Maalimu Seif asikitishwa na udanganyifu katika mitihani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maalimu Seif asikitishwa na udanganyifu katika mitihani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Mar 11, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad


  Tanzania ipo katika hatari ya kuwa na kundi la wataalam wasiokuwa na sifa iwapo tatizo la udanganyifu wa mitihani kwa wanafunzi halitodhibitiwa na wizara yenye dhamana nchini.
  Tamko hilo limetolewa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad, katika mahafali ya 11 kidato cha nne ya Shule ya Sekondari ya Sunni Madrassa mjini hapa jana.
  Alisema vitendo vya wanafunzi kutafuta kufaulu kwa njia za mkato athari zake ni kubwa kwa maendeleo ya vijana na Taifa.
  “Tutakuwa hatuna wataalam walioendeleza vipaji vyao na badala yake tutakuwa na wataalam feki Zanzibar,” alisema Maalim Seif.
  Aliwataka wazazi na wanafunzi Zanzibar kujiepusha na tabia ya kusaidia watoto wao kufaulu kwa njia haramu za kusadia kununua mitihani ili lengo la serikali la kuimarisha kiwango cha ubora wa elimu kifanikiwe nchini.
  Alitoa kauli hiyo kufuatia wanafunzi 3,303 wa kidato cha nne kufutiwa matokeo ya mtihani baada ya kuthibitika walifanya udaganyifu wa kusaidiwa majibu na wasimamizi wakiwemo 1,200 kutoka Zanzibar.
  Alisema wakati umefika kwa Wizara ya Elimu Zanzibar na Tanzania Bara kuunda tume ya kuchunguza chanzo cha tatizo na kuondoa udhaifu uliopo katika usimamizi wa mitihani kwa vyombo husika nchini.
  Alisema adhabu ya kuwafungia kwa muda wa miaka mitatu kufanya mtihani ni adhabu kubwa na Baraza la mitihani la taifa Tanzania (NECTA) linapaswa kuangalia upya sheria hiyo.
  Alisema malengo ya serikali ya kuimarisha kiwango bora cha elimu Tanzania yatafikiwa iwapo kila uongozi wa shule utajiwekea malengo na mikakati.
  Hata hivyo, akizungumza na Kamati ya Maendeleo ya Wanawake na Ustawii wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Machi 5, mwaka huu, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dk Joyce Ndalinacho, alisema baraza hilo limeamua kuunda kamati ya kuchunguza kashfa hiyo.
  Alisema kamati hiyo itaundwa na wajumbe kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ili walimu na maofisa elimu wa mikoa watakaoguswa na uchunguzi huo wachukuliwe hatua za kinidhamu na kisheria.
  Hata hivyo alisema NECTA haina uwezo wa kutoa adhabu kwa walimu waliohusika kusadia majibu ya mitihani wanafunzi kwa vile siyo waajiriwa wa Baraza hilo.
  Dk Ndalinacho, alisema kamati yake itawahoji wanafunzi waliyofutiwa mitihani, maafisa elimu wa mikoa, wasimamizi wa mitihani, Polisi na Usalama wa Taifa ambao walikuwa na dhamana ya mitihani hiyo.
  Dk Ndalinacho alisema vitendo vya udaganyifu wa mitihani lazima vithibitiwe ili kulinda kiwango cha ubora wa elimu ya Tanzania kwa maendeleo ya Taifa na wananchi wake.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

   
Loading...