Maamuzi magumu kwa JK ni yepi?

GAGL

JF-Expert Member
Aug 5, 2010
388
391
Jamani wa jf naomba tueleweshane hapa. UVCCM wanamtaka JK kuchukua maamuzi magumu katika masuala ya kitaifa. Mtanisamehe kama nitakuwa sikuelewa tamko lao. Lakini swali la msingi hapa ni hili, kama wanamtaka JK achukue maamuzi magumu kuhusu dowans, hivi kumfukuza kazi mtu au kumfunga kwa sababu ya wizi wa mali za umma, ni kuchukua maamuzi magumu?
 
Jamani wa jf naomba tueleweshane hapa. UVCCM wanamtaka JK kuchukua maamuzi magumu katika masuala ya kitaifa. Mtanisamehe kama nitakuwa sikuelewa tamko lao. Lakini swali la msingi hapa ni hili, kama wanamtaka JK achukue maamuzi magumu kuhusu dowans, hivi kumfukuza kazi mtu au kumfunga kwa sababu ya wizi wa mali za umma, ni kuchukua maamuzi magumu?[/QUOTE]

among other things, YES! tuone kama ana ubavu.
 
Jamani wa jf naomba tueleweshane hapa. UVCCM wanamtaka JK kuchukua maamuzi magumu katika masuala ya kitaifa. Mtanisamehe kama nitakuwa sikuelewa tamko lao. Lakini swali la msingi hapa ni hili, kama wanamtaka JK achukue maamuzi magumu kuhusu dowans, hivi kumfukuza kazi mtu au kumfunga kwa sababu ya wizi wa mali za umma, ni kuchukua maamuzi magumu?

He's remotely controlled by those political tycoons. Hivyo maamuzi ni magumu sana kwake! Kimsingi JK ni ceremonial president watendaji ni akina EL, RA etc, hivyo maamuzi sio magumu ila si yake labda wenye nayo waamue kuyachukua kitu ambacho haiwezekani wajikaange wenyewe.
 
JK ni Amiri Jeshi Mkuu (Rais), Mwenyekiti wa chama, Mwajiri mkuu, kwa kifupi ni mkuu wa kila kitu hapa Tanzania. Dowans, Katiba Mpya, utendaji mbovu wa watumishi wa umma, wizi, rushwa, vyote viko ndani ya mamlaka ya JK. tatizo ni uoga wake wa kutimiza majukumu yake ya kawaida sana kama Rais, ndio maana yanaonekana ni maamuzi magumu.
Hebu fikiria: RA, EL wana nguvu gani iliyo wazi kumzidi JK kama Rais - haiingii akilini mtu aliye chini yako akawa na nguvu isipokuwa udhaifu wako. Tunaposema achukue maamuzi magumu kimantiki tunamkumbusha kufanya kazi yake. AS SIMPLE AS THAT. Hizo ndioo kazi alizoomba kwenye kampeni si kuuza sura..
 
maamuzi magumu,labda uvccm wangetudadavulia zaid na kwa mifano pia wa hayo wanayoyaita maamuzi magumu kwa bosi wao.inawezekana kabisa kukaa kimya kwa JK ikawa ndo maamuzi magumu kwake yeye.tutafakari
 
Hamjawaelewa uvccm maamuzu magumu kwa jk kwa mustakabali wa taifa ni kujiuzulu...pekee kutaleta heshima na atasifiwa kuwa amechukua uamuzi mgumu wengi unawashinda...ona Mugabe,Gabgo etc....angeachia tu...aombe kupumzika likizo ya ugonjwa nchi ampe bilal basi
 
Naunga mkono
 
Hao UVCCM wamewalenga Sitta na Mwakyembe. Wanataka JK awafute kazi wapiganaji hawa eti kwa kupingana na mawaziri wenzao (Ni katika kupinga malipo kwa wahuni wa Dowans). Don't take UVCCM seriously, ni vibaraka tu waliotumwa na Lowassa. Nakusanya ushahidi, tukutane humu jamvini Jumatatu niwape inside story. Stay tuned.
 
Ebu ngojeni JK atakapolipuka na uamuzi wa ajabu juu ya dowans endeleeni kuchangia yeye ataconclude
 
Wanataka apunguze safari zisizo na tija kwa taifa, ili achape kazi. Suala la Richmonduli na dowans, hayo anayafahamu fika; sina uhakika kama Uvccm wanayafahamu fika hayo makampuni kumzidi mzee wa magogoni. Tafakari
 
Jamani wa jf naomba tueleweshane hapa. UVCCM wanamtaka JK kuchukua maamuzi magumu katika masuala ya kitaifa. Mtanisamehe kama nitakuwa sikuelewa tamko lao. Lakini swali la msingi hapa ni hili, kama wanamtaka JK achukue maamuzi magumu kuhusu dowans, hivi kumfukuza kazi mtu au kumfunga kwa sababu ya wizi wa mali za umma, ni kuchukua maamuzi magumu?

Jamani mimi hii naiona ni zuga ya kutosha hakuna lolote ambalo kimsingi linamantiki zaidi ya kutaka kudumaza juhudi na kazi ya wapigaji kwa kudhani kuwa UVCCM ni msaada katika juhudi za kupambana na Ufisadi na kila uozo ndani ya serikali ya mkwere.

Naamni hayo matamko ni mbinu mbadala ya kunyamazisha juhudi za wapambanaji, kiukweli tusipokaa mamcho mbinu hii itawaweka CCM mahala pazuri tu kwa kufanya wapamabanaji kubweteka. Kwa kifupi hawana msaada wowote katika kuikomboa nchi hawa ndo wale wale!!!
 
Maamuzi magumu ni haya:
1.Kumfilisi RA, maana ndiye aliyemili Richmond then Dowans.
2.Kutumia machinery yake kuwabana akina Nazir K, Msabaha, Mramba, YONA,Liyumba, Jeetu Patel et al,
3.Pia awataje wale tycoons wa drugs, maana anayo list mezani kwake
4.Amtose EL, na asikubali kuwa remotely controlled nae.
5.Atamke hadharani kuwa hatuwalipi dowans, na tuko tayari kukosa msaada wa mzungu!
6. etc.
 
He will never do that... not even in his dream.... for that will be absolutely suicidal for him. Hayo ndo matokeo ya Raisi kushirikiana na mafisadi!!
 
Back
Top Bottom