Maalim Sif sasa ababaika, ati "walikubaliana" kuivunja ZEC!

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
18,173
13,776
Katika hali inayoashiria kuwa Maalim Seif sasa kachanganyikiwa, sasa ameenda kudai kuwa ati Dr Shein "amemgeuka".
Ati katika mazungumzo yao "walikubaliana" kuivunja ZEC, Tume ya Uchaguzi Zanzibar iliyo chini ya mzee Jecha.
(MWANANCHI pg2 leo Februari 7, 2016)

Kwa wafuatiliaji wa sakata la uchaguzi na figisu zilizojiri watakumbuka kuwa Maalim Seif alijitoa kwenye mazungumzo hayo baada ya kushauriwa na UKAWA!
Sasa kwa akili ndogo tu mtu atajiuliza hayo makubaliano na Dr Shein yalifikiwa lini na wapi, ilhali Maalim alibwaga manyanga katika mazungumzo hayo.
Ni muhimu CUF ikahakikisha kwamba kila hatua achukuayo kiongozi wao anakuwa katika stable mind, sasa hivi ni kama amechanganyikiwa!
Fuatilia habari hii ya Jan 20, 2016.
Kutoka magazetini.

Seif Shariff Hamad amejitoa rasmi kwenye mazungumzo yaliyokuwa yanaendelea.

Ni baada ya viongozi wakuu wa vyama vinavyounda UKAWA kukutana jijini kwa siri kubwa na baada ya Seif kufanya mazungumzo na aliyekuwa mgombea urais wa Chadema kwa mwamvuli wa Ukawa mh. Edward Lowassa.
 
Maalim seif ni mnafiki kwani kwa kauli yake hiyo ni dhahiri alikubali kurudiwa uchaguzi kama hayo matakwa yake yangekubaliwa,lakini siku zote yeye na viongozi wenzake wa cuf walikuwa wanadai hawatokubali uchaguzi kurudiwa
Njia ya mwongo ni fupi, ukweli utajulikana.
 
Maalim seif ni mnafiki kwani kwa kauli yake hiyo ni dhahiri alikubali kurudiwa uchaguzi kama hayo matakwa yake yangekubaliwa,lakini siku zote yeye na viongozi wenzake wa cuf walikuwa wanadai hawatokubali uchaguzi kurudiwa
Mkuu za mwizi arobaini, na waswahili wanasema panapofuka moshi pana moto!
 
Katika hali inayoashiria kuwa Maalim Seif sasa kachanganyikiwa, sasa ameenda kudai kuwa ati Dr Shein "amemgeuka".
Ati katika mazungumzo yao "walikubaliana" kuivunja ZEC, Tume ya Uchaguzi Zanzibar iliyo chini ya mzee Jecha.
(MWANANCHI pg2 leo Februari 7, 2016)

....
Mimi ningeshangaa sana kama Dr. Shein angeweka na kutimiza ahadi yake. CCM hawana utamaduni wa kutimiza makubaliano. Waulize wananchi wa Tanzania kuhusu ahadi hewa za CCM.

Seif akifanya mazungumzo na CCM tena aingie na timu kama CCM wanavyoingiza timu ya wabakaji.
CCM wanabaka demokrasia, mbakwaji anaingia peke yake kukabiliana na wabakaji. Hilo la kuivunja ZEC litajulikana ni muda tu. Katika hao CCM walioingia kwenye vikao atasema kama hilo lilizungumzwa.
Moyo alipojitambua alitoa habari za magumashi waliyofanya CCM 2010.
Dr. Shein amebadilika?
 
Sasa ikawa vipi tena Seif kubwaga manyanga?
 
Seif amesema au hukumsikia au kusoma sehemu?
Aligundua kuwa Shein si mkweli. Shein na Balozi Seif Iddi baada ya vikao walikuwa wanawatumia vijana wa ccm kutoa matamko ya kuharibu mazungumzo. Seif pia amenukuliwa akisema kuwa aliomba vielelezo kutoka kwa ccm kufuatia malalamiko yao kwa tume kuwa kulikuwa na dosari. CCM , Shein na Seif Iddi walishindwa kutoa vielelezo. Hiyo unayoiita kubwaga manyanga ni baada ya Seif kujiridhisha kuwa uungwana wake wa 2010 ulionekana kama ubwege(udhaifu).
 
Maalim Seif kubabaika ?? Naona umeamua tu kumlisha maneno ,sio Mpemba yule aisee
Yaani wewe umeshindwa kuelewa kwamba kulikua na vikao tisa ,yote yaliyoongelewa huko unayajua ?? Seif anayatoa sasa hivi unasema kababaika
Ila kaza mzee Jaramba la Jakaya kwa Magufuli ili awakumbuke sio mchezo huwenda ukakumbukwa
 
Ndugu zangu,
Kuweza kuchangia siasa za Zanzibar inataka kwanza uijue historia ya Zanzibar
vyema.

Maalim Seif si kiongozi wa kuchanganyikiwa.
Maalim Seif ni kiongozi makini sana.

Katika uchaguzi wa 2010 Dr. Sheni alishindwa.
Ujumbe maalum ukiongozwa na Mzee Hassan Nassoro Moyo ulitumwa kwake.

Huu ujumbe ulikuwa na salaam maalum na kama si busara za Maalim Seif damu
ingemwagika tena nyingi kushinda ya 2001 kuanzia pale pale Bwawani.

Alipozungumza na Wazanzibari pale Bwawani yalipokuwa yanatangazwa matokeo
ya uchaguzi, Maalim Seif alisema: ''Walioshinda ni Wazanzibari.''

Akamalizia kwa kusema kuwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar haifai.
Muhimu katika hili ni kuwa Dr. Shein kashindwa uchaguzi.

Kura chache alizopata Dr. Magufuli Zanzibar zinaakisi kura alizopata Dr. Shein.
Sasa hebu tuaagalie nani aliyechanganyikiwa.

Je, ni yule aliyeshinda uchaguzi na matokeo kuwekwa mwenye mbao na shahda
kutolewa au yule aliyesimamisha uchaguzi na kuingiza vyombo vya dola kuzingira
Tume ya Uchaguzi na kumkamata Makamu Mwenyekiti wa Tume na kumpeleka polisi?
 
Mkuu japo mimi ni kijana wa juzi juzi sina ninalo lijua kuhusu historia ya Zanzibar zaidi ya hii tunayo isoma ambayo pia hujui uamini nini maana mambo mengi yamefichwa ama kwa makusudi au kwa kupotosha ,na pengine tungekua tunaijua vizuri historia ya Zanzibar ikiwa ni pamoja na huu Muungano labda leo tusingefikia hapa tulipo ,Kwa mda mchache niliomfahamu Maalim Seif sijawahi kuona akibabaika ama kwa kutokujua anachosimamia au kwa uchu wa madaraka ,siku zote ni mtu jasiri ,ajuaye anachokifanya na zaidi sana anajali utu na ndio maana nimemshangaa mleta mada
Zanzibar itapita kipindi kirefu kuja kumpata mwanasiasa aina ya Maalim Seif endapo ataamua kuachana na siasa hizi
 
UncleBen,
Ingia hapa: mohammedsaid.com search, Zanzibar, Karume, Mapinduzi etc. etc.
Utakuta mengi katika historia ya Zanzibar.
 
Nashukuru Mzee wangu na wala sio mara yangu ya kwanza kukusoma katika mabandiko yako hapa yahusiyo historia
Kwa kukumbusha tu kuna sehemu kwenye maandiko yako ulisema mama Maria Nyerere aliwahi kuwa na duka la mafuta ya taa Magomeni ila mwanae Andrew Nyerere akakanusha kwamba mama yake hakuwa na duka wala kuuza mafuta ya taa popote .
Shida ambayo tunapata sisi vijana wa leo ni hatujui ni wapi tusimamie
Nashukuru sana
 
Simama kwenye ukweli.
Penye ukweli uongo hujitenga.

Tuanze na historia ya Ali Msham.

Ali Msham alikuwako na picha zake na tawi la TANU aliloanzisha nyumbani
kwake wanae wamenipa na mimi nikaziweka katika mtandao.

DSCN1793.JPG

Kushoto wa kwanza Ali Msham aliyekaa kwenye meza ni Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Sote tumeziona.

Picha zile zimemuonyesha Ali Msham akiwa na Nyerere, John Rupia, Zuberi
Mtemvu, Sheikh Suleiman Takadiri, Bi. Titi Mohamed
na wazalendo wengine
miaka ya 1954/55.

Mtoto wa Ali Msham, Abdulrahman Ali Msham ndiye alionieleza mimi historia ya
baba yake wakati wa kupigani uhuru wa Tanganyika.

Kuhusu duka la mafuta ya taa wanasema baba yao alimuanzishia Mama Nyerere
mradi wa kuuza mafuta ya taa na kabla ya kufungua duka wakiuza katika kwama.

Baadae biashara ilipokua ndipo Ali Msham akamfungulia Mama Maria duka pale
nyumbani kwake.

Abdulrahman alinieleza kuwa Mama Maria katika kazi alizokuwa akifanya pale
dukani alikuwa akifuma sweta na alikuwa na kijana wake Joseph Kiboko Nyerere.

Kijana aliyekuwa akimsindikiza Mama Maria jioni kurejea kwake alikuwa Abdallah
Omari Likonda
ambae alikuwa mpwa wake Ali Masham.

Huyu Abdallah Omari Likonda yu hai hadi leo.
Ikiwa leo hii historia hawaitaki wala hapana haja ya ubishi.

Mimi nawaachia wasomaji wangu waamue wenyewe nani mkweli na nani muongo.

DSCN1803.JPG

Abdulrahman Ali Mshama akiwa amesimama nje ya nyumba yao ulipokuwa tawi la TANU 1954/55
 
Asante Mzee wangu na pia nitaendelea kusoma vitabu ama bandiko lolote kuhusu historia yetu kutoka katika vyanzo tofauti tofauti
Naam ukweli daima hujitenga na uongo.
 
Back
Top Bottom