Daniel Anderson
JF-Expert Member
- Aug 7, 2011
- 872
- 141
Ndugu zangu, watanzania wenzangu,
Kwa takriban mwezi sasa unapita huku wingu la kisiasa hapa nchini likiwa limegubikwa na mijadala kuhusu siasa za chama kikuu cha upinzani (CHADEMA). Ilianza mivutano kuhusu maamuzi ya mwenyekiti wa PAC ndugu Zitto kuwataka makatibu wakuu wa vyama kujieleza ni kwa nini hawajawasilisha ukaguzi wa vyama vyao kwa mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali kwa ukaguzi kama sheria yetu inavyotaka.
Miongoni mwa waathirika wa maamuzi haya kilikuwa ni chama chake mwenyewe cha CHADEMA na hivyo kufanya matamko mengi juu ya uamuzi huu, tena chama chake kikitoa matamko karibu kila siku kumpinga mwanachama wao huyu.
Zikaanza kuibuka shutuma na vioja vingi vya ajabu kabisa katika historia ya siasa zetu hapa nchini, ambapo hadharani kabisa, Mbunge Godbless Lema alijitokeza kuwasha moto wa migogoro kwa kuupinga msimamo wa chama kuhusu posho. Akahalalisha kile wanachadema tulichokiona ni haramu tangu baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 (posho za kukaa kwa wabunge) kwa kumwita Zitto ni mnafiki na anayeudanganya umma wa watanzania. Hapa hatukujiuliza ni nani mnafiki kati ya Zito aliye walk the talk au aliyegoma na kupokea kimyakimya?
Kwa nini Lema ametumia nguvu kubwa kwa Zitto badala ya kuhoji maamuzi ya KUB kurejesha gari alilikataa mwanzo, tena kimya kimya bila kutoa sababu zenye mashiko za kumfanya afanye hivyo? Kwani kwa kufanya vile KUB alijitofautisha vipi na hawa CCM tunao waparua kila siku kuwa ni wanafiki? Anyway, sijadili suala la KUB, ila mazingira na maamuzi ya CC juu ya Zitto & Co.
Ni kweli Zitto ni msaliti? Mbona kwenye kamati kuu alijibu hoja zote mlizozitoa juu yake na hakuna kosa lililoonekana juu yake? Kama ni walaka ambao amekiri haujui kabisa, ambao ni kweli unamtaja kwamba atahusishwa (bt hakuhusishwa up to the point) kwa nini ahukumiwe kwa kuonekana tu kuwa unamlenga japo hajashiriki? Hebu tuambieni tena na tena ili tuwaelewe lakini vinginevyo, tunavunjika sana moyo sisi wanachama.
Elezeni Zitto has amefanya nini. Ile ripoti ya siri si mliikataa wenyewe? Si mlisema hamuhusiani nayo? Kwa kweli ingekuwa ni ile ripoti basi hata mimi ningeunga mkono na wala si hii ya pili ambayo haina uhalisia hata kidogo.
Kamati kuu hebu tuambieni, mbona mnajichanganya kuhusu hata huu waraka wenyewe? Si mlisema ndo huu mliouweka mtandaoni? Mbona bada ya mijadala na kuonekana hauna tatizo mgkageuka na kusema upo mwingine? Mbona hata Mwigamba kakiri kuwa huu ndio wenyewe? Au mnafikiri hatuwezi kuhoji maamuzi ya kamati kuu?
Kwa nini mgogoro na Zitto uwe sasa na si wakati mwingine? Kwa nini tunapoelekea uchaguzi na si kabla? Kwa nini ripoti ya siri ambayo, kwangu ningeipa nafasi zaidi katika maamuzi, iwe leo tunapoelekea uchaguzi? Kwa nini tunaweka mazingira ya Mbowe kutawala daima? Mbona hata shutuma dhidi yake tunazipuuza? Kwa nini hatukuamua vinginevyo dhidi yake kwa kashfa ya kukiuzia chama magari mabovu? Kwa nini tuli'mute' alipobainika kuwa na jumba la kifahari Dubai?
Mbona hatujahoji iweje naye kwake jimboni upinzani hauna nguvu hata ukilinganisha na iringa mjini? Kwa nini chama kinaenda kwa matukio na si agenda ya chama? Kwa nini amekuwa akiongoza chama kwa mfumo wa matamko na kulaani?
Ukweli ni kuwa tunahitaji mabadiliko ndani ya chama tena mapema iwezekanavyo. Umepita ule wakati wa kwenda na fikra na matamaanio ya mwenyekiti badala ya mahitaji ya chama. Chama ni cha watanzania wote si Mbowe pekee ndiye mwenye hati miliki ya kuwa mwenyekiti daima.
Tunahitaji msukumo mpya wa kutuwezesha kujiimarisha vijijini zaidi. Hizi porojo tulizonazo za nyuma ya keyboard zinatudanganya. Tembelea Matombo hadi Kisaki uone kazi ilivyo kubwa. Nenda Engusero hadi Pori kwa pori uone watu walivyo na kiu ya mabadiliko. Nenda Matwiga, Mafyeko, Lupa, Makongorosi na Chunya kwa ujumla uone haja kubwa ya mabadiliko ilivyokubwa miongoni mwa watanzania wa kule.
Siyo sifa kufukuzana kila kukicha tena kwa apparent reasons kama zinazotolewa na uongozo sasa. Nasema hivi, hata kama mkiamua kumfukuza Zitto, mjue wapo wengine watakaokuja kuwa na misimamo thabiti ya kuenenda kwa kadiri ya maneno yao kama Zitto alivyo. Mtawaita wasaliti kwa kuwa na msimamo sahihi wa kuyapeleka mambo ndani ya chama, lakini chama ni cha wanachama wote.
Nawapa challenge tu, itisheni leo baraza kuu muone kama hakutakuwa na ngumi kwa sababu ya maamuzi yenu haya.