Maamuzi ni juu ya mtu mwenyewe na nature

laii

JF-Expert Member
Oct 10, 2016
834
1,060
Kwanza nianze kuwapa hongera kwa sikukuu ya Uhuru,na imani Hasubuhi ya leo kila mtu anaamkia kwenye mihangaiko yake iwe umeajiriwa au umejiajiri.

Kwa kawaida binadamu wote tulizaliwa na mama zetu hapa duniani,wakati wa kuzaliwa kiuhalisia watoto wote wanategemea kulishwa na wazazi au walezi,hapa hata uwe umezaliwa katika familia ya mfalme huwezi kua na maamuzi,mambo yote unaamuliwa,tunakua tunaenda chekechea,hapa inategemea vitu viwili ili uweze kutoboa kwenye masomo uwezo wa mzazi kumpeleka mtoto shule nzuri au akili ya mtoto bila kujali mazingira aliopo,hapa akili ni muhimu zaidi

Tunaenda la kwanza mpaka tunamaliza la 7 na hapa ndo msingi wa elimu unapojengwa,-hapa pia hatuwezi kujipima au kupima uwezo wa mtoto maana kuna factor nyingi,kuna mwanafunzi hamuelewi mwalimu,kuna ambae michezo inakua mingi kiujumla akili inakua haijakomaa

Baada ya hapa kuna wanaofaulu kwenda shule za serekali na kuna wanofeli wanaenda private school,sasa hapa ndo uwezo wa mtu unaanza kuonekana,unakuta aliefaulu anafel na alie fel la saba anafaulu form4,hivyohivyo kwa form six,baada ya hapa kuna wanaoenda chuo na wanakuja mtaani

Kwenye issue ya mafanikio kwenye level hii inakua ni personal matter asilimia 95%,ni mtu mwenyewe kuchagua aina ya maisha anayotaka kuishi,haijalishi background uwe umetoka kwenye familia masikini au familia tajiri kama huna malengo hapa hutoboi ndugu na maanisha katu hutoboi,hichi ni kipindi cha kuamua unataka kufanya nini kwenye hii Dunia,ni wakati wa kuchagua marafiki kwa makini sana ni wakati wa kuchuja marafiki,kuacha tabia za ajabuajabu ulizokua ukizifanya huko,kama ulikuwa mlevi punguza au acha kabisa,na kama hujawahi kunywa au kuvuta si kipindi cha kujifunza kabisa,ni wakati wa Kumtumikia Mungu na kuuheshimu mwili wako,si leo uko na mpenzi huyu kesho yule,namaanisha kama ulifanikiwa kwenda chuo shikilia sana elimu,kama ukibaki mtaani pambana na chochote halali utafanikiwa.

Hii level ni ya juhudi binafsi hahiitaji tuition ni wewe kuamua na kupanga na kuheshimu kila mtu na kila kitu ambacho unafanya hakika nature itakubeba,ni kipindi cha kupambana haswa ni kipindi mchumba anaandaliwa,ni kipindi unaanda maisha yako ya baadae ni kipindi unaandalia familia yako maisha yao ya baadae,ukimbwela hapa ukasema life begin at 40,utapata tabu.

Mara nyingi wanasema @ 40 uwe angalau una kwako si kupanga kama ni kupanga ni kwa ajili ya biashara,uwe angalau umeshamalizana na shule,uwe na familia.

Ila yote haya hakika peke yetu hatuwezi ni Kumwomba Mungu kwa juhudi zetu zote na hakika Mungu hamtupi mja wake.
Karibuni kwa kuchangia.

Wasalaam
Laii
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom