Maamuzi ambayo siyajutii

Deva

JF-Expert Member
May 29, 2018
1,238
1,801
Za mida hii wakuu.

Nimekuwa nikifanya kazi kwa kujitolea katika taasisi fulani, kwa muda wa miezi kadhaa, ikiwa mpaka sasa nimeacha kazi eneo hilo.

Nilipokuwa kwenye kitengo cha wajawazito, nilihusika na kutoa huduma na ushauri juu ya umuhimu wa kufanya ultrasound pale inapohitajika, huduma hiyo ilikuwa ikiletwa na mtu wa kutoka nje ya taasisi, hivyo akihitajika anakuja, halafu anaacha kiasi fulani cha kwenye ofisi.

Ilifika kipindi mtaalamu huyo aliniambia kuwa atamfanyia ultrasound mwanamke wangu ambaye ni mjamzito, kwa sababu mimi ni staff wa eneo hilo na pili nimekuwa nikimfikishia wateja wa kutosha, ila anilipa kigezo kwamba akipatikana mjamzito mwingine wa kulipia ndio nimuite na wa kwangu aje amfanyie, ili asiwe ametoka umbali mrefu kwa ajili ya kuja kufanya ya bila malipo, nikamwambia sawa

Siku ya jana alipatikana anayehitaji ultrasound, basi nikamuita huyo mtaalamu, na vile vile nikamuita mwanamke wangu ambaye ni mjamzito, sikuwa zamu ila niliingia kwa ajili ya hilo, muda nafika getini nikamkuta Manager getini, akaniuliza Vipi uko zamu?nikamjibu Hapana, akaniuliza kuna shida gani Nikamueleza kuna jambo limenileta, halafu nikaingia.

Nikawa nimeingia ndani na kuwaweka tayari yule mteja pamoja na mwanamke wangu kwa maandalizi ya awali ya kufanya ultrasound, baada ya hapo nikaenda kwa manager, kumpa taarifa juu ya lile suala maana yeye ndio anayepokea pesa eneo lile asije kuona mtu wangu anaingia na kutoka pasipo kuelewa inakuwaje.

Baada ya kumueleza manager akaanza kunifokea, mbele ya wagonjwa hapo akiwepo mwanamke wangu, kwa sauti, akisema kwamba hicho kitu hakiwezi kufanyika katika hospitali yake, kama nimeelewana na yule mtaalamu ningeenda nikafanyie Guest au Nyumbani, kama ni hapo hospitali nilipie, huku akiendelea kutoa maneno ya kashfa na kudhalilisha, nikajisikia vibaya sana nikamrudishia maneno, nikamwambia isiwe shida nitalipa ila baada ya hapo nitaacha kujitolea eneo hilo.

Basi mwanamke wangu akapimwa na majibu yakatoka nikamsindikiza niliporudi nikawakusanya staff wenzangu akiwepo na manager nikawaambia dhumuni langu la kuacha kazi, manager akaanza kuniambia kwanza nimekosea hata kuingia kazini na sipo zamu mlinzi angekuwepo angenikamata, nikamueleza hakuna sheria ya hivyo, na amekosea sana kunidhalilisha mbele ya wagonjwa nilipoenda kumuelezea shida yangu, hivyo sitoweza kuendelea kujitolea eneo hilo, nikaandika barua ikiwa na sababu ya kuacha kujitolea eneo hilo kwa sababu ya kudhalilishwa na manager, nikamkabidhi barua mbele ya kikao, nikaaga staff wenzangu, nikaondoka.
 
Ukweli unaponza, hapa duniani ukiwa mkweli kwenye kila jambo utateseka sana.ungewahudumia ukatoka ukakabidhi pesa ya mtu mmoja ukatoka na mkeo, usingeulizwa na ungeulizwa ungewaambia nimepita kumhudumia huyu mgonjwa mm na wife tunatoka kuna sehemu tunaenda.

Tafuta kazi uajiriwe, Huyo mpuuzi Meneja angekuwa umeajiriwa asingekufokea hivyo mbele za wagonjwa, kama umekosea ilibidi akuite ofisini muyamalize kimya kimya.

Hayo maamuzi nimeyapenda yanakupa hasira za kujiajiri hata kama huna mtaji pambana.
 
Kwa kauli ndogo tu hizo unaacha kazi?

wewe hujakutana na maboss na kauli zao, hapa nilipo jana tu nilipigwa matusi ya nguoni tena wife nafanya nae kazi tulikua kikao akisikia kila kitu na muda huu tunarudi kazi kama kawaida

mabosi ndivyo walivyo,,,uamuzi uliochukua utaujutia baadae
 
Mkuu ulikuwa soft sana, ulipaswa upachimbe vizuri. Kwenye kikao wakati ukiongea ulipaswa umuweke menaja chini ya ulinzi kwa kumkwida shati, kwa kuchanganyikiwa angeweza kutoa maelekezo wafanyakazi waanze kuripoti kwako. Kumwacha hivi hivi ni kumpa ushindi wa mezani.
 
kazi ya kujitolea unaandika barua ya kuacha ya nini, we unaondoka zako tu bila hata kuaga, mi niliacha bila kumuaga yoyote, kujitolea ni upuuzi zinawafaa wanawake maana wanadanga kwa wafanyakaz, kwa mwanaume bora uuze kahawa mtaan kujiko kujitolea
 
Kwa kauli ndogo tu hizo unaacha kazi?

wewe hujakutana na maboss na kauli zao, hapa nilipo jana tu nilipigwa matusi ya nguoni tena wife nafanya nae kazi tulikua kikao akisikia kila kitu na muda huu tunarudi kazi kama kawaida

mabosi ndivyo walivyo,,,uamuzi uliochukua utaujutia baadae
Siwezi kuujutia kwa maana sikuajiriwa bali nilikuwa najitolea bila malipo yoyote, hata nauli sikuwa napata.
 
kazi ya kujitolea unaandika barua ya kuacha ya nini, we unaondoka zako tu bila hata kuaga, mi niliacha bila kumuaga yoyote, kujitolea ni upuuzi zinawafaa wanawake maana wanadanga kwa wafanyakaz, kwa mwanaume bora uuze kahawa mtaan kujiko kujitolea
Kweli kabisa mkuu,
 
Back
Top Bottom