Maalum kwa ajili ya wanyama pori

WAKUNJOMBE

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2010
Messages
441
Points
500

WAKUNJOMBE

JF-Expert Member
Joined Dec 27, 2010
441 500
Habari gani members wa JF? Kama una swali lolote kuhusu Hifadhi zetu za taifa, pia maswali kuhusu wanyama pori wa hapa EAST AFRICA(mammals,reptiles,birds,etc) na baadhi ya maswala yanayohusu utalii. Unaweza ukauliza hapa!

Kwa wale ambao hawana idea ngoja niwadokeze kidogo!

Kwa Tanzania kuna Hifadhi za taifa takribani 16 mpaka sasa! Hifadhi kubwa kuliko zote ni RUAHA NATIONAL PARK ikifuatiwa na SERENGETI NATIONAL PARK yenye ukubwa wa 14763km square
Kuna baadhi ya mkanganyiko na baadhi ya watu wakihusisha NGORONGORO kama hifadhi ya taifa, kwa ufupi NGORONGORO ni mbuga inayo simamiwa na mamlaka ya ngorongoro yaani NGORONGORO CONSERVATION AREA AUTHORITY. Hii ni mbuga ambayo binadamu na wanyama huishi kwa pamoja chini ya sheria zilizowekwa.

Katika hifadhi izi kuna wanyama mbalimbali wakiwemo THE BIG FIVE ambao wote kwa pamoja wanapatikana SERENGETI,MKOMAZI,NGORONGORO na pori la akiba la SELOUS. Katika hifadhi nyingine mnyama ambaye hayupo sana ni FARU kwaiyo unaweza ukawapata THE BIG FOUR. Wanyama wengine wanaopatikana kwa uraisi ni logo ya Taifa letu (TWIGA), swala pala, punda milia, nyumbu, pofu, tohe, ngedere, tumbili, honey badger, buffalo, ngiri,bush baby, bweha,caracal,fisi mbwa mwitu, nguruwe pori, water buck, heartbeast, chimpanzee, duma,mamba, kiboko na wengine wengi siwez kuwataja wote

Lakini kuna ndege pia kama vile EAGLES, STORKS, STARLINGS, WEAVERS, VULTURES, BEE EATERS , KING FISHERS, HORN BILLS, OWLS, ROLLERS, na wengine wengi zaid ya species 900
pamoja na wadudu

KARIBUNI WADAU!

Sent using Jamii Forums mobile app
Nini tofauti ya MBUGA na HIFADHI?
Kwa uelewa wangu..mbugani unaruhiswa kuwinda while kwenye hifadhi hurusiwi..

Naomba ufafanuzi zaidi/
 

PANTHERA LEO

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2019
Messages
2,172
Points
2,000

PANTHERA LEO

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2019
2,172 2,000
Nini tofauti ya MBUGA na HIFADHI?
Kwa uelewa wangu..mbugani unaruhiswa kuwinda while kwenye hifadhi hurusiwi..

Naomba ufafanuzi zaidi/
Mbuga ni neno lilikuwa linatumika zamani... Walikuwa wakiita Mbuga za wanyama...

ila kwasasa kuna hifadhi za Taifa na mapori ya akiba, na Hifadhi ya mamlaka ya ngorongoro na mapori tengefu
 

Forum statistics

Threads 1,343,409
Members 515,033
Posts 32,783,815
Top