Maamuzi na vigezo vilivyotumika kuwabadilisha/kuwafuta kazi trafiki si sahihi

Mbugi

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,488
257
Hivi karibuni trafiki kadhaa wamebadilishiwa vitengo ama kufutwa kazi ya utrafiki kwa vigezo visivyo sahihi kwani vilizingatia zaidi kushuka kwa mapato yanayotokana na faini za barabarani.

Ki msingi kigezo cha kushuka kwa mapato hayo ni matokeo mazuri ya juhudi iliyofanywa kwa makusudi na jeshi letu kupeleka elimu ya kutosha kwa wananchi na jamii kwa ujumla ktk kupunguza ajali na kuhakikisha vyombo hivi vya usafiri vinakuwa ktk hali ya ubora unaostahili hivyo tusingetemea tena makosa hayo kuongezeka badala ya kupungua.

Mfano mkoa wa Mbeya peke yake zaidi askari 54 wamebadilishiwa vitengo vyao kwa kushindwa kufikia malengo ya ukusanyaji wa faini hizo wangali wakijua watanzania wengi elimu ktk matumizi ya vyombo hivi imekuwa na wameelewa.

Huu si utaratibu mzuri na jeshi likae likijua faini hizi zitaendelea kupungua siku hadi siku sasa hatujui kama budget yetu inategemea mapato kama haya na wakusanya masurufu haya wakaendelea kubanwa kwa ku-underpeform sizani kama tutafika salama.
 
Hujajiuliza pengine hayo mapato walikuwa wakiyaelekeza kwenye mifuko yao badala ya mfuko wa umma? By the way, traffick police ni police tu kama wengine hivyo ni hiyari ya rpc kuamua kazi ya kumpangia, anaweza akamuweka cid, ffu, kikosi cha mbwa au police wa kazi za kawaida, so binafsi sijaona tatizo hapo. Anyway, pole kwa yaliyo kusibu.
 
Hicho kitengo kingefutwa kabisa, hakuna askari kuvaa nguo za trifiki sijui nini. Then wa barabarani wawe wanapangwa kwa zamu tu kama wanavyopanga kwenye mabenki na sehemu zingine. Hii ingeongeza ufanisi na kupunguza malalamiko kwa wananchi
 
Mbona bado Traffic Wengi mmezidi Kuendekeza Rushwa bila Aibu... Rais Magufuli toa Maelekezo Kikosi cha Usalama barabarani kisiwe na Askari wakudumu Ili kiendane na speed yako... lkn pia Kuepusha Matabaka ndani ya Jeshi la polisi nakuleta dhana ya Usawa... Ifike wakati tuwaone watoto Wa vigogo Wakilinda Mabenki na Kuopareti Magari ya Maji washa washa na Watoto wasio Wavigogo kwenye post nzuri Kama Mipakani, Traffic na Upepelezi.

Rais Magufuli Muundo Wa Idara za Jeshi la Polisi Unapaswa Kumulikwa Upya Kwa Ujenzi Wa Tanzania Mpya.
 
Rushwa barabarani imenifanya nisibadili PROFILE PICTURE yangu kwa zaidi ya miaka miwili

Barabarani pamekuwa ni sehemu hovyo ya kutufanya tuichukie nchi yetu.....

kumbe "huenda" wanaagizwa ma mabosi wao kiwango cha kupeleka kwa siku.... usipopeleka pesa hiyo ya mboga kwa mabosi zako unatolewa kitengo
 
Hicho kitengo kingefutwa kabisa, hakuna askari kuvaa nguo za trifiki sijui nini. Then wa barabarani wawe wanapangwa kwa zamu tu kama wanavyopanga kwenye mabenki na sehemu zingine. Hii ingeongeza ufanisi na kupunguza malalamiko kwa wananchi
umenenea haswaaaa hawa wapangwe kama wa benk tu.
 
Back
Top Bottom