Maalumu Kwa Wana CCM tu! Upinzani Hakuna Kusoma!

payuka

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
829
127
Ndugu zangu!

Wote tumeshuhudia jinsi Dr. Wilbroad Slaa alivyomtoa MKuu wetu Kamasi! Ushindi tumepata wa kishindo, lakini si kishindo kikubwa kama kile cha awamu iliyopita. Tujipe moyo tu kwani ushindi ni ushindi hata uwe wa mezani.

Tuyaache hayo kwani yameshapita na hayatunyimi uzingizi. Lakini ndugu zanguni tukitafakari sana, tena kwa kina mbona mambo yanazidi kuwa magumu? tutafika kweli? ( tafadhalini msinione kwamba nakata tamaa...). Mara katiba mupya, mara Dowans, Mara Weakleaks! Mmmh yaani inatia shaka sana....lakini si mnajua ule msemo wa " mtaka cha uvunguni sharti ainame?" Basi wembe ni ule ule ...ukipata upenyo Chukua Chako Mapema kabla mambo hayajakuwa mabaya. Eeeh nasema chukua chako mapema kwa sababu watanzania ni mbumbumbu ....bado wamelala!

Hakikisheni mnawapa command mbwa wenu wawasaidieni kutuliza ghasia pale upepo unapokuwa mbaya, Nimefurahi sana mlivyofanya kule kaskazini! Mngewaacha kabisa wale mbwa wamuue yule mmasai! eeeh nasema hivo kwa sababu ukiona mchezo umekuelemea ndani ya dakika tisini tumia hata mikono yako kufunga goli...ebo kwani lazima ufunge kwa mguu?? nani kakwambia??...sisi ni miafrica na hizo sheria ni za kwao wazungu hazituusu sisi!

Mwisho kabisa ndungu zangu! sisi ni wateule wachache tuliojaaliwa, ni bahati ya kipekee tuliyoipata..hivyo hatuna budi kuilinda kwa nguvu zote. Mkijifanya kusikiliza kelele za hao wakesha hoi jueni mtafunga mirija yenu yote! Hivi nini kinawashinda? haya nawapeni mbinu rahisi kuwalindieni kitumbua chenu....fungeni midomo yenu af wekeni pamba kwenye masikio kama alivyofanya yule bwana mnene mnene wa " Mambooooo kiitikio: Poaaaaaa) yeye si walisema eti anamiliki misitu ya mkaa kule kiwira mbeya...lakini amekaa kimya hadi wameacha kumfuata fuata. Msiwe kama yule domo kaya anayependwa na wakesha hoi, ndio maana mkulu ameamua kumpeleka huko mbali akashugulikie lile lijumuia lililomshinda hata baba wa taifa!

Mwaka 2011 ni kasi na nguvu ya ajabu kuchukua vyetu!

Kidumu kidumu kidumu chama chetu!
 
Your days are countable

Your days are numbered! Ngoja ipatikane katiba MPYA uone tunavyoibuka.....sasa hivi si unaona wengi (Ikiwamo na wewe) tunatumia majina bandia na kujificha nyuma ya pc tuki-type!
 
Inaonekana inakuuma sana waliopo katika mtandao wanavyokula maisha kwa kuchukua vyao mapema,ila unashindwa kujitenga nao usije nawe kukosa vijihela vya kutumia katika kusogeza siku na umeamua kujifanya u mmojawao wakati ukweli halisi hauko hivyo.
Kuwa wazi na msimamo wako ili watu wakuelewe na wala huna haja ya kujificha miongoni mwao na jioneshe kuwa wewe ni MPINZANI HALISI!
 
Siku ya Kufa nyani miti yote huteleza. Kufa kwa mdomo meno hutawanyika. kufa kwa mk...u ma..i hutawanyika. sasa subirini mkione nyau nyie.
 
Siku ya Kufa nyani miti yote huteleza. Kufa kwa mdomo meno hutawanyika. kufa kwa mk...u ma..i hutawanyika. sasa subirini mkione nyau nyie.
Angalia thread zangu zilizopita ___________________unaifahamu vizuri historia ya raila Odinga? na Mzee wake je? Odinga Odinga --------fuatilia historia yake vizuri utagundua ni mtu wa namna gani!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom