Maamuzi ambayo siyajutii

Bahati nzuri sijawahi fanya kazi rahisi kama unavyofikiri.
Mimi huvumilia mahali panspo lipa, huwa nasaka maarifa na sio kazi maandazi.
Nenda Saudia Arabia ukafanye kazi za nyumbani ndiyo kunakufaa. Binadamu unaamua kuuza utu wako kwa sababu ya njaa? Umnyenyekee mtu mmoja kwani yeye ndiye yuko hapa duniani peke yake? Bora nifanye kazi ya kupasua mawe kuliko kufanya kazi ya umeneja huku utu wangu unadhalilishwa.
 
Mara nyingine uko too harsh for nothing
Nenda Saudia Arabia ukafanye kazi za nyumbani ndiyo kunakufaa. Binadamu unaamua kuuza utu wako kwa sababu ya njaa? Umnyenyekee mtu mmoja kwani yeye ndiye yuko hapa duniani peke yake? Bora nifanye kazi ya kupasua mawe kuliko kufanya kazi ya umeneja huku utu wangu unadhalilishwa.
 
Bahati nzuri sijawahi fanya kazi rahisi kama unavyofikiri.
Mimi huvumilia mahali panspo lipa, huwa nasaka maarifa na sio kazi maandazi.
Sasa kwanini unamdanganya mwenzako avumilie unyanyasaji usio na malipo? Ni kweli kuna sehemu mtu unaweza kuvaa miwani ya mbao kwa sababu unajua unapata, lakini kwa kesi ya huyu alivyoeleza siwezi kumshauri avumilie ujinga kama huo.
 
Stori yako inafanana na ya mrembo flani naye amefanyiwa figusi kama hizi naye kashtuka ameafanya usaili mahali ili kuhakikisha kikinuka ana pa kujishikiza
ahahahaha.maisha ni kuviziana mkuu. muda wowote ukizubaa unaliwa kichwa
 
Nimekupa like tangu lakini jifunze hakuna urafiki wa kudumu kati ya mwajiri na mfanyakazi.....ulijidekeza sana jitahidi kuwa mwanaume hupaswi kuwa much loyal to others. Soma sana vitabu how to influence people and winning friends....hukupaswa kuonyesha kuwa kuna namna unafaidika jifunze
Za mida hii wakuu.

Nimekuwa nikifanya kazi kwa kujitolea katika taasisi fulani, kwa muda wa miezi kadhaa, ikiwa mpaka sasa nimeacha kazi eneo hilo.

Nilipokuwa kwenye kitengo cha wajawazito, nilihusika na kutoa huduma na ushauri juu ya umuhimu wa kufanya ultrasound pale inapohitajika, huduma hiyo ilikuwa ikiletwa na mtu wa kutoka nje ya taasisi, hivyo akihitajika anakuja, halafu anaacha kiasi fulani cha kwenye ofisi.

Ilifika kipindi mtaalamu huyo aliniambia kuwa atamfanyia ultrasound mwanamke wangu ambaye ni mjamzito, kwa sababu mimi ni staff wa eneo hilo na pili nimekuwa nikimfikishia wateja wa kutosha, ila anilipa kigezo kwamba akipatikana mjamzito mwingine wa kulipia ndio nimuite na wa kwangu aje amfanyie, ili asiwe ametoka umbali mrefu kwa ajili ya kuja kufanya ya bila malipo, nikamwambia sawa

Siku ya jana alipatikana anayehitaji ultrasound, basi nikamuita huyo mtaalamu, na vile vile nikamuita mwanamke wangu ambaye ni mjamzito, sikuwa zamu ila niliingia kwa ajili ya hilo, muda nafika getini nikamkuta Manager getini, akaniuliza Vipi uko zamu?nikamjibu Hapana, akaniuliza kuna shida gani Nikamueleza kuna jambo limenileta, halafu nikaingia.

Nikawa nimeingia ndani na kuwaweka tayari yule mteja pamoja na mwanamke wangu kwa maandalizi ya awali ya kufanya ultrasound, baada ya hapo nikaenda kwa manager, kumpa taarifa juu ya lile suala maana yeye ndio anayepokea pesa eneo lile asije kuona mtu wangu anaingia na kutoka pasipo kuelewa inakuwaje.

Baada ya kumueleza manager akaanza kunifokea, mbele ya wagonjwa hapo akiwepo mwanamke wangu, kwa sauti, akisema kwamba hicho kitu hakiwezi kufanyika katika hospitali yake, kama nimeelewana na yule mtaalamu ningeenda nikafanyie Guest au Nyumbani, kama ni hapo hospitali nilipie, huku akiendelea kutoa maneno ya kashfa na kudhalilisha, nikajisikia vibaya sana nikamrudishia maneno, nikamwambia isiwe shida nitalipa ila baada ya hapo nitaacha kujitolea eneo hilo.

Basi mwanamke wangu akapimwa na majibu yakatoka nikamsindikiza niliporudi nikawakusanya staff wenzangu akiwepo na manager nikawaambia dhumuni langu la kuacha kazi, manager akaanza kuniambia kwanza nimekosea hata kuingia kazini na sipo zamu mlinzi angekuwepo angenikamata, nikamueleza hakuna sheria ya hivyo, na amekosea sana kunidhalilisha mbele ya wagonjwa nilipoenda kumuelezea shida yangu, hivyo sitoweza kuendelea kujitolea eneo hilo, nikaandika barua ikiwa na sababu ya kuacha kujitolea eneo hilo kwa sababu ya kudhalilishwa na manager, nikamkabidhi barua mbele ya kikao, nikaaga staff wenzangu, nikaondoka.
 
Mkuu kuna kujitolea kwa lazima, huyu hajitolei sababu ameamua bali ni sehemu ya kukamilisha masomo yake, yaani kutengeneza uzoefu ksbla ya kuomba ajira, tufikiri kwa undani...amrkosea kuwa mlaini kiasi hicho.
Ona amedhalilishwa na ameacha kaxi, amefaidi nini?
Kama alikasirika basi angemtwanga ngumi huyo mwajiri.
Vinginevyo kazi hana na smeondoka na aibu zake.
Maisha sio ya watu walaini na wepesi kiasi hicho.
Sikuwa najitolea kwa lazima kukamilisha masomo, mimi nilishamaliza masomo, hiari yangu ilikuwa kujitolea, si kila mhitimu lazima ajitolee.
 
Hasira hasara ujue!!
Sasa muda wote uliofanya kazi hapo nani atakuandikia rikomendesheni?
Sikuwa natafuta recommendation.

Nilikuwa natafuta Maarifa ya kuweka kichwani na sio barua ya kutembeza nionekane nimefanya kazi wapi na wapi.
 
Nenda Saudia Arabia ukafanye kazi za nyumbani ndiyo kunakufaa. Binadamu unaamua kuuza utu wako kwa sababu ya njaa? Umnyenyekee mtu mmoja kwani yeye ndiye yuko hapa duniani peke yake? Bora nifanye kazi ya kupasua mawe kuliko kufanya kazi ya umeneja huku utu wangu unadhalilishwa.
Ndio nilichokataa mkuu siwezi kudhalilisha utu wangu kwa kazi ya kujitolea.
 
Back
Top Bottom