Maambukizi mapya ya Virusi Vya UKIMWI yamepungua kutoka 130,000 mpaka 68,400 kwa mwaka

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) imesema maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi yamepungua kutoka 130,000 mpaka 68,400 kwa mwaka kutokana na elimu inayoendelea kutolewa kwa wananchi ya kujikinga na maambukizi hayo.

Mkurugenzi wa tume hiyo, Dk Leonard Maboko, amesema hayo leo Noemba 24, 2020 alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu siku ya ukimwi duniani inayoadhimishwa Desemba mosi kila mwaka. Maadhimisho ya mwaka huu kitaifa yatafanyika mkoani Kilimanjaro.

"Takwimu za mwaka 2001 mpaka 2019 zinaonyesha idadi ya vifo kwa watu wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi imepungua kutoka vifo 85,000 mpaka 25,000 mwaka 2019 kutokana na watu wenye maambukizi kupata elimu ya umuhimu wa matumizi ya dawa za kufubaza virusi,”amesema Dk.Maboko.

Amesema njia pekee ya kupunguza na kuzuia maambukizi mapya ni elimu kwa wananchi hususani vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 ambao wengi wao wako hatarini kupata maambukizi.

Pi amesema matumizi sahihi ya dawa za kufubaza virusi hivyo (ARV) yanasaidia kupungua kuenea kwa maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi.

Kuhusu unyanyapaa kwa watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi, amesema tume na mashirika mbalimbali wamekua wakielekeza nguvu kubwa katika utoaji elimu kwamba nao wanastahili kupata haki zotwe za msingi kama ilivyo kwa watu wengine.

Mwenyekiti wa Baraza la watu wanaoishi na virusi vya ukimwi nchini (NACOPHA), Leticia Maurice ameishukuru Serikali kwa jitihada za kutoa bure vifaa tiba, dawa pamoja na elimu kwa jamii.

Amesema kama kaulimbiu ya maamdhimisho ya mwaka huu inavyosema “Mshikamano wa kimataifa tuwajibike kwa pamoja”, baraza hilo nalo wamejipanga kutoa elimu ikiwemo ya kujikinga na maambukizi ya ukimwi pamoja na kuhamasisha ujasiriamali.


Mwananchi
 
Hivyo vifo ni kwa mwaka au mwezi au siku? Na hiyo namba ya maambukizi kama ni kwa mwaka basi nchi hii hakuna ukimwi tunatishana sana kuliko uhalisia
 
Ile ya week kadhaa ina sema viwango vimeongezeka, Leo vimepungua...
 
Sasa wewe Kama unafikiri maambukizi yamepungua kula nyama nyama uone Moto.
Ssiku hizi umeona kila ukipima malaria unaambiwa huna lkn homa unalo. Ukinywa metakelfin homa inakwisha.
Hizi takwimu zisitubweteshe.
Unaambiwa mfumuko wa Bei umepungua lkn ukiingia sokoni na elfu kumi hairudi.
 

Kutoka 130,000 mpaka 60,000s... Lakini kila mwaka ina kadiliwa maambukizi mapya 70,000 kila mwaka hachana na maambukizi yaliyopo kwa wakati huo...
 
Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) imesema maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi yamepungua kutoka 130,000 mpaka 68,400 kwa mwaka kutokana na elimu inayoendelea kutolewa kwa wananchi ya kujikinga na maambukizi hayo.

Mie sidhani kama hiyo sababu ni ya kweli, hiyo elimu wanatoa wapi na kwa nani na lini, labda wangesema chanzo ni uchumi kukaba sana na matanuzi kupungua
 
Back
Top Bottom