Nataka nifanye maamuzi magumu ya kutengana na mke wangu

Duuh tungemsikiliza na bidada ingekuwa vyema, tunaweza kuona mke mbaya kumbe na wew una mapicha picha hayavumiliki. Ila una force mke ayavumilie matokeo yake ndio hayo mtu anaamua kumbwaga manyanga
 
Mie simshangai huyu kaka kusita kufanya maamuzi lakini,,,,familia ni kama investment,kupoteza na kuanza upya ni swala linaloogofya kidogo ,wengi wanakufa na tai zao shingoni
 
hata vitabu vya dini vinasema mwanamke atavunja ndoa yake kwa mikono yake! huwa sio rahisi kwa mwanaume kumuacha mwanamke.emu nimbie ni kosa gani kubwa ambalo mwanaume anaweza kufanya mpaka mwanamke akaamua kumuacha mwanaume? ukiacha la kuhudumia familia

Mwanaume hamuachi mkewe?
Kuna case kama za mume kupata mchepuko Akasukwa akasukika

Kuna mambo ya mume kupata ghafla na kuamua kutafuta wa fasheni

Kuna mume kukimbia majukumu maisha yakimlemea!
 
Mkuu, kwanza pole sana kwa haya uyapitiayo kwa sasa......
Maisha ya kuishi wawili ni maisha yanayoitaji busara na maelewano..
Hadi sasa kutokana na maelezo yako, inathibitisha wazi hakuna muelekeo mzuri kati yako na mkeo...
Ninawasiwasi hata mimba aliyoitoa yawezekana haikuwa yako Mkuu.
Pili maamuzi ya kukopa Bank pasipo kukushirikisha ni kosa kubwa ambalo linaonyesha dharau aliyonayo kwako.. Mkeo ameshindwa kuwa mwaminifu kwako hadi kuomba pesa kwa kidume mwingine, hii inathibitisha ANA KUSALITI waziwazi...🔥🔥🔥

Achana kabisa na huyo mwanamke kabla hujapata jeraha kubwa litakalo kuchoma sana....

MUACHEEE AENDE ZAKEEE✔✔✔
 
Mbaya zaidi nyumbani kwangu amegoma kusaidia chochote anasema si kazi yake!

Nilisafiri nikarudi ghafla bila taarifa nakuta anaongea na mwanaume kwa simu SAA saba usiku tena anamwomba amsaidie pesa alipe ada!

Amesafir kikazi wiki ya tatu sasa simu hapokei, SMS, hajibu akipokea haongei....Namsubir arudi niite ndugu pande zote mbili niwambie nimeshindwa.!!


HUNA MKE braza. Tengua teuzi, na anza mchakato wa kuoa kwingine. Kila la kheri.
 
NI Mwaliimu?

Members naomba tu niandike kwa ufupi naamini mtanielewa na kama kuna ushauri nakaribisha.

Tumebahatika kupata mtoto mmoja 5yrs now, wote ni watumishi.

2013 akaomba nimsaidie kumtafutia shule mdogo wake wa kiume arudie kidato cha pili baada ya kufeli form four na kukaa nyumbani miaka karibu mitatu nikafanya hivyo, baada ya muda shemeji akaanza dharau na kiburi kwangu tena mbele ya Dada yake, nikilalamika Dada mtu anachukulia poa, nikavumilia baada ya muda mfupi kapigwa suspension akapiga magoti nimsaidie asifukuzwe shule, nilipoona habadiliki nikajitoa kumsaidia but ilikuwa ni baada ya Dada yake kusema kama naona taabu ye atalipa ninamsema sana mdogo wake.

Dogo kamaliza na division 3 point 26, wakaomba chuo cha afya government wakakosa, huruma ikanijia nikamwambia Dada mtu aende private kidato cha tano akakataa akakomalia kuwa anampeleka chuo cha afya private kama 4 million ada na mahitaji mengine nikamwambia haitawezekana hali ni ngumu kiuchumi aende advance.... nikaambulia matusi kuwa nina "gubu" na maendeleo ya mdogo wake na nisijali yeye na ndugu zake watalipa ( by this time tulikuwa tupo mbali sababu za uhamisho), mi nikaona nisiingilie ndugu.

Kumbe hakuna lolote yeye ndo mlipaji wa kila kitu, nikaja jua baadaye kuwa amekopa bank bila kunijulisha na pesa sijajua kafanyia nini kumuuliza anasema anasomesha......sijakaa sawa kumbe alikokuwa mwanzo kakopa pesa za watu million mbili kwa ajili ya jambo hilo na hajarejesha hadi sasa pamoja na riba inafika nearly 4 million.

Ametoa mimba ili aweze kujikeep busy na biashara nje ya kazi ili kuweza kugharamia masomo ya mdogo wake nilipobaini anasema maisha magumu tusubiri kwanza nilipombana anasema bahati mbaya....uwongo...

Nilisafiri nikarudi ghafla bila taarifa nakuta anaongea na mwanaume kwa simu SAA saba usiku tena anamwomba amsaidie pesa alipe ada......

Mbaya zaidi nyumbani kwangu amegoma kusaidia chochote anasema si kazi yake kufanya majukumu ya kifamilia Mimi kama baba natakiwa nitekeleze kila kitu akifanya ni huruma tu.....

Kila linaloendelea kwangu anawajulisha ndugu zake ( baba, mama na Dada zake), nikichukua hatua hata za kumzaba kidogo ili tuheshimiane basi kesho asubuhi kama ilikuwa ni usiku ntapokea simu za hao watu wakinishutumu nikiwaeleza yaliyojili inaonekana mi ndo nakosea....

Amesafir kikazi wiki ya tatu sasa simu hapokei, SMS, hajibu akipokea haongei....

Namsubir arudi niite ndugu pande zote mbili niwambie nimeshindwa....kweli wanaume tumeumbwa mateso!!
 
Mfano hii story iko upande mmoja kushutumu mke it seems wqnalipiziana sasa mwanaume ndo analia hasa baada ya kuchuniwa week Tatu hivi
Nimekutana nayo sana
Tena utakuta mwanaume anaongea kwa ushupavu sana

Ila wanawake huwa wanasema basi bwana ndo imeshatokea (malipo yake sasa!)
 
Back
Top Bottom