Maambukizi Katika Mfumo wa Uzazi wa Mwanamke (PID) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maambukizi Katika Mfumo wa Uzazi wa Mwanamke (PID)

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Oct 25, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  PELVIC INFLAMATORY DISEASES.jpg

  Maambukizi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke kwa kitaalamu Pelvic Inflamatory Diseases au kwa kifupi PID, ni moja ya matatizo ambayo huwaathiri sana wanawake. Kwa kawaida maambukizi haya huusisha shingo ya uzazi (cervix) hali ambayo hujulikana kama cervicitis, nyama ya mfuko wa uzazi (endometrium) ambayo kitaalamu huitwa endometritis, na mirija ya uzazi (fallopian tubes) hali ijulikanayo kitabibu kama salpingitis.  PID husababishwa na nini?

  Pamoja na aina kadhaa za vimelea kuhusishwa na PID, vimelea vya jamii ya Neisseria Gonorrhoeae pamoja na Chlamydia trachomatis ndivyo vinavyoongoza kwa umaarufu zaidi katika kusababisha PID kwa akina mama.


  Je mwanamke huambukizwaje PID?


  Kuna njia kadhaa ambazo mwanamke anaweza kuambukizwa PID. Njia hizo ni pamoja na

  • Kufanya ngono isiyo salama
  • Maambukizi ya njia ya uzazi hasa kipindi mara baada ya kujifungua (au postpartum period)
  • Maambukizi ya njia ya uzazi mara baada ya kutoa mimba kwa njia zisizo salama (post abortion) au mara baada ya mimba kutoka (miscarriage)
  • Kutumia vipandikizi vya ndani ya mfuko wa uzazi (IUCD) kama njia mojawapo ya uzazi wa mpango, na
  • Kuambukizwa kupitia damu iliyo na vimelea vya PID.
  Dalili za PID ni zipi?
  Zipo dalili kadhaa za ugonjwa huu wa PID. Miongoni mwa dalili hizi ni
  • Mwanamke kuhisi maumivu ya tumbo hasa maeneo ya chini ya kitovu
  • Kupata maumivu ya mgongo
  • Mwanamke kupata utoko mchafu sehemu za siri. Utoko huu huambatana na harufu mbaya.
  • Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
  • Kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa
  • Kutoka damu bila mpangilio wakati wa hedhi
  • Kupata homa
  • Wakati fulani kuhisi kichefuchefu na
  • Pia kutapika
  Vipimo vya PID
  Ili kuweza kutambua kama mwanamke ameambukizwa ugonjwa huu, tabibu anaweza kufanya vipimo kadhaa vikiwemo
  • Kuchunguza mkojo ili kufahamu kama mgonjwa ana mimba. Kipimo hiki ni muhimu hasa kwa mwanamke aliye katika umri wa kuzaa au mwenye uwezo wa kubeba mimba
  • Uchunguzi wa mkojo kwenye darubini ili kutambua aina za vimelea vinavyomletea mgonjwa uambukizi. Aidha mkojo huweza kuoteshwa katika maabara kwa ajili ya kutambua aina nyingine za vimelea viletavyo uambukizi huo.
  • Kupima damu kwa ajili ya kuchunguza jinsi aina mbalimbali za chembe za damu zilivyoathiriwa na uambukizi huo au kama kuna mwingiliano na magonjwa mengine yaliyojificha. Kipimo hiki kwa kitaalamu huitwa Full Blood Picture.
  • Kuchukua utando unaozunguka shingo ya uzazi na kuuotesha kwa ajili ya utambuzi wa aina za vimelea viletavyo maambukizi hayo. Kipimo hiki huitwa cervical culture
  • Aidha ni muhimu pia kufanya vipimo vingine kwa ajili ya utambuzi wa magonjwa yaambukizwayo kwa njia ya kujamiiana, kama vile virusi vya ukimwi na kisonono.
  • Mgonjwa pia anaweza kufanyiwa ultrasound ya nyonga ili kuangalia kama kuna athari yeyote katika mfumo wake wa uzazi.
  Matibabu
  Mara mgonjwa anapogunduliwa kuwa ameathiriwa na ugonjwa huu, dawa za jamii ya antibayotiki huweza kutumika kwa ajili ya kuua vimelea vya ugonjwa. Hata hivyo ieleweke kuwa matumizi ya dawa hizi hufuata miongozo mbalimbali ambayo imewekwa na wizara au mamlaka za afya zinazohusika. Miongozo hii hutofautiana kati ya sehemu na sehemu au nchi na nchi, ingawa kiujumla Shirika la Afya Duniani (WHO) nalo limeweka muongozo wake kwa ajili ya kufuatwa na nchi mbalimbali.

  Miongoni mwa dawa hizo ni pamoja na Cefotetan na Doxycycline; Clindamycin pamoja na Gentamycin; Ampicillin na Sulbactam kwa pamoja na Doxycycline; na Ceftriaxone au Cefoxitin pamoja na Doxycycline.
  Ieleweke pia haishauriwi kujinunulia na kutumia dawa hizi bila kupata ushauri ushauri wa mtaalamu wa afya. Aidha ili kuondoa maumivu na kushusha homa, dawa kama Paracetamol (Panadol) yaweza kutumika.


  Jinsi ya kuzuia maambukizi katika mfumo wa uzazi


  Kuna njia kadhaa za kuzuia maambukizi katika mfumo wa uzazi. Njia hizi ni pamoja na

  • Kufanya ngono salama kwa kutumia kondomu au kama ikiwezekana kujizuia kabisa kufanya ngono.
  • Kuwahi kuwaona wataalamu wa afya mara dalili za ugonjwa huu zinapoanza kujitokeza au pindi tu unapogundua kuwa mwenzi wako ana dalili za magonjwa ya zinaa
  • Kufanya vipimo mara kwa mara hasa vya mfumo wa uzazi, pamoja na vipimo vya maambukizi ya magonjwa yanayosambazwa kwa njia ya ngono (STI).
  • Kutofanya ngono mara baada ya kujifungua, mimba kutoka au mara baada ya kutoa mimba ili kuhakikisha njia ya shingo ya uzazi imefunga vema.


  Ukiwa na Shida yoyote ile
  Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu
  Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe. fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169
   
 2. D

  Deborita Member

  #2
  May 9, 2014
  Joined: Sep 10, 2013
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadau naomba kujua chanzo,dalili na jinsi ya kuzuia tatizo hili la PID(pelvic infections).Madaktar au yeyote mwenye ujuz naomba msaada wenu
   
 3. gorgeousmimi

  gorgeousmimi JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2014
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 8,839
  Likes Received: 321
  Trophy Points: 180
  [FONT=Arial, Verdana, Helvetica, sans-serif]Pelvic inflammatory disease(PID) inasababishwa na infection kwenye viungo vya uzazi vya mwanamke.PID inasababishwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa kwa wanake na hatimae kupelekea majeraha yasiyorekebishika kwenye mfuko wa uzazi,mirija ya uzazi ,mayai au hata viungo vingine vya uzazi.Matatizo haya yanaweza kupelekea hata ugumba.[/FONT]

  Nini inasababisha ugonjwa huu?
  [FONT=Arial, Verdana, Helvetica, sans-serif]​Kawaida (Cervix)mlango wa uzazi unazuia bacteria wanaotoka kwenye uke kuingia kwenye viungo via uzazi.
  Kama mlango wa uzazi umeathirika na magonjwa ya zinaa kama kisonono au klamidia,mlango huo unapata infections/unadhurika na hatimae kushindwa kuzuia vijidudu kutoka kwenye uke kusambaa kwenye kizazi.Magonjwa kama kisonono na klamidia ndio yanasababisha kwa asilimia 90%.Sababu nyingine ni kutoa ujauzito/mimba,kuzaa/kujfungua na uchunguzi wa kwenye eneo hilo(kimatibabu)
  [/FONT].
  cervix.jpg
  [FONT=Arial, Verdana, Helvetica, sans-serif]
  Dalili zake ni zipi:
  [/FONT]
  • Maumivu kwenye eneo la chini/juu la tumbo
  • Kutokwa na "Vaginal disharge" zenye rangi ya njano au kijani na zenye harufu isio ya kawaida
  • Maumivu wakati wa kujisaidia haja ndogo
  • Homa kali
  • Kichefuchefu na kutapika
  • Maumivu wakati wa kujamiiana
  Mambo yanayomuweka mwanamke katika kundi la kupata PID

  • Wanawake wenye maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama kisonono na klamidia
  • Wanawake walopata maabukizi ya PID awali,wana athari kubwa ya kupata gonjwa hilo tena
  • Wanawake walio "SEXUALLY ACTIVE"
  • Wanawake walio na wenza wengi,zaidi ya mmoja.


   
 4. D

  Deborita Member

  #4
  May 11, 2014
  Joined: Sep 10, 2013
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asante kwa maelezo,na tiba yake huwa ni nini?
   
 5. gorgeousmimi

  gorgeousmimi JF-Expert Member

  #5
  May 11, 2014
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 8,839
  Likes Received: 321
  Trophy Points: 180
  Tiba yake ni antibiotics au surgery kama eneo hilo kama limetengeneza majipu/abscess
   
 6. halati88

  halati88 JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2014
  Joined: Apr 4, 2014
  Messages: 462
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Habari zenu wadau, madokta wa jf ninaombeni msaada kuhusu hilo gonjwa hapo juu,mimi binafsi silielewi hili gonjwa vizuri,ila mdogo wangu anasumbuliwa na huu ugonjwa kwa muda mrefu,mimi alichonieleza ni kwamba kila anapokutana kimwili na mume wake anapata u.t.i na anatokwa maji maji mengi ukeni,amehangaika sana hospital bila mafanikio na alimpata specialist mmoja huko kerege akaambiwa kwamba ni bacteria ndio wameshambulia maeneo ya kizazi,walimpatia dawa akapata nafuu sasa hivi vimerudi upya tena,naombeni msaada wenu madokta au kama kuna anaemfahamu specialist mzuri wa magonjwa hayo tumuelekeze,maana ndoa yake ipo hatarini mume kachoka kunywa dawa za u.t.i kila mara. Naomba mnisamehe kwa uandishi mbaya natumia kimeo.
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Dec 16, 2014
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280

  UGONJWA WA KWENYE MFUMO WA UZAZI WA MWANAMKE (PELVIC INFLAMATORY DISEASES)


  [​IMG]

  MAAMBUKIZI ugonjwa wa kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke (Pelvic Inflamatory Diseases) ambao pia hujulikana kama shingo ya uzazi (kitaalamu huitwa cervix) ambayo hujulikana kwa jina la cervicitis hutesa sana wanawake wengi wenye umri mbalimbali.


  Maambukizi hayo husambaa hadi kwenye mfuko wa uzazi (endometrium) ambayo kitaalamu huitwa endometritis na mirija ya uzazi (fallopian tubes) hali ijulikanayo kitabibu kama salpingitis.
  Ugonjwa huu husababishwa na vimelea vya jamii ya Neisseria Gonorrhoeae pamoja na Chlamydia Trachomatis ndivyo vinavyosababisha ugonjwa huu kwa akina mama na wataalamu huuita Pelvic Inflamatory Diseases (PID) yanayotokea kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke.
  Kuna njia kadhaa ambazo mwanamke anaweza kuambukizwa ugonjwa huu, njia hizo ni pamoja na kufanya ngono isiyo salama, maambukizi ya njia ya uzazi hasa baada ya kujifungua.
  Wanawake wanaotoa mimba kwa njia zisizo salama, wana uwezekano wa kupata maambukizi au wale ambao mimba hutoka (miscarriage) au wakipewa damu iliyo na vimelea vya maambukizi.
  Dalili za ugonjwa huu
  Dalili za ugonjwa huu wa PID ni nyingi kama vile mwanamke kuhisi maumivu ya tumbo hasa maeneo ya chini ya kitovu, kupata maumivu ya mgongo au mwanamke kutokwa na uchafu wenye harufu sehemu za siri.
  Kuna dalili nyingine kama vile kuhisi maumivu wakati wa kukojoa au wakati wa tendo la ndoa. Kutoka damu bila mpangilio wakati wa hedhi na mgonjwa kuwa na homa na kuhisi kichefuchefu au kutapika.
  Mwanamke aliyeambukizwa maradhi haya ya maambukizi, anaweza kufanya vipimo kwa kuchunguza mkojo ili kufahamu kama mgonjwa ana mimba.
  Mkojo huchunguzwa na darubini ili kutambua aina za vimelea vinavyomletea mgonjwa maambukizi.
  Kuna kipimo kiitwacho kitaalamu Full Blood Picture hutumika ili kujua aina mbalimbali za chembe za damu zilivyoathiriwa na maambukizi hayo au kama kuna mwingiliano na magonjwa mengine yaliyojificha.
  Daktari anaweza kujua kama mgonjwa ana maradhi haya kwa kuchukua utando unaozunguka shingo ya uzazi na kuuotesha kwa ajili ya utambuzi wa aina za vimelea viletavyo maambukizi hayo. Kipimo hiki huitwa cervical culture.
  Mgonjwa pia anaweza kufanya vipimo vingine ili kujua kama ana maambukizi ya magonjwa yatokanayo na kujamiiana, kama vile virusi vya ukimwi na kisonono. Mgonjwa pia anaweza kufanyiwa ultrasound ya nyonga ili kuangalia kama kuna athari yoyote katika mfumo wake wa uzazi.
  Matibabu
  Mara mgonjwa anapogunduliwa kuwa ana magonjwa hayo, atatibiwa na dawa za jamii ya antibayotiki ili kuua vimelea vya ugonjwa.
  Dawa za maradhi haya zipo nyingi kama vile Cefoxitin pamoja na Doxycycline, Cefotetan na Doxycycline; Clindamycin pamoja na Gentamycin; Ampicillin nakadhalika. Tunashauri kuwa dawa hizi zinunuliwe kwa kushauriwa na daktari.
  Ushauri
  Kuna njia kadhaa zinazoshauriwa kuzuia maambukizi katika mfumo wa uzazi kama vile kufanya ngono salama kwa kutumia kondomu au kujizuia kabisa kufanya ngono, kuwahi kuwaona wataalamu wa afya mara dalili za ugonjwa huu zinapoanza kujitokeza na kupimwa vipimo vya maambukizi ya magonjwa yanayosambazwa kwa njia ya ngono (STI).

  Ukiwa na Shida yoyote ile
  Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu
  Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe. fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169
   
 8. halati88

  halati88 JF-Expert Member

  #8
  Dec 16, 2014
  Joined: Apr 4, 2014
  Messages: 462
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Asante sana MziziMkavu tutakutafuta sasa nimeelewa kuhusu huu ugonjwa, amepima vipimo vyote H.i.v magonjwa ya zinaa hamna yani anakunywa dawa mpaka anasema nyingine hazikumbuki hata majina.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. deebo

  deebo JF-Expert Member

  #9
  Dec 17, 2014
  Joined: Sep 25, 2013
  Messages: 329
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  Pid ni tatizo linalo sababishwa na untreated u.t.i inayosababishwa na bacteria. Yaan ktk stage hiyo hiyo bacteria wanakua wamesha fika kwenye mfuko wa uzazi na kushambulia ovary na mirija ya uzazi.. hali hii usababisha hizi sehem kupata chronic inflamation...pia ureter na figo zinakua ktk mashambulizi ya bacteria hao....

  Ushauri;
  Aende kupima ili kubaini exactly ni aina gan ya bacteria pia kufanyiwa sensitivity kwa dawa tofauti ili kubain best dawa ya kumpa...asikimbilie antibiotics ovyo kwan ndo zinaweza kuongeza tatizo... see lab scientists atasaidia zoezi hili..
   
 10. deebo

  deebo JF-Expert Member

  #10
  Dec 17, 2014
  Joined: Sep 25, 2013
  Messages: 329
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  Na kama kisha kunywa madawa ovyo inaelekea hao bacteria wame develop multidrug resistance... nadhan inahitajika sayansi nzito ya kimaabara ya kubaini combination ya dawa zitazo saidia yy kupona....kama tatizo litaendelea kuzembewa meanz atapoteza hata uwezo wa kuzaa
   
 11. halati88

  halati88 JF-Expert Member

  #11
  Dec 17, 2014
  Joined: Apr 4, 2014
  Messages: 462
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Asante mkuu,sasa unamshauri aende hospital gani maana sasa hivi mumewe hana ushirikiano kiivyo anakuwa km anamnyanyapaa.
   
 12. m

  mushi b New Member

  #12
  Feb 24, 2017
  Joined: Dec 9, 2016
  Messages: 1
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
   
Loading...