kidogo, Ikirudi na tukashindwa ,Tutaahirisha

Jaji: uliishia Kuhusu kumpigia simu Mkuu wa Upelelezi Chalinze

Mallya: nilimuuliza Mkuu wa Upelelezi alijibu Kitu gani

Shahidi: alisema amepigiwa simu Kutoka Moshi

Jaji: naona Mvua haitupi Muda wa kuendelea, siwezi Kukadiria kwa muda gani. Kwa muda Mchache nahairisha Shauri, Jaji anatoka Nje.

--------------------------------------------------------​

Jaji amerejea Mvua Imekatika Sasa Kesi inatajwa Kesi namba 16 ya Mwaka 2021,Jamuhuri dhidi ya Halfan Bwire, Adam Hassan Kasekwa (Adamoo), Mohammed Abdalah Ling'wenya na Freeman Aikael Mbowe

Jaji: wakili John Mallya tuendelee

Mallya: Baada ya Kuwa ameshakwambia kuwa alipigiwa simu Kutoka Moshi kitu gani kilifuata

Shahidi: Muda ulikuwa umeshaenda , nikasema itabidi Kesho yake niende kwa sababu sikuamini alichoniambia

Mallya: Kesho yake ikawaje

Jaji: Tunasikilizana, kama Mvua Inanisubiri Mimi, (Imeanza Kunyesha)

Mallya: Ulisema Ulienda Kituoni kesho yake wapi

Shahidi: Kituo cha Chalinze

Jaji: sasa ilikuwa Jumatatu

Mallya: tarehe 05 Umepigia Umemkosa, Tarehe 09 ukakuta kumesachiwa, Kitu gani kilitokea Tarehe 10 Ya Jumatatu pale Kituoni

Shahidi: Nikaomba Kuonana na Mpelelezi, Nilipo muona nikajitambulisha Kuwa Mimi ni Yule Dada ambaye Mmekuja Nyumbani Kusachi

Mallya: akakwambiaje

Shahidi: akasema kama nilivyokueleza sina ambacho nakijua zaidi ya Kuchukuliwa na kuwasindikiza Kwenda Nyumbani Kwako Kusachi,Sina ninachokijua Zaidi

Mallya: Wewe ulikuwa unafanya Jitihada gani zingine

Shahidi: nilianza kutafuta namba za Mke wa Ling'wenya

Mallya: awali ulituambia namba za Ling'wenya ulikuwa nazo na Ukampigia, za Mke wake unazitafuta, Za Ling'wenya ulitoa wapi

Shahidi: ni Mtu wa Karibu wa Mme wangu, Rafiki yake, tuseme siku wanaondoka walikuwa naye

Mallya: ulitumia Njia gani za Kupata namba za Mke wa Ling'wenya

Shahidi: nilimtafuta Mwenzao SHIKUNZI aliyekuwa anaishi nao Kimara

Jaji: Mwenzao, Kwamba alikuwa Askari Jeshi

Shahidi: Ndiyo

Mallya: alikuwa kimara anakaa na nani

Shahidi: alikuwa anakaa karibu na Ling'wenya

Mallya: kikichokufanya Umtafute SHIKUNZI ili umtafute Mke wa Ling'wenya ni nini.?

Shahidi: Nilitaka kumuuliza Mke wa Ling'wenya ili Kumuuliza huko kwake ni nini kilikuwa kinaendelea.?

Jaji: Kwanini hukumtafuta SHIKUNZI.?

Shahidi: walikuwa ni Majirani

Mallya: SHIKUNZI akafanyeje..?

Shahidi: alinipatia namba ya Mke wa Ling'wenya

Mallya: ulifanya hatua gani..?

Shahidi: nilimpigia Mke wa Ling'wenya Ilikuqa siku ya Jumatatu, na yeye akaniambia Siku ya Jumapili ambayo ni Jana yake walienda Nyumbani Kwake wakafanya Upekuzi

Mallya: nini kilifuata baada ya hapo

Shahidi: akaniambia baada ya hapo walienda Kwa Mwingine anaitwa Bwire, tumtafute Mke wa Bwire. nikamwambia wewe huko ni Jirani Mtafute Mke wa Bwire

Mallya: Kitu gani alikueleza Mke wa Ling'wenya

Shahidi: kwamba nilitaka Kujua kama kwake walienda kusachi akaniambia Wameenda kusachi, akaniambia pia tutafute Mke wa Bwire

Mallya: ulipata namba ya Mke wa Bwire na Unaweza kukumbuka Majina yao

Shahidi: Mke wa Bwire anaitwa mama Itham na Mke wa Ling'wenya anaitwa Mama Somoye

Mallya: nini Kinafuata

Shahidi: Mke wa Bwire alikuwa Dar es salaam anakasema Inabidi nitoke Chalinze nije Dar es salaam

Jaji: alisema utoke wapi.?

Shahidi: Chalinze nije Dar es salaam

Mallya: hii sintofahamu yote ilitokana na nini

Shahidi: Kutokana na kutokujua Mwenza wangu yupo wapi, namtafuta simpati alafu Nyumbani wamekuja Kusachi

Mallya: baada ya Kushauriwa Ulichukua hatua gani

Shahidi: Nilitafuta Nauli nikaja Dar es salaam

Mallya: ilikuwa lini.?

Shahidi: Sikumbuki

Mallya: Baada ya Kufika Dar es salaam nini Kilifuata

Shahidi: tulishauriana tuanze Kutafuta Vituo Vyote vya Polisi

Mallya: unaweza Kujua Nyumbani Kwake Bwire

Shahidi: Maeneo ya Temeke

Mallya: Unaweza kukumbuka mlianzia Wapi

Shahidi: Kituo cha Polisi CHANG'OMBE

Mallya: halafu

Shahidi: Tukajitambulisha kuwa sisi Waume zetu Wamekamatwa hatujui wamepelekwa Kituo gani

Mallya: mlimkuta Polisi gani

Shahidi: Polisi wa zamu

Mallya: Mkajitambulishaje..

Shahidi: Kwa Majina yetu na Waume zetu

Mallya: baada ya hapo yule Askari alifanyeje

Shahidi: akaanza kupekua Kitabu kwa kuangalia yale Majina ya waume zetu hatukuyaona

Mallya: Baada ya Kutoyaona Majina ya Mnaowatafuta Kitu gani Kilifuata

Shahidi: tulienda kituo Kingine

Mallya: Kituo gani

Shahidi: Central Police Dar es salaam

Mallya: Ikawaje

Shahidi: vile vile tukajitambukisha ya kwamba, sisi waume zetu wameletwa polisi na hatujui Kituo gani

Mallya: baada ya Kujitambulisha kwa Askari nini Kilifuata

Shahidi: aliangalia kile Kitabu hakuona yale Majina yetu

Mallya: wakati anaangalia Majina ya waume zenu Nyie Mlishiriki Vipi

Shahidi: Wakati anaangalia Kitabu, Wote tuliinama kuangalia Majina ya Waume zetu kwa usahihi

Mallya: Mmeangalia pamoja na Askari Majina ya wenza wenu hamjayaona, nini Kiliendelea baada ya hapi

Shahidi: tulitoka Kituo vha Polisi Central Police tukaenda Oysterbay, Tukajitambulisha kwa Askari wa zamu akaangalia kwenye kitabu, Majina yao, hayakwepo

Mallya: baada ya Kuwakosa Central nini kilifuata

Shahidi: tulienda Tazara

Mallya: unaweza Kueleza Kwanini Mlienda Tazara

Shahidi: tulienda kwa Sababu tulikuwa kwenye Kuendelea kuwatafuta Kituo gani cha Polisi wamepelekwa

Mallya: Unaweza Kuiambaia Mahakama mara zote mlipokuwa mnatafuta mlikuwa mnawatafuta kwa Namna gani

Shahidi: mara zote tunataja Majina na Mimi nilitaja Jina la Mme wangu Adamu Khalfani Kasekwa

Mallya: Kitu gani Kilifuata

Shahidi: Hatukuyaona Majina yao

Mallya: Mmeshaenda Vituo Vinne Kutafuta wenza wenu, hatua gani ilifuata baada ya hapo

Shahidi: Tulirudi Nyumbani kwa sababu Muda ulikuwa umeenda na tuliacha watoto wadogo

Mallya: Nyumbani kwa Maana Wapi

Shahidi: Kwa Mke wa Bwire

Mallya: kwa Mazungumzo yako na Mke wa Bwire alikwambia nini kimetokea Kule Moshi

Shahidi: akaniambia Kule Moshi kuna wifi yake ambaye ni Dada wa Mohammed Abdilah Ling'wenya

Jaji: twendeni Taratibu, Mmeshazunguka Vituo Vyote ilikuwa siku gani..?

Shahidi: Tarehe 13

Jaji: ooohhh tunakosa Mtiririko kwa sababu nilikuwa bado nipo kwenye Vituo Vya Polisi

Mallya: Samahani Mheshimiwa Jaji nilirudi Nyuma Kumuuliza kama waliongea na Mke wa Bwire

Mallya: alikwambia nini sasa

Shahidi: Kwamba Wifi yake amempigia Simu Kuwa Adam wakiwa Moshi na Mohamed, akiwa anakunywa Chai Adamu alikuwa anazungumza na Simu, ikawa kama kelele za Mvutano, Niache niache baada ya hapo wakawa wanamvuta Kumleta Sehemu za Vyakula sasa.

Mallya: Nini kilifuata

Shahidi: Kwamba alikuwa amepigwa akawa anavuja Damu

Jaji: hii ni Habari ambayo umesema Umeambiwa na Mke wa nani..?

Shahidi: Mke wa Ling'wenya Tukiwa kwa Mke wa Bwire

Mallya: huyo wifi yake anaitwa nani.?

Shahidi: anaitwa Athima

Jaji: nafikiri tulirudi kwenye Mstari hapo tunaanza kuzungumzia "Here say" yeye kaambiwa na Mke wa Ling'wenya na Mke wa Ling'wenya kaambiwa na Wifi nafikiri Mkiona Kuna Umuhimu mumwite Wifi yake aje kutoa Ushahidi ila Hatuwezi Kwenda hivyo.

Mallya: sawa Mheshimiwa Jaji

Mallya: Mliporudi Nyumbani ikawaje

Shahidi: tulikubaliana tupite Hospitalini

Mallya: Mlikuwa na Nyenzo gani katika Kuwatafuta

Shahidi: Tulikuwa na Picha zao

Mallya: Mlianzia Wapi

Shahidi: tulianzia Hospitali ya Muhimbili

Jaji: Kwanini Mlianza Kuwatafuta Kwenye Mahospitali

Shahidi: Ni baada ya Kuwakosa Kwenye Vituo vya Polisi

Jaji: Kwa Off Record tu, Moshi waliwambiaje

Shahidi: kwamba huku hawapo wameletwa Dar es salaam tukahisi labda wamepata Ajali

Mallya: Mlipofika Muhimbili ikawaje

Shahidi: Tukajitambulisha na Kueleza kuwa tunawatafuta Waume zetu, tulizunguka Kwenye wodi na Monchwari hatukuwaona

Mallya: nini Kikafuata

Shahidi: Tukaenda Hospitali ya Amana, Tukajitambulisha na Kuingia Kwenye Mawodi na Monchwari hatukuwaona pia

Mallya: baada ya Amana .?

Shahidi: tulienda Mwananyamala tukajitambulisha na Kuwatafuta waume zetu kwenye Mawodi na Mochwari hatukuwaona

Mallya: Siku ya tatu Sasa Mmeanda Muhimbili, Amana na Mwananyamala mkawakosa, Ulichukua hatua gani

Shahidi: ilibidi nirudi Chalinze kwa Sababu nauli ilikuwa imeshaaanza kuisha na Kwa sababu nina wawasiliano ikabidi nirudi Chalinze

Mallya: baada ya Kurudi Nyumbani, kwa Mara ya kwanza Ulipata Taarifa ya Mume wako yupo wapi

Shahidi: Ilikuwa kwenye Taarifa Ya Habari ya Jioni

Mallya: uliwaona wakiwa wapi

Shahidi: Mahakamani Kisutu Mallya Kituo gani Cha Habari

Shahidi: ITV

Mallya: Uliwaona au Ulisimuliwa

Shahidi: niliona

Mallya: wanatuhumiwa kwa Makosa gani

Shahidi: Anashitakiwa kwa Ugaidi na uhujumu Uchumi

Mallya: mara Ya Mwisho Mme wako wakati anakuaga alikwambia anaenda Moshi Kufanya nini

Shahidi: kwamba Kuna kaz Imepatikana anaenda kuifanya

Mallya: ikawaje

Shahidi: Niliwasiliana na wenzangu

Mallya: Uliona hiyo Taarifa ya Habari ITV saa ngapi

Shahidi: Ilikuwa Saa 2 za Usiku

Mallya: mkafanya Mawasiliano, Mawasiliano gani

Shahidi: tulikubaliana Twende Mahabusu kwa Sababu hatukujua wamepelekwa Mahabusu gani

Mallya: Baada ya hapo nini kilifuata

Shahidi: Mzee Ling'wenya alikuja kutoka Mtwara

Mallya: kitu gani alifanya baada ya Kutoka Mtwara Mzee Ling'wenya

Shahidi: Tulikuwa hatuelewi wapo Mahabusu gani, Tulianza kutafuta Mahabusu waliopo

Mallya: mlianza kutafuta Mahabusu gani

Shahidi: Mimi sikwepo nilikuwa Chalinze, Tulifanya Mawasiliano

Mallya: wakakwambiaje

Shahidi: Kwamba wameenda Keko wamewakosa ila Segerea Wamewakuta wapo

Jaji: ni akina nani

Shahidi: Mke wa Mohammed Abdilah Ling'wenya na Mzee Ling'wenya

Jaji: Mke wa Ling'wenya na nani..?

Shahidi: Na Baba Mkwe wake, Mzee Ling'wenya

Mallya: sasa Ushajua Mwenza wako yupo Segerea hatua gani ilifuata

Shahidi: Nilikuja Jumapili kutoka Chalinze, Jumatatu tuliamka wote Mke wa Bwire, Ling'wenya tukaenda Wote Segerea

Mallya: Mlipofika Segerea ikawaje

Shahidi: Tulipokelewa na Askari wa Jinsia ya kike akatueleza leo siyo siku ya kuwaona Mahabusu Mje Jumamosi au Junapili

Mallya: baada hapo ulifanya Hatua gani

Shahidi: Nilienda Jumamosi

shahidi: nilisikia Ma ASKARI wakisema ndiyo Yule Jamaa ambaye yupo Kabatini

Mallya: ni nani aliteyaongea hayo

Shahidi: ni Ma Askari niliowaleza Majina kuwa namtafuta Mme wangu

Mallya: hatua gani ilifuata

Shahidi: Wakachukua funguo wakasema tunaenda kumleta

Mallya: unaweza Kutuambia hapo ulipokuwepo pana taswira gani ili Mheshimiwa jaji apate Picha

Shahidi: Ukiingia Segerea maeneo ambayo kuna Meza ya Kuwekea Chakula na Kuna Chuma kama Grill lililotenganisha

Mallya: Kitu gani kilifuata

Shahidi: nilimuona Mume wangu akitembea Kwa tabu kama Vile inaonekana ameteswa

Mallya: Unaeeza Kukumbuka Mume wako alikuwa amevaaje

Shahidi: Alikuwa amevaa kama Singlendi

Mallya: hali yake ilikuwaje

Shahidi: Amedhoofika, alikuwa amekonda Sana

Mallya: Mwendo wake ulikuwaje, alivyokuwa anatembea.?

Shahidi: alikuwa anachechemea

Mallya: Ulichukua hatua gani

Shahidi: Kama Utaratibu ulivyo wa pale, Nilibeba vitu kwa ajili yake

Jaji: ukikuwa umeleta Vitu gani

Shahidi: Chakula, shuka na Sababuni

Jaji: Vitu ulimkabidhi nani.?

Shahidi: Askari akishakagua anachukua ukiwa unamuona

Mallya: ulisema ulikuwa unamuona Mume wako anaelekea sehemu, Ni sehemu gani

Shahidi: Eneo la Nyavu ambalo mnaweza Kuzungumza

Mallya: ilikuwaje Mazungumzo kati yenu

Shahidi: Nilimuuliza Hali yake na Kilichotokea

Mallya: alikujibu nini

Shahidi: HaLi yangu ni hivyo hivyo ila siyo Nzuri

Mallya: alikwambia kwanini hali yake siyo Nzuri

Shahidi: aliniambia Kuna Mateso alipitia wakati yupo Moshi, alipigwa sana Ndiyo Maana Unaniona nipo Kwenye hali hii

Mallya: Baada ya Hapo.?

Shahidi: alichukuliwa akapelekwa Mahabusu

Mallya: nitakurudisha Nyuma Kidogo, Kilichokufanya utamtafute Vituo vya Polisi na Mahospitali Mume wako ni Kitu gani

Wakili wa Serikali: OBJECTION wakili ameshauliza

Mallya: Sikuuliza, Kama aliulizwa ni Off Records nataka sasa iingie kwenye Records

Wakili wa Serikali: Ameshaliuliza hilo swali

Jaji: Sijachoka Kuandika, Muuulize tena

Mallya: nitakurudisha Nyuma Kidogo, Kilichokufanya umtafute Vituo vya Polisi na Mahospitali Mume wako ni Kitu gani.

Shahidi: Kwa sababu tuliambiwa kuwa Walitolewa Moshi Kuja Dar es salaam na tulienda Vituo Vya Polisi Kwa Sababu tuliamini Kama wangetusaidia

Mallya: Vipi Kuhusu Ushiriki wa Ndugu zake Mwanamme

Shahidi: alikuja Mama yake, tukaenda naye Moshi

Mallya: Kwanini wewe namba ya Mume wako umesema huikumbuki kwa kichwa miye ya Mke wangu naikumbuka

Shahidi: Kwa sababu alikuwa na line Mpya aliyotoka Kuisajili

Mallya: Kwanini Unasema Ulipoenda Segerea hali yake ilikuwa tofauti

Shahidi: alikuwa amekonda sana na Macho yameingia Ndani Kama Yameganda, amekonda kwa kweli na Pia Nilimuona akiwa na alama Kwenye Mkono wakati anaenda Moshi alikuwa hana

Jaji: ulisema Uliona nini Kwenye mkono

Shahidi: alama ya Kovu kwenye Mkono, Awali alikuwa hana wakati anaenda Moshi

Mallya: ya kwangu ni hayo

Jaji: Asante sana Mallya

Jaji: pamoja na Mvua kutuharibia ratiba yetu, lakini tutabreak tena kidogo tutarejea Saa 6 Kamili, Jaji ananyanyuka anatoka.
Mungu wa Mbinguni awwtie nguvu mashahidi, watuhumiwa na awawezeshe Mahakimu watende haki.

Sifa na utukufu viwe kwa Bwana.
 
aisee kumbe Majaji na Mahakimu wanakazi sana!
nauliza tu haya maneno yote wanarekodi kwa mkono au mashine?
na yanaandikwa kwa lugha ya kiswahili au kizungu?!
kama ni kwa kizungu inamaana wanatafsiri muda gani?! yaani wanatafasiri wenyewe au wanatafasiriwa?!
hii kazi yote ya nini, kwani haiwezekani kuandikwa kwa lugha ya Taifa?
Nilidhani mimi nina kazi kumbe sio. Mahakimu na majaji wanakazi kubwa sana.

hasa kesi za kutunga hizi.
 
Serikali, polisi, jeshi na nchi zima tuko uchi. Sakata hili limeonyesha ni kwa jinsi makomando wetu ni mdebwedo, ni kwa jinsi gani polisi hawaijui kazi yao na wala hawaijui miongozo yao wenyewe PGO.
Kiufupi Tanzania hatujali haki za msingi za kibinadamu. Tunaishi kama mahayawani.

Unawezaje kumtesa mtubumiwa kiasi hicho na bado watu hawajali kwa sababu tu wana Ukaribu Na Mh Mbowe??

madaraka haya ndio Maana Mungu kamnyanganya Jiwe na kumtowesha kabisa. Mbinu zote hizi zilifanyika kumdhoofisha Mbowe na Chama Chake wakati wa uchaguzi mwaka jana.
 
Shukrani kwa taarifa mkuu
 
Kingai ,Mahita ,Godluck ,jumanne na Sirro wanapaswa kushitakiwa kwa kukiuka haki za mwanadamu.

Kina Adamo walinyimwa haki zao nyingi sana.

Polisi yetu magaidi utadhani KGB au CIA
Unakosa heshima kutaja vyombo makini kama KGB na CIA.

hivi vyombo vinafanya kazi kwa weledi mkubwa mno. Ukiwa mtuhumiwa wao unaishi kama paradiso mpaka uchunguzi wa kina utakapogundua wewe u a hatia.
 
Mie nilishasema hivi niliwahi kufanyiwa uonevu flani na police miaka ya nyuma nikakubali kuwapa hela waliyoitaka ishu ikaisha kimya ila sijawahi kusahau na kwa akili niliyonayo sa hivi ikitokea police akaingia kwenye anga zangu mfano kunifanyia uonevu kama huo ntakachokifanya ni zaidi ya Hamza maana huwa nina hasira sana na hawa watu!
 
Tunafuatilia kama kawaida yetu leo tarehe 29 September 2021. Kesi ndogo ndani ya kesi kubwa .

..mke wa mtuhumiwa anadai polisi walivunja mlango wa nyumba yao.

..na anao utetezi wa madai yake kwa ushuhuda wa jirani yake.

..ushahidi huo utakwenda kuleta shida kwenye vielelezo vilivyokusanywa dhidi ya mtuhumiwa.

..upande wa utetezi unajenga picha kwamba polisi walikuwa hawafuati sheria na taratibu ktk uchunguzi na ukamataji wa watuhumiwa.
 
Jamhuri kuburuzwa katika hii kesi ni kutokana na sababu moja ndogo sana;

Awali katika awamu zote zilizopita, nchi ilikua imeshajiwekea kama ni haki ya vyombo vya serikali kufanya kazi bila kufuata misingi ya sheria na katiba (Kufanya Kazi Kwa Mazoea, Kukomoa, Kuajuana, Kuepwa Maelekezo Toka Juu, Kuonea). Vyombo vya Serikali vilikua juu ya sheria na katiba. Sasa wanaburuzwa kutokana na hayo mambo kuwekwa pembeni kwenye hii kesi ya Freeman Mbowe, na ni muda wa kudhalilika kwa serikali kwa utendaji kazi wao waliokua wakifanya na kujizoesha.

Amini maneno yangu, Kama kesi zote mahakamani zikiendeshwa kwa kufuata misingi ya sheria na katiba, bila kutolewa maelekezo tokea juu wala kujuana, "HAKUNA HATA KESI MOJA JAMHURI ITASHINDA".

NOTE THAT;

Nlianzisha uzi wa kuomba kuungwa mkono ili kesi hii irushwe LIVE COVERAGE katika television na channel maalum, kama ilivotokea Kenya na South Africa, nliomba kabla hata kesi haijaanza, kwasababu nilijua haya yote yatatokea ila watu hawakua na maono ya mbali, hawakuunga mkono kuomba hili swala. Ila kama lingerushwa LIVE COVERAGE basi dunia ingeona mengi sana (Sio kwa Kusoma Tu Threads).

Tafakari "KAMA RAIA WOTE MNGEKUA MNAANGALIA LIVE JINSI MASHAHIDI WANAVOPIGWA SPANA ZA VICHWA HUKO MAHAKAMANI, BADALA YA KUSOMA WALICHOONGEA"

Its not late, Advocate Kibatala Na Jopo Lake La Utetezi hajachelewa kufanya maombi haya mbele ya mahakama. Kwasababu kesi ina "PUBLIC INTEREST NDANI NA NJE YA NCHI" na mahakama ni ndogo haiwezi kutosheleza watu wote tanzania kuingia humo kutekeleza haki yao ya kikatiba.

Ngoja na mimi niiombe mahakama iangalie uwezekano wa kesi hii kurushwa hewani kwenye TV
 
..mke wa mtuhumiwa anadai polisi walivunja mlango wa nyumba yao.

..na anao utetezi wa madai yake kwa ushuhuda wa jirani yake.

..ushahidi huo utakwenda kuleta shida kwenye vielelezo vilivyokusanywa dhidi ya mtuhumiwa.

..upande wa utetezi unajenga picha kwamba polisi walikuwa hawafuati sheria na taratibu ktk uchunguzi na ukamataji wa watuhumiwa.
Polisi wamejisahau sana ! Wakubwa wao wanawadanganya kibwege sana kwamba wako juu ya sheria !
 
Mie nilishasema hivi niliwahi kufanyiwa uonevu flani na police miaka ya nyuma nikakubali kuwapa hela waliyoitaka ishu ikaisha kimya ila sijawahi kusahau na kwa akili niliyonayo sa hivi ikitokea police akaingia kwenye anga zangu mfano kunifanyia uonevu kama huo ntakachokifanya ni zaidi ya Hamza maana huwa nina hasira sana na hawa watu!
Ilikuwaje ebu tueleze kidogo
 
Ngoja na mimi niiombe mahakama iangalie uwezekano wa kesi hii kurushwa hewani kwenye TV
Hilo swala ndugu sio la uwezekano, ni haki kufanywa vile na mahakama itaridhia tu;

1) Ni haki ya kikatiba kwa kila raia kufuatilia kesi yoyote mahakamani inayomhusu yeye au maslahi yake au mtu anaemfahamu kama raia. Kesi hio ina Public Interest.

2) Mahakama ni ndogo haina uwezo wa kumudu watu zaidi ya millioni 60 kwenda kufuatilia hio kesi mahakamani. Hivo live coverage inapunguza msongamano na hatari ya raia au watu kufanya fujo.

3) Kupunguza msongamano kwaajili ya afya (Covid 19), live coverage itafanya watu watulie majumbani mwao huku wakifatilia kesi bila kujazana kwenye daladala wala mahakamani.

4) Usalama kwa washtakiwa. Live coverage itapunguza msongamano wa watu nje ya mahakama kwaajili ya usalama wa washtakiwa. Sio kesho tusikie watu wasiojulikana wamemimina risasi kwenye gari ya washtakiwa na kuwaua au kuwajeruhi. Week hii gari ya kina Freeman Mbowe iliharibika mahakamani, hivi kweli unasafirisha makomandoo na mwenyekiti wa upinzani ambao wana kesi kubwa na yenye public interest kidunia kwenye gari bovu??? Usalama wao huoni unakua mashakani??? Watu wasiojulikana (Kama Serikali inavo waita) wakivamia na silaha za moto na kuwamiminia risasi???

Nikiendelea kukuandikia points ntaishia kujaza server za JF. . . . Hizo ni baadhi tu. . . .
 
Back
Top Bottom