MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Umewatuliza wafuasi wako baada ya kuona haki na demokrasia vikikanyagwa kwa wakati moja, wafuasi wako walisubiri kuona kunywa chako kinatamka nini wakutii, wafuasi wako walipandwa na munkari wakisubiri kauli zako za mwisho! Lakini kauli yako kwao ilikua ni "Kuweni watulivu na wavumilivu, Kuweni na amani, tuko kwenye mazungumzo" Wafuasi hawa kwa kuipenda nchi yao bila hiyana wakatii kauli zako ndiko ulipowafikisha mpaka hivi sasa.
Maalim Seif hata watoto wadogo wanaijua haki yako tukiacha jumuiya na taasisi mbali mbali za kimataifa, Mpaka Leo kuna watu wanasema unachomwa jicho kwa kidole na hasimu wako umetulia tu! Maalim Seif kwa hakika Mungu atakulipa, Wewe ni mvumilivu wa ajabu, unawathamini sana Wazanzibar kwa ujumla, Wamekuelewa na wanaendelea kukuelewa.Ni dhahiri kabisa hata kwa sasa unawasikiliza Wafuasi wako na wewe! Mungu azidi kukupa busara wewe na wafuasi wako.
Maalim Seif Tumeongea na viongozi wakuu wote wa nchi hii, umeongea na kujadili sana nà mahasimu wako, lakini kwa hotuba yako ya juzi ni dhahiri kabisa kwamba hujasikilizwa, Sio wewe tu hii ni pamoja na wafuasi wako! Maana kila ulichokifanya ni kwa niaba yao.
Hakika wewe ni Mtu mtulivu sana pamoja na kupokwa haki yako kwa makusudi lakini wewe ndiye unayefanya jitihada zote za halali kuhakikisha inapatikana.
Maalim Seif mpaka hapa hakuna anayekulaumu pamoja na utaarabu wako kuonekana kukinaiwa na watu wengine mpaka kufikia kukutana na Lugha za kibaguzi ndani ya ardhi yako.
Usikate tamaa kuisaka haki uliyopokwa wewe na wafuasi wako Mungu yu pamoja nawe kitaeleweka tu.