#COVID19 Maambukizi Afrika Kusini yameongezeka maradufu. Visa 8,500 vyarekodiwa ndani ya saa 24

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Afrika Kusini imerekodi ongezeko kubwa la maambukizi ya virusi vya corona ambayo yameongezeka maradufu kote nchini humo tangu Jumatatu.

Maafisa wa afya wanasema aina mpya ya Omicron iliyogunduliwa inaweza kuwa inachochea kuongezeka, ingawa haijulikani wazi ni watu wangapi kati ya wenye maambukizi ya kirusi kipya.

Baadhi ya maambukizi 8,500 ya Covid yamesajiliwa katika saa 24 zilizopita.

Afrika Kusini ilikuwa nchi ya kwanza kugundua aina mpya ambayo ilitangazwa wiki iliyopita.

Marekani imebaini mtu wa kwanza mwenye kirusi cha Omicronkisa kwa mtu ambaye alikuwa amerejea nchini kutoka Afrika Kusini.

Maswali mengi kuhusu kirusi kipya bado hayajajibiwa, ikiwa ni pamoja na iwapo inaweza kuambukizwa zaidi na ni ulinzi wa kiasi gani chanjo za sasa zinatoa.

BBC Swahili
 
Back
Top Bottom