Patriot
JF-Expert Member
- Feb 11, 2008
- 5,698
- 4,693
Inasikitisha kuona kwamba serikali kupitia wizara ya Nishati na madini kitengo cha REA, inaendelea kupoteza pesa nyingi sana kwa kuhangaika kufunga umeme jua, yaani Solar energy. Kuna wakandarasi wengi sana wakitumia pesa nyimngi za mikopo wakifunga umeme wa ainahii.
Naomba niseme ni upotevu wa pesa ya serikali. Solar energy ni nzuri kwa matumizi ya familia na hasa vijijini au mijini pale tunapohitaji umeme kidogo kwa ajili ya mwanga aukuendesha mashine ndogo kabisa. Je, ktk hali hii kweli ofisi za serikali zinazohitaji umeme wa kuendesha kompyuta, friji na photocopier machines, kweli ni halali kupoteza pesa za mikopo ambazo leo zimetajwa kufikia dola milioni 10 kwa mkoa wa Tabora!
Kijiji kitashukuru sana kama kitapata umeme ili kiweze kusaga nafaka, kiweze kupasua mbao, kiweze kusukuma maji, nk. Umeme huu wa solara hauwezi kufanya hayo!