Maalum kwa ajili ya wanyama pori

Habari gani members wa JF? Kama una swali lolote kuhusu Hifadhi zetu za taifa, pia maswali kuhusu wanyama pori wa hapa EAST AFRICA(mammals,reptiles,birds,etc) na baadhi ya maswala yanayohusu utalii. Unaweza ukauliza hapa!

Kwa wale ambao hawana idea ngoja niwadokeze kidogo!

Kwa Tanzania kuna Hifadhi za taifa takribani 16 mpaka sasa! Hifadhi kubwa kuliko zote ni RUAHA NATIONAL PARK ikifuatiwa na SERENGETI NATIONAL PARK yenye ukubwa wa 14763km square
Kuna baadhi ya mkanganyiko na baadhi ya watu wakihusisha NGORONGORO kama hifadhi ya taifa, kwa ufupi NGORONGORO ni mbuga inayo simamiwa na mamlaka ya ngorongoro yaani NGORONGORO CONSERVATION AREA AUTHORITY. Hii ni mbuga ambayo binadamu na wanyama huishi kwa pamoja chini ya sheria zilizowekwa.

Katika hifadhi izi kuna wanyama mbalimbali wakiwemo THE BIG FIVE ambao wote kwa pamoja wanapatikana SERENGETI,MKOMAZI,NGORONGORO na pori la akiba la SELOUS. Katika hifadhi nyingine mnyama ambaye hayupo sana ni FARU kwaiyo unaweza ukawapata THE BIG FOUR. Wanyama wengine wanaopatikana kwa uraisi ni logo ya Taifa letu (TWIGA), swala pala, punda milia, nyumbu, pofu, tohe, ngedere, tumbili, honey badger, buffalo, ngiri,bush baby, bweha,caracal,fisi mbwa mwitu, nguruwe pori, water buck, heartbeast, chimpanzee, duma,mamba, kiboko na wengine wengi siwez kuwataja wote

Lakini kuna ndege pia kama vile EAGLES, STORKS, STARLINGS, WEAVERS, VULTURES, BEE EATERS , KING FISHERS, HORN BILLS, OWLS, ROLLERS, na wengine wengi zaid ya species 900
pamoja na wadudu

KARIBUNI WADAU!

Sent using Jamii Forums mobile app
Nini tofauti ya MBUGA na HIFADHI?
Kwa uelewa wangu..mbugani unaruhiswa kuwinda while kwenye hifadhi hurusiwi..

Naomba ufafanuzi zaidi/
 
Nini tofauti ya MBUGA na HIFADHI?
Kwa uelewa wangu..mbugani unaruhiswa kuwinda while kwenye hifadhi hurusiwi..

Naomba ufafanuzi zaidi/
Mbuga ni neno lilikuwa linatumika zamani... Walikuwa wakiita Mbuga za wanyama...

ila kwasasa kuna hifadhi za Taifa na mapori ya akiba, na Hifadhi ya mamlaka ya ngorongoro na mapori tengefu
 
Nini tofauti ya MBUGA na HIFADHI?
Kwa uelewa wangu..mbugani unaruhiswa kuwinda while kwenye hifadhi hurusiwi..

Naomba ufafanuzi zaidi/
Ukisema mbuga ya wanyama unakosea kwasababu kule sio wanyama tu wanalindwa, kuna Mimea,ardhi na vyanzo vya maji
 
Kwanza unatakiwa u control hisia zako! Usipige kelele kama hajakuvamia! Ukiona anakuangalia nawewe mwangalie machoni! Jongea kinyume nyume uku ukimwangalia machoni! Na kumsoma anataka kufanyaje, ukikaa dk 10 hajakufanya chochote endelea tu kusogea taratibu mpk ukifikikisha umbali kama metre 70 ivi nd uanze kukimbia!

Kama ana kuvamia tumia uwanaume waku ata kama ana kuparua! Usikubali kumpa shingo! Alafu hakikisha ukipata chance mtoboe macho kwa kutumia vidole vyako! Au kama una mchanga mrushie machoni

Sent using Jamii Forums mobile app
Labda ki movie movie chief simba hapana aisee hii shughuli dah
 
Naam
Caracal ni moja kati ya paka wadogo wanaopatikana katika felidae family yaani familia ya paka. Jina la kisayansi anaitwa "felis caracal"
Ni paka mzito kati ya paka wadogo! Nikisema paka wadogo namaanisha (wild cat, serval cat, domestic cat na caracal)

Hubeba mimba kwa siku 60 adi 70
Ana masikio marefu! Yenye nywele ndefu juu
Ana rangi ya tawny
Uzito wake unaweza kufikia kilo 10 kwa majike na 20 kwa madume
Huwa wanapenda kuwinda ndege! Kwasababu wana uwezo wa kuruka kwenda juu metre 3 ad 4
Mlo wake kwa siku ni 1kg up to 2

Wanapatikana serengetiView attachment 1026563

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni rafiki kwa binadamu hawa paka?
 
Huyu ataniua mchana kweupe hahahaa..yaani hata kope duh...inaonekana hapendi mazoea ya ovyo ovyo huyu nyoka

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
Wanasema huwa anavuta bangi huyu nyoka maana sifa yake nyingine kubwa anapenda harufu ya bangi kupita maelezo, unaweza kaa unajivutia zako unashangaa huyu hapa pembeni anakugongea
 
Mmmmmh... Hivi koboko ukutane nae utulie tu ...binafsi siwezi ni mwendo wa mbio na kelele kama zote



Sent using Jamii Forums mobile app
Huwezi kumkimbia, ana mbio sana sana yaani inshort koboko ukikutana nae kikubwa ni kusali tu usamehewe madhambi yako, au akuache aende zake vinginevyo ni kifo, kuna uzi upo humu wa koboko visa vipo vingi sana utacheka, utasikitika n.k wengine hadi wamepoteza ndugu zao, hafai kabisa ana kisirani cha hovyo sana
 
Hutoweza kumgonga hata kwa dawa...atakachokifanya the way atakavyonasa kwenye boneti hutaona, hutajua, utahisi umemgongelea mbali (yule ni mzee wa kukwepa hatari na ni mshapu balaa) so ni mwendo wa kukusubiria ufike mwisho wa safari yako ukishuka tu unapewa KUBWA!

Refer my previous comment ya yule mzungu wa SA kilichompata! Ni same case na story yako hii



Sent using Jamii Forums mobile app
Unaweza ukaleta madhara makubwa sana bila kujijua, mfano umekutana nae umeongeza speed umkanyage karuka kakaa kwenye boneti umeenda zako umefika mfano stand, bar, nyumbani au popope penye mkunyasiko wa watu, hebu fikiria itakuwaje.. kama aangusha zizi la ng'ombe zima watu inakuwaje?
 
Huyo nae ni mbaya kinoma, japo mpole sana halafu mvivu...

Akikupa bite...the way utakavyooza, papai bovu lina nafuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mvivu balaa, aliwahi ingia ghetto kwangu wakati nasoma chuo, chini ya meza kajilaza nimenyoosha na miguu kabisa jirani yake katulia tu, japo ana milio yake kukushtua usimguse ndicho kilichonishtua ni nini hiki kumbe yeye, nikamuua
 
Eeeeh!!!!

Nilivyomuona tu nikasaka fimbo nikapiga ikadunda uzuri halina mbio nikalitafutia panga huku napiga makelele wadau wanafika wanakuta natiririkwa jasho acha wanicheke eti nyoka mwenyewe kifutu ungemuacha tu......

mwenzio happ nilijua napambana na mtoto wa chatu

Sent using Jamii Forums mobile app
Yes hana shida kifutu japo sumu yake si mchezo, mpole sana ila usimguse
 
Back
Top Bottom