Maamuzi magumu: The biggest joke of the century | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maamuzi magumu: The biggest joke of the century

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by W. J. Malecela, Jul 6, 2011.

 1. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #1
  Jul 6, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  FACEBOOK: by William Malecela on Tuesday, July 5, 2011 at 8:40pm[/h]

  @ NEW YORK CITY-US: The biggest political joke this week, ilikuwa ni ushauri wa maamuzi magumu kwa Serikali kwa Kiongozi aliyetuingiza taifa hasara ya USD $ 170 Million kwa ajili ya umeme wa dharura wa Megawati 100 ambao haupo. Sasa cha ajabu sana ni wananchi na baadhi ya Wabunge wa CCM waliosimama na kumshangilia sana, ninasema hawa wote tunahitaji kuwakamata na kuwachapa bakora sana, kama Mwalimu alivyokuwa akiwafanyia maviongozi magoi goi kule Ikulu zamani. I mean what happened to this Nation? Tumelogwa na nani hasa? Hili taifa kama ni maamuzi magumu tunatakiwa kuyafanya kwa kusimamia Sheria kwanza, ambako ndiko hasa kwenye ubovu na huyu Kiongozi akiwa ni mfano hai wa hilo la kutoheshimu sheria!

  - Kutoheshimu sheria sasa kumetufikisha mahali ripoti ya W/B inasema 20% ya bajeti yetu kila mwaka inaishia kwenye Rushwa, mfano mwingine kati ya kesi 10,000 zilizofikishwa Takukuru toka ianzishwe ni 5% tu zilizofikishwa kwenye Sheria, zingine zimeishia hewani kwa sababu ya Rushwa, Wakulima wetu wa Mbao hishia kupata only 5% ya kilimo chao huku 95% zikienda kwa Viongozi wa juu na makampuni husika kupitia Rushwa. Mh. Lowassa anasema maamuzi magumu ni pamoja na kutafuta madeni zaidi, huku akijua wazi kwamba toka ashike madaraka ya juu mpaka leo, deni la taifa limeongezeka kwa kasi kubwa sana kutoka USD $ 6.1 Billion mpaka sasa USD $ 10.2 Billion, huku Serikali ikiwa haina cha maana cha kuonyesha na hasa umeme ambao aliufanyia maamuzi magumu. Huko kwenye ukusanyaji kodi ndio kabisaa kumeoza, kila mwaka TRA wanashindwa kukusanya Shillingi Billion 100 kwa sababu ya Rushwa, matokeo ni kuongezeka kwa inflation 8%!

  - Cha kusikitisha zaidi ni jinsi Serikali ilivyomjibu, ikjikanyaga kanyaga na maneno ya Bara bara ya Mkapa na Chuo Cha Dodoma, badala ya kufanya maamuzi ya magumu ya haraka sana kwa kumkamata haraka sana yeye mwenyewe kwanza na genge lake, ili wakajibu zile USD $ 170 Million za gademu umeme wa dharura ambao haupo ziko wapi? I mean my people, unajua Mungu anahitaji kwenda kuwaomba Radhi watu wa Sodoma na Ghomorah kwa sababu sio siri we are more than them this Nation, look here kati ya wananchi Millioni moja wa Tanzania walioulizwa kama wanaamini tuna Sheria, ni 19% tu waliokubali kwamba zipo, now what about the rest 81% ambao wanaamini kwamba hakuna Sheria? Masikini ya Mungu hili taifa nani atatuokoa? maana hakuna wa kumsaidia mwingine I mean haiwezekani binadam akashindwa kuona na kufikiri pia, kwamba what Mh. Lowassa said is the biggest political joke of all our times na the saddest thing kuna waliomshangilia, dawa ni kukamata wote na kuchapa viboko mbele ya gademu public!

  - Tanzania; maamuzi magumu yaanzie kwenye utawala unaoheshimu sheria kwanza!

  Mungu Aibariki Tanzania!


  William Malecela @ NYC, USA.
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Jul 6, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mzee wamekukorofisha kweli!!!
   
 3. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #3
  Jul 6, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Mkuu wangu sometimes ninashindwa kuelewa hili taifa, the symbol ya maamuzi magumu ya wizi anaposimama na kutukejeli kwamba hatuwezi kutoa maamuzi magumu, I mean inasikitisha sana!

  Willie @ NYC, USA.
   
 4. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  The biggest joke ni namna watanzania tunavyokubali kutumia billions kuhudumia wabunge wa viti maalum ambao hawana manufaa (si kutoka chama tawala si kutoka upinzani)

  It's a joke kukubali kukatwa kodi kwenye mshahara mdogo uliopo akalipwa mwanamke mara 17 ya mshahara huo bila ya kukatwa kodi kwa sababu tu amezaliwa mwanamke

  It's a joke kukubali mfumo huo ambao majimbo mengine yanakuwa na wabunge hadi wanne na mengine kuwa na mbunge mmoja.
   
 5. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #5
  Jul 6, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Sisi ni taifa la wasioona mbali, na Lowassa anasema ukweli. Kama kweli tunaweza kuchukua maamuzi magumu, kwa nini hatujawachukulia hatua za kisheria yeye pamoja na Chenge? Tunaogopa kuiacha sheria ichkue mkondo wake, jambo linaloweza kuonekana kuwa uamuzi mgumu kwa walioko madarakani.
   
 6. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #6
  Jul 6, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Serikali haichukui uamuzi mgumu kwa sababu wananchi hatujaitaka ifanye hivyo. Wananchi tukitaka serikali haitakuwa na budi ila kutekeleza matakwa hayo
   
 7. Sn2139

  Sn2139 JF-Expert Member

  #7
  Jul 6, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 827
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  William, hongera kwa maoni yako mazito na ya kweli. Leo umenileta karibu zaidi na wewe kuliko jana na juzi!

  Opinion yangu ni kwamba, una uwezo mkubwa wa akili, lakini umepungukiwa na jambo moja, nenda kauze mali zako zote uwape maskini. Hilo ndio tatizo la watu wengi, wenye akili na wajinga, hawawezi kukana nafsi zao na kuwaona watu wengine kuwa ni watu kama wao. Juzi ulipotukana nikawa nakushangaa sana, hadi nikadhani kumbe aliyeshiba hakosi kiburi, majivuno na dharau hata akipewa ushauri mzuri. Nilitamani kulia niliposoma jibu lako dhidi ya ushauri wa Ally (?). Ushauri ule ulikuwa mzuri mno kwako na kwa wengine. Kitu cha kushangaza si kwamba uliukataa peke yake, bali ulimtukana!!! Je ulikuwa umepata moja baridi moja moto?

  Hata hivyo, tukirudi kwenye mada iliyopo mezani, nakubaliana kabisa na kilio chako uliposema
  . Mimi pia ninalia hivyo. Mimi ni mwana CCM tangu wakati wa TANU, lakini ninakosa mtu makini ndani ya CCM anayeweza kujibu kilio chako hicho, na kwa dhati ya moyo wangu, niaona kuna mwana CCM mmoja tu ambaye alihamia CDM, Dr W. Slaa. Huyu mtu ana sifa zinazoelekea kwa Mwl. Nyerere. Tunaweza tuache kujadili kuhusu uzuri na ubaya wa CDM, lakini tumwangalie Dr W. Slaa kama yeye, kama jinsi Dr JK Nyerere alivyo yeye tofauti na CCM.

  Hilo ndio pendekezo langu kwako ndugu yangu. Aksante
  Sungura
   
 8. P

  PresidentSalum Senior Member

  #8
  Jul 6, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 184
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Dogo, tatizo lako unachanganya chuki zako pamoja na hisia zako za ovyo, na hapo ndipo unaposhindwa hata kabla ya kuanza.
  umeonyesha kiwango kikubwa cha kutokuwa na akili, huu ni grade A upupu.
  Babako Malecela hakuwa na akili, na wewe umeamua kumuunga mkono kwa kutokuwa na akili. Hiki ni kilio tosha ndani ya familia yenu
   
 9. P

  PresidentSalum Senior Member

  #9
  Jul 6, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 184
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Utaelewaje matatizo ya mtanzania halisi wakati wewe upo NYC kwa pesa za wizi uliofanywa na JSM?
   
 10. T

  Technology JF-Expert Member

  #10
  Jul 6, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 733
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  wewe predident salum: nahisi ulikua jela.
  Join Date : 3rd December 2006
  Posts : 12

  Rep Power : 0
   
 11. Facts1

  Facts1 JF-Expert Member

  #11
  Jul 6, 2011
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 308
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwanza naungana na mjumbe aliyetangulia hapo juu Sn2139 kuwa kwa siku mbili tatu zilizopita umejishushia heshima mbele ya members wengi waliokuwa wanakuheshimu nikinukuu swali lako moja ulilomuuliza Slaa 'Kabla ya wewe kukuita fisadi tuambie huo mshahara wako kweli unatoa kodi kama si fisadi ni nani' tuachane na hayo.

  Nampongeza sana Mh.Lowassa kwa kuwaonyesha wabunge wenzake na watanzania kuwa si lazima kila siku kuipongeza serikali kuna wakati inatakiwa kukosolewa inapokwenda kinyume na kikosoa si kuwa umekuwa mpinzani. Kwenye maelezo yako umesema Lowassa alisema maamuzi magumu ni pamoja na kutafuta madeni zaidi nafikiri hiyo sentensi si ya Lowassa ni yako mzee sijawahi kuisikia kutoka kinywani mwa Lowassa.

  Ukisoma vizuri ujumbe wako sehemu nyingi unailaumu serikali kwa kutotekeleza wajibu wake umesema haina cha kuonyesha, umeme hakuna ukusanyaji kodi umeoza lakini cha ajabu unaishia kumlaumu Lowassa kana kwamba yeye bado yuko madarakani unashindwa sijui kama ni technical kuwa pin point wahusika wakuu wanaosababisha hayo yote.

  Lengo lako lilikuwa kuonyesha Lowassa amekosea aliposema serikali inashindwa kufanya maamuzi magumu lakini umeshindwa kujenga hoja na matokeo yake umeanza kumvika Lowassa matatizo ya serikali kana kwamba yeye ndiye ameyasababisha ili kufikia malengo yako yaliyoshindwa ya kumlaumu Lowassa. Binafsi nilipoona heading 'Maamuzi magumu the biggest joke' nikadhani unaongelea ugumu wa CCM kujivua gamba kuwa ni joke of the Century.
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Jul 6, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,780
  Likes Received: 83,136
  Trophy Points: 280
  Bora useme na wewe maana wakisema wengine wataambiwa wanamchukia kwa sababu ni chaguo la Mungu, kafanya mengi sana, kaleta uhuru wa kuzungumza, wanamchukia kwa sababu ni Muislamu wanataka kumweka Mkristo mwenzao huku Taifa likiendelea kuangamia kwa kasi ya kutisha. Wengine tulianza kuishtukia hii Serikali dhalimu siku nyingi sana na hata zile zilizopita bora na wewe taratibu unaanza kuona hivyo kama inavyoonyesha hapo kwenye rangi nyekundu.
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Jul 6, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Alichofanya Lowassa ni kuwathubutisha serikali kuwa kama kweli "mnaweza kufanya maamuzi magumu tukatamateni, tufukuzeni"..
   
 14. N

  Navoyne JF-Expert Member

  #14
  Jul 6, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 871
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  I have to give applause to Lowassa is not only too big for CCM but also our current government .............sasa kama mnaweza kufanya maamuzi fanyeni sio kila siku mnakuja na strategies tu.
   
 15. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #15
  Jul 6, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  kwa kweli hii ishu ya viti maalum na tule tujimbo twa zanzibar twenye wapiga kura 2000, ndiyo hunimaliza kabiza mimi. bunge limejaa watu wanaolipwa kodi zinazokatwa kwenye mishahara yetu ya "saidia Mungu" ili wajivike dhahabu na kupuliziwa upepo wa viyoyozi vya mashangingi huku mamilioni ya wanawake wenzao wengine wakinunuliwa bajaji ziwapeleke labor kujifungua!!

  kwa kweli nchi hii tuna majokes makubwa zaidi ya hayo aliyoona malecela!!
   
 16. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #16
  Jul 6, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,973
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mkuu, matusi ya kifamilia ya nini? Haingii akilini unapomkosoa Willy kwa kutumia tabia hiyo hiyo ya matusi. Tena cha kishangaza hata hoja yake hukuijadili umeishia kumtukana tu yeye na familia yake!Jamani tuweni wastaarabu hata tunapokuwa tumetofautiana kihoja na kimtizamo.Back to topic: Willy, maamuzi magumu hayawezekani serikalini kwa sababu chama chenu kimeoza. Mwalimu aliwahi kusema "chama legelege huzaa serikali legelege." Ndo hayo tunayashuhudia; serikali legelege inatupeleka shimoni. Solution ni kukiondoa hichi chama ouzo na kuweka serikali ya nyingine ambayo haitokani na hicho chama.
   
 17. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #17
  Jul 6, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Unaposema taifa hili ni lipi hilo la Marekani au maana neno hili ni sehemu ulipo,
  kama ulimaanisha taifa la tanzania naungana na wewe kuwa huwezi kulielewa, usumbufu wa foleni Ubungo mataa Dar ni tofauti na foleni ya NYC na mgawo wa umeme hadi bungeni nafikiri haukuhusu kwa hiyo huwezi kujua machungu yake.

  Halafu huyo symbol wa maamuzi magumu anayewakejeli yaelekea ni Lowassa, anawakejeli kuwa hamuwezi kutoa maamuzi magumu including YOU give me a break.
   
 18. U

  Unstoppable JF-Expert Member

  #18
  Jul 6, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,049
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kwangu mimi CCM chairman and MPS ndio the biggest joke of the century; First: pale Lowassa anapomkebehi yeye na serikali yake na bado hana chakumfanya. 2.Pale MPS wanapomsafisha Chenge mchana kweupe ili hali kesi ya Rada iko wazi. 3. Wanapopoteza resources and energy kwenye propaganda ya kujivua gamba wakati wanajua haiwezekani and the list goes on
   
 19. a

  arigold JF-Expert Member

  #19
  Jul 6, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 594
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 60

  [​IMG]  na mmoja kati ya hao waliotuingiza kwenye MKENGE huo wa umeme ni huyu Mama.....

  je tuanze kumpiga yeye viboko au?
   
 20. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #20
  Jul 6, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kaka Malecela angalau umesema kweli. tuseme sasa unaungana/kukubaliana na wanaosema CCM imeshindwa? maana madhila yote haya yanasababishwa na serkali ya ccm. watu wanapohamaisha umma uiondoe ccm madarakani (kwa kura) si kwa sababu nyingine bali ni kushindwa kwake kama ambavyo umeanza kuainisha hata wewe.
   
Loading...