Maamuzi haya vyuo vikuu ni hatari kwa taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maamuzi haya vyuo vikuu ni hatari kwa taifa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Jan 12, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,609
  Likes Received: 82,187
  Trophy Points: 280
  Maamuzi haya vyuo vikuu ni hatari kwa taifa
  Tanzania Daima~Sauti ya Watu​

  ITAKUMBUKWA kuwa Novemba 12, 2008 wanafunzi wa vyuo mbalimbali nchini walisimamishwa masomo kutokana na migomo iliyofanyika katika vyuo hivyo, ambayo wanafunzi walikuwa wakipinga sera ya uchangiaji wakitaka Bodi ya Mikopo iwalipie ada kwa asilimia 100.

  Juzi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na cha Sokoine cha Kilimo (SUA) vimetoa orodha ya wanafunzi waliokubaliwa kurudi chuoni huku ikibainika kwamba wengi wameachwa kutokana na kutokidhi masharti waliyopewa.

  Taarifa iliyotolewa na Naibu Makamu Mkuu wa UDSM, anayeshughulikia taaluma, Makenya Maboko, ilisema kati ya wanafunzi 9,000 waliorudisha fomu zilizochambuliwa, ni wanafunzi 3,000 pekee ndio waliokidhi vigezo na kutangaziwa kurudi chuoni.

  Ilisema chuo hicho kitafunguliwa Januari 19 mwaka huu na wanafunzi watakaotakiwa kuripoti, ni wale ambao majina yao yamo katika orodha iliyotolewa, kwamba wanafunzi ambao majina yao hayakutajwa katika orodha wajihesabu kuwa hawakufanikiwa na hivyo hawaruhusiwi kuingia katika mazingira ya chuo.

  Taarifa hiyo ilisema kuwa wale waliowasilisha fomu za maombi lakini hawakulipa ada ya mwaka 2008/09 wanatakiwa kulipa kiwango wanachodaiwa kupitia benki kabla ya Alhamisi ijayo.

  Kwamba kutokana na asilimia kubwa ya fomu kubainika kuwa na dosari, chuo hicho kimetoa muda hadi Alhamisi ijayo, wanafunzi hao wapatao 6,000 wawe wametatua dosari hizo, na orodha ya watakaorekebishwa itatolewa katika tovuti ya chuo Ijumaa ijayo.

  Kwa upande wa SUA, taarifa iliyotolewa imewaelekeza wanafunzi wote ambao majina yao yamo katika orodha warejee chuoni hapo kuanzia juzi hadi jana, kwamba wanafunzi ambao majina yao hayataonekana katika orodha, wajue kwamba hawakukidhi masharti ya udahili na hawatatakiwa kuripoti kwa ajili ya masomo.

  Kwetu sisi, uamuzi wa uongozi wa vyuo hivyo kuacha kuwarejesha masomoni idadi kubwa ya wanafunzi, kwa kuzingatia kigezo cha ujazaji wa fomu na sharti la ulipaji ada, haupaswi kuungwa mkono na Mtanzania yeyote mwenye kujali haki na mustakabali mwema wa taifa lake, tunasema hivyo tukizingatia yafuatayo: wanafunzi hawa waligoma wakitaka kupewa mikopo ya asilimia 100 ili walipe ada na kugharamia mahitaji yote ya kielimu, hatuoni uhalali wa serikali kukataa au kushindwa kutoa mikopo hiyo, hasa ikizingatiwa kuwa ina uwezo huo na baada ya kuhitimu, itarejeshwa.

  Wanafunzi wengi kushindwa kukidhi vigezo na masharti yaliyowekwa kwenye fomu za kuomba kurejereshwa chuoni ni kielelezo cha wazi wazi kuwa wazazi wao hawana uwezo huo na ndio maana waligoma wakiitaka serikali itoe mikopo ya asilimia 100 ili maskini hao ambao ndio wengi waweze kusoma.

  Hatua ya vyuo hivyo kuamua tu kuwachukua wanafunzi wachache walioweza kukidhi vigezo na masharti yaliyowekwa kwenye fomu hizo, inatoa tafsiri ya kibaguzi kati ya watoto wa maskini walioshindwa kukidhi masharti hayo ikiwemo sharti la kulipia ada, na watoto wa familia zinazojiweza ambao wamemudu masharti hayo.

  Kwanini tunazidi kutengeneza matabaka katika jamii? Serikali inapata faida gani kwa kuacha wanafunzi hao warudi nyumbani huku ikijua fika kuwa taifa linakabiliwa na upungufu mkubwa wa madaktari, walimu na wataalamu wengine?

  Ni rai yetu kwa serikali na wadau wote wa elimu nchini, kuingilia kati kwa mazungumzo ili wanafunzi hao waweze kurejea chuoni, vinginevyo maamuzi haya ya vyuo vikuu ni hatari mno kwa amani na mustakabali wa maendeleo ya taifa letu.
   
 2. G

  Giroy Member

  #2
  Jan 12, 2009
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sioni kama serikali yetu ina nia ya dhati ya kuelimisha wananchi wake.kwangu mimi naona ni matunda sisiemu ambao ni watawala wetu.chama hicho ambacho uchaguzi wake wa vijana unachangiwa mamia ya milioni na magabacholi unategemea kitakutetea wewe kijiji uliyetoka namtumbo au kasulu! Hawa jamaa sijasikia wanachangia shule, wao mpira na sisiemu.wakati wenzetu wanaongeza idadi ya wasomi kwa kasi sisi ndiyo kwanza tunaipunguza!sawa awazee nchi hii yenu,mtakavyoamua ndivyo itakavyokuwa.idadi yawasomi ikiongezeka hamtaweza kuwatawala vizuri.
   
 3. m

  mayers Member

  #3
  May 18, 2014
  Joined: Nov 28, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kumbukeni senate zote zimejaa maprofesa wa kitanzania wenye damu ya chama kinachoitwa revolution partyn yaani ccm hili nalo ni tanzani wasomi wa tanzania ------------ na wanasiasa hawatoi maamuzisahii jiulize rahasha kama nao wengifukuzwa wakati wanadai haki zao ingekajehapo? Tatzo no kwamba wengi wa maprofesa wetu wanakalili sana elimu zao yaani walikuwa wanauwezo mkubwa wa kukalili ila hawana knowledge watawezaje kutoa maamuzi ya kuwatete wanafunzi wa kitanzania ndani ya nchi yao yapo yamekaa kuchambua form then hapo hapo yametumia kodi za watanznia kulipwa posho kwa ajili ya kutowarudisha watoto wetu vyoni
   
 4. aloycious

  aloycious JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2014
  Joined: Dec 17, 2012
  Messages: 5,522
  Likes Received: 388
  Trophy Points: 180
  Hatari sana hii nchi! Vijana hatuna kuikataa selikali iliyopo madarakani.
   
Loading...