Maalum kwa ajili ya wanyama pori

Sawa mkuu....Ni kweli koboko ni nyoka mkorofi au ni mpaka uingie anga zake?

Sent using Jamii Forums mobile app
Yani huyo ni hatari sana kingereza huitwa black mamba ana sumu kali haina cardiotoxic ambayo inasimamisha mapigo ya moyo na within 20 minutes unakufa ikiwa ni single bite! Ni mkorofi sana anaweza kusimamisha robo tatu ya mwili wake ili akudunge usoni! Na ni nyoka mwenye tabia ya kumkimbiza binadamu! Kwa africa ni nyoka hatari zaid

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani huyo ni hatari sana kingereza huitwa black mamba ana sumu kali haina cardiotoxic ambayo inasimamisha mapigo ya moyo na within 20 minutes unakufa ikiwa ni single bite! Ni mkorofi sana anaweza kusimamisha robo tatu ya mwili wake ili akudunge usoni! Na ni nyuko mwenye tabia ya kumkimbiza binadamu! Kwa africa ni nyoka hatari zaid

Sent using Jamii Forums mobile app
Duuuh...Asante mkuu, but ni kweli kuwa akikuona anakufata akufanyizie au ni ile umeingia anga zake?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Shirima, navutiwa sana na mambo ya wanyama. Nijuze mambo yafuatayo;
1) Simba akishakula mlo wake, anakaa siku ngapi tena hadi aje aue mnyama mwingine tena kwa ajili ya mlo?

2) Nimeona mara nyingi kwenye video Simba akiwa amejeruhiwa, sasa anapokua ana majeraha yanayomfanya asiweze hata kutembea vizuri, anawezaje kuwinda kupata mlo wake?

3)Simba anapendelea kuua mnyama gani hasa kwa ajili ya mlo?

4) Je, inawezekana simba akikosa kitoweo kumla simba mwenzie au chui, duma, fisi, mbwa mwitu au paka pori?

4) ni kweli kwamba Tiger anapenda zaidi kula mamba kuliko prey wengine?

Hi hayo tu kwasasa.
 
1:Ni kweli kuwa Simba jike yupo aggressive Sana kwa binadamu kuliko Simba dume? Kama ni kweli kwanini?

2: Viboko wanaozurura mitaani kwenye makazi ya watu peke yao kama Yule aliyeonekana mwaka Jana Morogoro huwa wanakuwa wametengwa na jamii zao na kufukuzwa kutoka jamii hiyo ndiyo maana wanajitembelea Tu bila kujua waendako?

3: ukikutana na kundi la nyati usiwe na wasiwasi maana uwezekano wa wao kukujeruhi ni mdogo lakini ukimkuta nyati peke yake jitahidi kukimbia na kukaa naye mbali Sana maana si kawaida yao hivyo huenda kajeruhiwa au mzazi na kipindi hicho huwa anakuwa mkali Sana kwa kila kinachoingia anga zake. Hii ni kweli?

4: Tembo hapatani kabisa na rangi nyeupe/ nyekundu. Akiiona lazima ashambulie.

Mkuu hebu nipe shule juu ya haya tunayosimuliana vijiweni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama nina shamba na ninataka kulibadilisha matumizi na kuweka uzio halafu nikafuga swala,nsha na digidigi kwa ajili ya nyama je inawezekana?
Kuna uwezekano wa kupata kibali kuanzia kwa Lukuvi mpaka kwa HK?

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Mkuu Shirima, navutiwa sana na mambo ya wanyama. Nijuze mambo yafuatayo;
1) Simba akishakula mlo wake, anakaa siku ngapi tena hadi aje aue mnyama mwingine tena kwa ajili ya mlo?

2) Nimeona mara nyingi kwenye video Simba akiwa amejeruhiwa, sasa anapokua ana majeraha yanayomfanya asiweze hata kutembea vizuri, anawezaje kuwinda kupata mlo wake?

3)Simba anapendelea kuua mnyama gani hasa kwa ajili ya mlo?

4) Je, inawezekana simba akikosa kitoweo kumla simba mwenzie au chui, duma, fisi, mbwa mwitu au paka pori?

4) ni kweli kwamba Tiger anapenda zaidi kula mamba kuliko prey wengine?

Hi hayo tu kwasasa.
Naam asante kwa maswali mazuri

1. Simba akila akishiba kabisa ana uwezo wa kukaa siku 5 hadi 7 bila kula! Simba mkubwa kabisa anaweza kula kilo 14 za nyama

2.kuhusu kujeruiwa kama nlivyosema mwanzo, simba huishi kwa makundi, hivyo ikitokea mmoja amejeruiwa sio lazima awinde yeye! Wata winda wengine kisha watamletea chakula

3. Chakula anachopendelea simba ni ZEBRA kwakuwa nyama yake ni tamu na pia inatosheleza, lakini sababu nyingine zebra hana uwezo mkubwa wa kukimbia! Hivyo ni rahisi kumuwinda! Wanyama wengine ni nyati na nyumbu pia hawa hupendwa

4.Kuhusu kula simba mwenzake huwa haitokei! ila sana sana kula watoto wake! Pia ana uwezo wa kumla chui

5. Kuhusu tiger huyu hapatikani Africa! Na sio yeye anaependa kumla mamba! Mnyama anaye muwinda na kumla mamba ni JAGUAR, pia nimewai kushuhudia simba akipambana na mamba katika mto gurumeti serenget. Lakini kutokana na ukubwa na nguvu za mamba, simba yule alikata tamaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1:Ni kweli kuwa Simba jike yupo aggressive Sana kwa binadamu kuliko Simba dume? Kama ni kweli kwanini?

2: Viboko wanaozurura mitaani kwenye makazi ya watu peke yao kama Yule aliyeonekana mwaka Jana Morogoro huwa wanakuwa wametengwa na jamii zao na kufukuzwa kutoka jamii hiyo ndiyo maana wanajitembelea Tu bila kujua waendako?

3: ukikutana na kundi la nyati usiwe na wasiwasi maana uwezekano wa wao kukujeruhi ni mdogo lakini ukimkuta nyati peke yake jitahidi kukimbia na kukaa naye mbali Sana maana si kawaida yao hivyo huenda kajeruhiwa au mzazi na kipindi hicho huwa anakuwa mkali Sana kwa kila kinachoingia anga zake. Hii ni kweli?

4: Tembo hapatani kabisa na rangi nyeupe/ nyekundu. Akiiona lazima ashambulie.

Mkuu hebu nipe shule juu ya haya tunayosimuliana vijiweni.

Sent using Jamii Forums mobile app
NAAM!

1. Simba wote ni aggresive! ila simba jike mwenye mtoto ndo anakuwa aggresive sana! Nadhani umepata concept !

2.Kuhusu viboko kupotea na kwenda kwenye makazi ya watu! Hapo kuna sababu zaidi ya moja
@viboko huwa wanajitafutia chakula usiku, wakati wanaondoka kwenda kutafuta chakula, njian wakiwa wanatembea wanakojoa au kutapanya vinyesi vyao ili kujua njia wakati wanarudi! Vinyesi vyao vina individual smell, hivo wakati wanarudi wanafuata iyo smell! Kumbuka wanaeza kutembea ad kilometa 40 kutafuta chakula. Sasa kuna kuwa na changamoto pale mvua itakapo nyesha! Mvua ikinyesha lazima wapoteze direction, maana mvua itabeba mkojo au kinyesi ipeleke sehemu nyingine! Hapa kupotea ni rahis

Kiboko dume akizeeka huwa anatengwa na familia! Hii inamfanya hawe na hasira na kutafuta sehemu yake mwenyewe

NGOZI ya kiboko ni laini hivyo ikipigwa na jua hupasuka pasuka! Wanaepuka jambo hilo kwa kukaa ndani ya maji! Ikitokea bwawa au mto umepengua sana maji! Lazima wakatafute sehemu sahihi ya kujistiri, hivyo muda mwingine hupotea na kuingia kwenye makaz ya binadam

HIZI NDIO SABABU ZA VIBOKO KUINGIA KWENYE MAKAZI YA WATU

3. Ni kweli! nyati akiwa peke yake anakua hatari zaidi! Kwasababu ya kuhofia usalama waje

4. Kuhusu rangi! Rangi nyekundu sio nzuri sana kwa tembo! na wanyama wengne pia! Ila kuhusu kukuvamia hiyo sio sababu kuu ndugu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom