Maamuzi matatu ya Serikali ya awamu ya sita yanayolalamikiwa yote yapo sahihi Na Sababu zangu ni kama ifuatavyo

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,099
27,067
Kwanza unatakiwa kujua kwamba Serikali inapokuwa inafanya maamuzi yake Inaweza isiwe sahihi Kwa mujibu WA katiba lakini ikawa sahihi kisiasa, kiuchumi, kiusalama wa nchi au kiutawala.( Constitutionally wrong but politically right etc and vice versa).

Utaratibu Huu upo katika Serikali zote duniani toka Enzi za Pontyo wa Pilato.

Maamuzi matatu yanayo lalamikiwa dhidi ya Serikali ya awamu ya sita yote yapo sahihi ama kisiasa,kiuchumi, kiusalama wa nchi na kiutawala.

1. Kuwaondoa Wamachinga : Maamuzi sahihi Kwa uchumi wa nchi.

2. Suala la Mbowe: Maamuzi sahihi Kwa usalama wa nchi/Maamuzi sahihi kisiasa

3. Suala la kukazia hukumu ya tamko la Serikali ya awamu ya Tano kuhusu kupiga marufuku Kazi za kisiasa: Maamuzi sahihi kisiasa(politically right). CCM Na Chadema Ni vyama shindani . CCM inataka kubaki kwenye Dola Na Chadema inataka kushika Dola. Ni sahihi kabisa kisiasa Na Ni wajibu WA Kila Chama kuwa Na mikakati ya kukidhoofisha Chama kinacho shindana nacho ili kusudi chenyewe Kibaki kuwa Na nguvu ili ima kiendelee kushikilia Dola ama kiweze kushika Dola.

NB: Washindani WA CCM wanasema wanataka katiba mpya Kwa Sababu HII iliyopo Sasa haifai kabisa .

Serikali wanazuia mikutano ya vyama vya siasa ambayo IPO Kwa mujibu WA katiba Ile Ile wanayo SEMA haifai.

Wapinzani wanasema katiba imevunjwa Na kutaka katiba ifuatwe. What's up katiba hamuitaki kwa sababu mnasema haifai halafu at the same time mnasema katiba hiyo hiyo msioitaka ifuatwe,which is which and which is not which?How can you contradict urself in less than five minutes?

Inawezekana wameivunja katiba msioitaka kwa sababu wanajua hata nyie hamuitaki..

In Samia we Trust. Kazi iendelee
 
UkiZoom Kilichoandikwa Kwa Mbaaali Utaona kuna 'Massage' , Lakini Inahitajika Utulivu Kuiona Sense Kwenye Nonsense
 
Hii nchi ya kijinga sana na watu wake kama nyie!!

Nchi inabid iendeshwe kwa katiba, hakuna kuvunja katiba afu unasema upo sahii kiuchumi sijui...
 
hii nchi ya kijinga sana na watu wake kama nyie!!
nchi inabid iendeshwe kwa katiba, hakuna kuvunja katiba afu unasema upo sahii kiuchumi sijui...
Usikariri
 
Hii nchi ina changamoto nyingi. Utashangaa mtoa mada ni mama wa watoto ambao wanategemea wajifunze kutoka kwake. Matokeo yake ni kuzalisha na kukuza kizazi cha mataahira kama mtoa mada.
 
Hii nchi ina changamoto nyingi. Utashangaa mtoa mada ni mama wa watoto ambao wanategemea wajifunze kutoka kwake. Matokeo yake ni kuzalisha na kukuza kizazi cha mataahira kama mtoa mada.
Hoja hupingwa Kwa hoja . Matusi Ni dalili za kutokuwa Na hoja .
 
Hata Sabaya maamuzi yake yalikuwa sahihi ila sasa hivi anaozea jela. Usahihi ni kwa sababu una nguvu tu, bila mamlaka unakuwa jinga flani. Ukisoma dhana ta "rationality" maamuzi yanatakiwa mchakato wa kipimwa hasa mpaka yatekelezwe.
 
Back
Top Bottom