Maalim Seif: Uporaji haki za Wazanzibari sasa basi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maalim Seif: Uporaji haki za Wazanzibari sasa basi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mdondoaji, Sep 16, 2009.

 1. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Salim Said na Elias Msuya

  KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) maalim Seif Sharif Hamad, amesema ukandamizaji na uporaji wa haki za wananchi unaoendelea kisiwani Zanzibar sasa basi.

  Maalim Seif alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaamu na kusisitiza kuwa watatumia nguvu ya umma kuhakikisha kwamba, wanaishinda dola kandamizaji iliyo chini ya CCM.

  Hamad alisema hayo akiwa makao makuu ya chama hicho, Buguruni jijini Dar es Salaam wakati akitoa msimamo wa chama chake kuhusiana na vurugu zinazoendelea Pemba katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura kisiwani humo.

  Kutokana na vurugu hizo tayari nyumba sita za mawakala wa CUF zimechomwa moto, huku baadhi yao wakijeruhiwa kutokana na mabomu ya kutoa machozi na kuwamwagia maji yenye kemikali ya kuwasha.

  Hamad alisema chama chake kinawapongeza wananchi hao kwa msimamo thabiti wa kukataa kudhulumiwa haki zao zinazoporwa kupitia chaguzi kuu tangu mwaka 1995.

  “Tunajua wanapatishwa mateso makubwa na watawala madhalimu wasiojali raia wao, lakini hiyo ndiyo gharama ya kudai haki. Hivyo tunawapongeza na kutoa wito kwamba, wasichoke wala kuyumba katika kutetea haki hizo,” alisema Hamad na kuongeza:

  “Umefika mwisho kwa watawala wakandamizaji wa CCM, tunasema ukandamizaji na uporwaji wa haki za wananchi wa Zanzibar sasa basi na tunawahakikishia kwamba nguvu ya umma itashinda dola kandamizaji.

  Hatua tunayoipita sasa pia wamepita wananchi wa nchi nyingine waliokandamizwa na kunyimwa haki zao, lakini hawakukata tamaa na mwishowe walishinda.”

  Aliahidi kwamba, viongozi wa chama hicho kwa kushirikiana na wananchi wapenda haki na demokrasia wa visiwa vya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla wataushinda udhalimu huo tu.

  Maalim alisisitiza kwamba, vurugu zote zinazotokea Zanzibar zinasababishwa na njama ovu za CCM na serikali zake kuwazuia wananchi wengi wenye sifa kutoandikishwa katika daftari la kudumu la wapigakura kwa lengo la kupunguza kura za upinzani katika uchaguzi mkuu.

  “Sambamba na hilo njama hizo zinahusisha kuwanyima haki wapigakura halali 175,000 kisiwani Pemba na kujaza watu wasio na sifa kwa idadi hiyohiyo, ambao ni pamoja na watu maalum wanaotoka sehemu mbalimbali za Tanzania, maarufu kwa jina la Janjaweed kwa ajili ya kuongeza kura za CCM,” alisema na kuongeza:

  “Njama hizi hazitosaidia chochote zaidi ya kuifanya hali kuwa mbaya zaidi na ni vyema serikali za CCM zikajifunza kutokana na matendo kama hayo yaliyofanywa huko nyuma”.

  Hamad alidai zaidi kuwa njama hizo zinatekelezwa kwa pamoja na Idara ya Vitambulisho vya Mzanzibari Mkazi (Zan ID) na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na kuratibiwa na Idara ya Usalama wa Taifa.

  “Katika njama hizo wanawatumia maofisa wa ngazi za juu ambao ni pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Zan ID, Mohammed Juma Ame na watendaji wa sekretarieti ya ZEC wakiongozwa na Mkurugenzi wake Salum Kassim Ali,” alidai Hamad.

  Hata hivyo, Salum Kassim alipoulizwa na gazeti hili alisema hiyo ni haki ya kidemokrasia ya Hamad kusema anachotaka na kuongeza kuwa ingekuwa bora angetoa mifano na kuthibitisha madai yake hayo.

  “Mimi ni mtendaji wa ZEC na nafanya kazi kwa mujibu wa sheria na kanuni zake na hakuna hata siku moja niliyoambiwa labda nimekiuka sheria, taratibu au kanuni za taasisi yangu katika utendaji,” alisema Kassim na kuongeza:

  “Maalim angekuwa ‘specific’(wazi) na kutoa ushahidi katika tuhuma zake mimi ningejibu, lakini kwa sasa siwezi kusema chochote hadi hapo atakapotoa uthibitisho wa madai yake na kwa kifupi nasema madai yake yote ni uongo mtupu”.

  Pia Kassim alikataa kwamba yeye ni afisa wa usalama wa taifa na kuongeza kwamba, hayo ni madai tu ambayo hata yeye anaweza kuibuka na kutoa madai yoyote kwa maalim Seif.

  Hamad alisema CUF inalaani vikali vitisho kwa wananchi na waandishi wa habari, matumizi makubwa ya nguvu kubwa ya kijeshi dhidi ya raia na kitendo cha utawala kuingilia mamlaka na utendaji wa tume ya uchaguzi.

  “Tunawataka wakuu wa mikoa, wilaya, mkurugenzi wa Idara ya Zan ID na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi kuacha kuingilia shughuli za ZEC na ZEC nao wakatae kuingiliwa katika shughuli zao,” alisema.

  Wakati huo huo, Maalim Seif alisema ameshtushwa na kauli za Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)aliyotoa alipokuwa akifafanua kuhusu mabaki ya vitambulisho vya kupigia kura vilivyookotwa na viongozi wa chama hicho baada ya kuchomwa moto katika Bohari Kuu ya Taifa hivi karibuni.

  “Namshangaa sana Kiravu (Rajab). Kwanini atoe kauli za kishabiki kama kiongozi wa chama cha siasa? Kauli kama hizo zinatakiwa kutolewa na viongozi wa vyama vya siasa hasa CCM. Yeye ni kiongozi wa chama gani? Kwa mtindo huo tutaiaminije Tume ya Taifa ya Uchaguzi?" alihoji.

  Niliwahi kusema siku moja tuuogopeni mwanadaamu akichoka kudhulumiwa huwa hajali litamtokea nini yaani huwa anabadilika na kuwa mnyama. Naona viongozi wetu watafute suluhu ya hili jambo ama sivyo Pemba na Zanzibar patatokea maafa.
   
 2. C

  Calipso JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu thanks kwa dataz..
  Mimi namuunga mkono Maalim mia kwa mia,tumechoka kudhulimiwa.. litakalokuwa na liwe lkn ccm watatoka tu inshaallah...
   
 3. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kitimbakwiri huyu- tayari yumo mbioni kubabaisha watu. Sifa za kuandikishwa kupiga kura tumekubaliana kuwa ni Zan ID pamoja na nyengine kama zilivyoorodheshwa kwenye sheria ya Uchaguzi, sasa kwa nini asiye na hizo aandikishwe? Wachocheao fujo Pemba ni wale wanaolazimisha Tume iache kufanya kazi zake kwa mujibu wa sheria na kulazimisha kuandikishwa kwa Wapiga kura mamluki kutoka Dar, Tanga, Mombasa na hata Unguja (daraja bovu, Jang'ombe. Mtoni na kwengineko. Nawasihi ZEC wawe macho waepushe wakaazi wa Pemba kuepelekewa mamluki katika shehia zao na majimbo ya uchaguzi -2010.
   
 4. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2009
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wapemba wasikubali kutumiwa kama ngazi za kuwapandisha chati kina Maalim Seif na kundi la waansiasa wanaotaka kuabudiwa.Maalim Seif alitakiwa atoe kauli akiwa huko Pemba ili kuonyesha namna anavyowajali wapemba cha ajabu anatoa kauli akiwa Dar.Vurugu zikianza anakimbilia UK yeye na wajukuu wake wananchi wa kawaida watachomewa nyumba,wakinamama watabakwa,wanasiasa uchwara watafunguliwa mashtaka hewa na nk.

  CUF haiwezi kushinda uchaguzi mkuu mwaka 2010 kama itaendelea kuwa na viongozi wa aina ya Maalim na Prof Lipumba.CCM imeshashinda kabla uchaguzi haujafanyika kwasababu tayari wanajua nani atagombea atawadanganya nini wananchi.Maalim wakati umefika kwa hawa viongozi wa CUF kugombea nafasi ya urais kwa upande wa Tanzania bara na Tanzania visiwani.

  Propaganda za kuwatisha watawala wakati inafahamika wazi vurugu zikitokea wananchi wa kawaida ndiyo watakaopata shida.Siasa za Maalim zimezalisha wakimbizi kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania,wakimbizi wa kizanzibar wanateseka kwenye makambi ya wakimbizi Maalim Seif anaendelea kupata mafao na stahi zote kama waziri kiongozi mstaafu.
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Kuna watu dunia hii wanaamini bila kushika madaraka makubwa kabisa basi maisha hayajakamilika. Kule Pemba kuna matatizo ila napata mashaka na kama mheshimiwa huyu analojibu la matatizo yaliyopo.
   
 6. K

  Kinyikani Member

  #6
  Sep 18, 2009
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 65
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kuna watu wanataka kubabaisha watu hivi kweli matatizo ya Zanzibar na Tanganyika hayajulikani. Kwa wale Viziwi na wenye chuki zidi ya Wapemba na wanzibari kwa ujumla matatizo ni CCM kungangnia madaraka hawako tayari kuiachia nchi hii wako tayari kwavyoyote.

  Hivi kweli ni nani anaye amini kuwa NEC sio CCM. hili tume la uchaguzi ni mi CCM mitupu.
  Hivi kweli ni nani anaye amini kewa Zec sio CCM. hali kadhalika haya ma Zec yote ni maCCM sasa hapo kunauchaguzi. si ndio kujambia mtoni.
  Mimi ushauri wangu ni bora upinzani wasijitabishe bure waiachie hiyo CCM itese milele vyenginevyo CCM watauwa.
   
 7. C

  Calipso JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  hahaha! na wale walotoka bara. inaonekana wewe ni mmoja kati ya wanaowadhulumu waznz hakki yao. lkn Mungu katuusia ktk mambo amabayo mtu hasamehewi mpaka arudishe hakki ya watu basi dhulma. sasa usishabikie. kwani muuzaji pombe,mpelekaji,mnywaji wote wamo hawa. Mungu akusaidie
   
 8. Ngida1

  Ngida1 JF-Expert Member

  #8
  Sep 18, 2009
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 554
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Dear Nd. Calipso,
  Tafadhali usizivunje mbavu zetu na Ramadhani hii. Nani hao kutoka Bara wanaowadhulumu waznz haki yao? Kama mnaona mnadhulumiwa sio tokeni tu kwenye Muungano?

  Vipi yule waziri wenu wa Nishati? Kafikia wapi tena na mafuta yake? Unafanya masikhara na CCM? Kawekwa sawa Dodoma!!!
  Sote tunakubali kuwa CCM inamashakili yake hasa tukizungumzia ufisadi, lakini when it comes to the Unity of this country it is really NUMARO UNO!!!

  Siku zile za mwanzo nilikuwa ninawasiwasi kuwa Kikwete atawaangusha waznz. Kwavile yeye ni Rais kijana nilidhania haifahamu ZNZ, lakini kumbe anaifahamu kuliko hata huyo mtoto wa Karume. Kwahilo nimemvulia kofia na ashikilie uzi huo huo. Kama na ufisadi nao angelikuwa ameupo umbele huo huo nadhani angelikuwa Rais wapili katika historia yetu baada ya Nyerere.

  Bara has nothing to lose, kwahivyo jamani bora tuheshimiane na kama kuna kitu mnataka tukizungumze basi tukae chini kwa salama na amani na sio mtu anazuka tu na kusema tunawadhulumu waznz haki yao. Au eti mtu kusema kuwa akifika kwenye kikao cha serikali ya Muungano atatupa docs kwenye meza zitiwe sahihi bila ya discussions. Mambo haya mmeyaona wapi? Sasa kafikia wapi na hizo docs zake? Hataki tena kuzitupa kwenye meza ili zitiwe sahihi? Naona badala ya kuzitupa kwenye meza, basi kazitupa kwenye dustbin mwenyewe.
  Eh waznz acheni janja hio. Tushaoana na kwahivyo wacheni sasa tulee wajukuu zetu!!!
   
 9. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #9
  Sep 18, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,399
  Likes Received: 3,726
  Trophy Points: 280
  Naomba list ya vitu wanavyoporwa Wazanzibar
  1.
  2.
  3.
  etc

  Nipe list ya vitu wanavyoporwa Watanganyika
  1. Umeme Wazanzibar mmeanza kulipa lini..???????? Na hizo siku kabla ya kuanza kulipa mlikuwa mnalipiwa na nani..?????

  2. Mmetudai sana Passport ya kuingilia Zanzibar.

  3.
  4.

  Leo hii mmeanza kudai mafuta ambayo hata haijulikani kama yatapatikana. Tukijitoa hamtaishia hapo, shea wa kitongoji chenye mafuta atajitoa kwenye uzanzibar wenu, na ndani ya kitongoji hicho watazichapa mpaka mshindi apatikane na mafuta yatakuwa yake. Na muda huo ukifika, wewe unayedai uzanzibar utakuwa ushakufa kwa vita.

  HIVI MNA UGOMVI NA TANGANYIKA AU CCM...???? HUKO HUKO MLIKO KUNA CCM.
   
 10. M

  Mchapakazi Member

  #10
  Sep 18, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 67
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mi najiuliza swali. Tanzania bara ni kubwa tunapakana na nchi ambazo zimekuwa na fujo na wakimbizi wengi wameingia Tanzania kutokea huko lakini hatuna TAN ID but kuna ZAN ID. Huu ni wizi mtupu huko Zanzibar wanachunga nini? Mbona vitimbi sana kwenye kuandikisha wapiga kura? CCM mmeiba sana na ninaona wizi wenu hamtaacha mpaka mtuingize vitani. Huku kung'ang'ania madaraka kwenu kwanipa wasiwasi sana kwa kweli.
  Nawasikitikia Wazanzibari jinsi walivyoshikwa masikio na mafisadi. Naona imeamuliwa Hussein Mwinyi lazima awe raisi so wapigane kama hawataki.
  KULALEKI tuuze nchi tugawane kila mtu aende kivyake. Nimechoka mizengwe
   
 11. mpenda pombe

  mpenda pombe JF-Expert Member

  #11
  Jul 8, 2017
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,188
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180

  Maalim kawa mpole.. Magufuli hayumbishwi.
   
Loading...