Elections 2010 Maalum: Kwa wale bado ni vipofu, wasioona mbele wala nyuma, walioamua kuichagua CCM

MwanaHaki

R I P
Oct 17, 2006
2,401
705
CCM inakiuka miongozo ya katiba yake, ikiwa ni pamoja na mwongozo wa Azimio la Arusha na Siasa ya TANU juu ya Ujamaa na Kujitegemea, kama ifuatavyo:

MISAADA NA MIKOPO
VITAHATARISHA UHURU WETU
Pili, japo kama tungeweza kuzipata; hivyo ndivyo tunavyotaka kweli? Kujitawala ni kujitegemea. Kujitawala kwa kweli hakuwezekani ikiwa Taifa moja linategemea misaada na mikopo ya Taifa jingine kwa maendeleo yake. Hata kama pangetokea Taifa au mataifa ambayo yako tayari kutupa fedha zote tunazohitaji kuendesha mipango yetu ya maendeleo isingekuwa sawa kwa nchi yetu kuipokea misaada hiyo bila kujiuliza matokeo yake yatakuwa nini kwa Uhuru wetu na uzima wetu.

Msaada ambao ni kama chombo cha kuongeza juhudi, au nyenzo ya juhudi, ni msaada ambao una manufaa. Lakini msaada unaoweza ukawa sumu ya juhudi si msaada wa kupokea bila kujiuliza maswali.

Kadhalika mikopo. Kweli mkopo ni bora kuliko misaada ya “bure”. Mkopo nia yake ni kuongeza jitihada au kuifanya jitihada itoe matunda mengi zaidi. Sharti moja la mkopo huwa ni kuonyesha jinsi utavyoweza kuulipa. Maana yake ni kwamba sharti uonyeshe
kuwa unakusudia kuufanyia kazi itakayoleta manufaa ya kukuwezesha kuulipa.
Lakini hata mikopo ina kikomo. Sharti upime uwezo wa kulipa.

Tunapokopa fedha kutoka nje mlipaji ni Mtanzania. Na kama tulivyokwisha sema Watanzania ni watu maskini. Kuwabebesha watu maskini mikopo ambayo inawazidi kimo si kuwasaidia bali ni kuwaumiza. Na hasa inapokuwa, mikopo hiyo ambayo wanatakiwa walipe haikuwafaidia wao, bali ilifaidia watu wachache tu.

Imetoka: http:www.ccmtz.org/nyaraka/azimiolaarusha.pdf

Bado mtaipa CCM kura zenu, wakati asilimia takriban 40 ya Bajeti ya Serikali Kuu ni mikopo na misaada kutoka nje ya nchi, mikopo ambayo inabebeshwa Watanzania ambao HAWANUFAIKI NAYO, jambo ambalo LINAWAUMIZA?

-> Mwana wa Haki!
 
Back
Top Bottom