Maamuzi mabaya ya serikali kufunga solar ofisi za serikali

Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
4,984
2,000
Inasikitisha kuona kwamba serikali kupitia wizara ya Nishati na madini kitengo cha REA, inaendelea kupoteza pesa nyingi sana kwa kuhangaika kufunga umeme jua, yaani Solar energy. Kuna wakandarasi wengi sana wakitumia pesa nyimngi za mikopo wakifunga umeme wa ainahii.

Naomba niseme ni upotevu wa pesa ya serikali. Solar energy ni nzuri kwa matumizi ya familia na hasa vijijini au mijini pale tunapohitaji umeme kidogo kwa ajili ya mwanga aukuendesha mashine ndogo kabisa. Je, ktk hali hii kweli ofisi za serikali zinazohitaji umeme wa kuendesha kompyuta, friji na photocopier machines, kweli ni halali kupoteza pesa za mikopo ambazo leo zimetajwa kufikia dola milioni 10 kwa mkoa wa Tabora!

Kijiji kitashukuru sana kama kitapata umeme ili kiweze kusaga nafaka, kiweze kupasua mbao, kiweze kusukuma maji, nk. Umeme huu wa solara hauwezi kufanya hayo!
 
Henge

JF-Expert Member
May 14, 2009
6,937
2,000
sijakuelewa mkuu kunatatizo gani na solar, either huui aina ya solar au unataka kulaumu kila kitu.
 
Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,386
2,000
Tatizo wataalamu wetu wanashindwa kutumia elimu yao kutupa umeme mbadala.Biogas na hasa kutumia hata kinyesi cha binadamu,mtambo huu unaweza kutumika kutengeneza umeme wa kutosha kuliko hata solar.

Na hapo bado ukapata hata gesi ya kupikia,ni namna tu ya wataalamu wetu pamoja na serikali kujipanga kufanya maamuzi yenye akili.
 
Bobuk

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
5,873
1,500
Mbona sioni ubaya wake. Mhe. William Ngereja akiwa waziri wa Nishati na Madini aliwezesha kufunga solar power kati Vituo vva Afya na Zahanati zote zilizoko katika jimbo lake la Sengerema. Leo ukienda Sengerema ukawaambia wananchi Solar power ni kitu kibaya na ni upotezaji wa pesa bure, nina hakika WATAKUPIGA KWA MAWE! Kwa maoni yangu huu mpango ndio unaweza ukatoa feasible and practical solution vijijini (ref REA) because I'm sure ni vijiji vichache sana kama hakuna kabisa vinavyoweza kulipia gharama ya umeme wa TANESCO tunaotozwa cent za Kimarekani 40/35 kwa unit.
 
tpmazembe

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
2,470
1,225
tatizo lako unafikiri solar ziko za aina moja. kwa taarifa yako kuna solar mpaka za kuendea viwanda.
 
Elly B

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
1,194
1,195
Inasikitisha kuona kwamba serikali kupitia wizara ya Nishati na madini kitengo cha REA, inaendelea kupoteza pesa nyingi sana kwa kuhangaika kufunga umeme jua, yaani Solar energy. Kuna wakandarasi wengi sana wakitumia pesa nyimngi za mikopo wakifunga umeme wa ainahii.

Naomba niseme ni upotevu wa pesa ya serikali. Solar energy ni nzuri kwa matumizi ya familia na hasa vijijini au mijini pale tunapohitaji umeme kidogo kwa ajili ya mwanga aukuendesha mashine ndogo kabisa. Je, ktk hali hii kweli ofisi za serikali zinazohitaji umeme wa kuendesha kompyuta, friji na photocopier machines, kweli ni halali kupoteza pesa za mikopo ambazo leo zimetajwa kufikia dola milioni 10 kwa mkoa wa Tabora!

Kijiji kitashukuru sana kama kitapata umeme ili kiweze kusaga nafaka, kiweze kupasua mbao, kiweze kusukuma maji, nk. Umeme huu wa solara hauwezi kufanya hayo!

Swala la solar kama solar siyo tatizo. Au labda swala la kwamba mitambo ya solar inatoa umeme mdogo wa TV na redio kwa hiyo ni hasara, hili nalo siyo kweli sana. Ukweli ni kwamba Umeme wa solar unaweza kuwa mwingi mpaka megawati zozote anazotaka mtumiaji. Kwa kifupi ni kwamba mitambo inayofungwa itategemea unataka kutumia nyumbani, ofisini au kiwandani.

Labda swali la msingi linapaswa kuwa Ni kwa nini serikali, pamoja na kuzuia makampuni na mashirika binafsi kuzalisha umeme, imeamua kuonyesha kukatishwa tamaa kuhudumiwa na umeme wa TANESCO? Ni kwa sababu hakuna mipango ya maendeleo ya umeme? au ni kwamba TANESCO haitegemei kuongeza uzalishaji, hususan vijijini? Au ni kwa kuwa kuna mipango ya makusudi ya kuhakikisha , kama mashirika mengine, TANESCO nayo inakufa?
 
Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
4,984
2,000
tatizo lako unafikiri solar ziko za aina moja. kwa taarifa yako kuna solar mpaka za kuendea viwanda.

Ukiamua kufunga solar ya kuendesha kiwanda, unaweza, lakini linganisha bei ya kufanya hivyo na ile ya kusambaza umeme wa grid. Hakuna nchi maskini inayoweza kutumia umeme wa solar kuendesha kiwanda na hakuna nchi inayopungukiwa umeme wa njia nyingine ikakimbilia solar. It will be a nonsense.

Tatizo la Tanesco ni kutumia pesa nyingi sana kupitia REA kwa kuweka umeme ambao hauna matumizi ya maana. Najua sababu kubwa ni 10% maana kazi hiyo inafanywa na makampuni wakati umeme wa grid ni Tanesco wenyewe. Hakuna 10%.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom