Maalim Seif you need to know the Question before trying to answer it

Simba zee 33

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
1,378
2,000
Mzee wangu Seif Sharif Hamad Unahitaji kujua swali kwanza kabla ya kujaribu kujibu, maana ukisha jua swali linauliza nini basi utakua umepata nusu ya Jibu.

Vinginevyo kila siku tutakua tunakuoneni mkidhalilika ndani ya nchi yenu

Kumbuka mafundisho ya kiislamu yanayosema '' 'MTU MUUMIN HAWEZI KUUMWA NA NYOKA YULE YULE MARA MBILI (zaidi ya mara moja) kwenye shimo lile lile

Maana ingine mnafiki Ndio hugongwa na yule yule nyoka kwenye shimo lilelile zaidi ya mara moja

Sheikh wangu, Mzee Mwenzangu, ndugu yangu, japokua mimi nipo ndani sana kwenye vijiji vya USANGI lakini yanayowakuta ndugu zetu yanatuumiza sana. Haswa tukijua Wewe au nyie ndio mnakua hamtaki kujua mzizi wa fitina ni kitu gani Akhiy nataka kukwambia mzizi wa fitina ni nyie WAZANZIBARI sio Sisi, Sisi ni matawi tu.

Fina ni hio SMZ ambayo ni kama mbwa asie na meno na uchu wa madaraka walionao hao '' So called SMZ leaders'
Viongozi wa SMZ wamaini endapo CCM ikianguka kule Zanzibar wao Tonge Lao litakua mashakani Ndio maana Kwa Hali na Mali wanajitahidi kuzuia Tonge ambalo lipo kinywani haliwezi kuwatoka. Kama ungelijua hilo mbona wala usinge taabika!!
NASAHA yangu kwako kama wao wanamwaga mboga mbona nyie msimwage ugali?

Maana yangu ni kwamba..
Mwl Nyerere falsafa yake ilikua serikali mbili kuendea serikali moja. Mimi naona wakati umefika Zanzibar iwe mikoa ya JMT.
Kule unguja pawe na mikoa miwili na kule Pemba mikoa miwili. Majimbo ya ubunge sana sana yawe matano kwa ujumla na kusiwe na Baraza la wawakilishi wala spika.

Kama itatikea hivyo najua watakuita msaliti lakini msaliti wa nini?

Baada ya mamia yao kukosa ajira na wakuu wa mikoa yao watakua watu kutoka kwetu kuwatawala Ndio ngoma itanoga maana kama sio maelfu basi mamia tutakua nao mtaani

Taasisi zote za SMZ zutafungiliwa mbali na wasaliti wa wazanzibari tutakua nao mitaani. Kwa kuwa njaa inauma vibaya kuliko kidonda Ndio watalijua jiji. Baada ya hapo Ndio mtakaa kama wazanzibari kutafuta hatma yenu

Huku Bara na sisi tutatafu angalau tupate serikali za majimbo ambayo mimi naamini Ndio itakua chachu ya maendeleo
Labda Bara tukipata serikali tano za Majimbo na serikali moja ya jimbo la Zanzibar serikali sita kila serikali inakua na gavana wake basi mambo yatakua swafi kwa sasa ni fujo tu hakuna maendeleo mpaka tupate ruzuku kutoka serikali kuu
That is me to you Maalim seif.

Serikali moja Ndio suluhisho japo kua ni Kwa muda
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom