MAALIM SEIF: Uchaguzi wa Zanzibar ulikua safi hauna GHILBA hongera ZEC

LUKAZA

Senior Member
Nov 30, 2010
140
70
MAALIM SEIF: Uchaguzi wa Zanzibar ulikua safi hauna GHILBA

Ndio huu ndio ukweli usionashaka kwa Watanzania kuambiwa ukweli na kuacha zile zama za Kina Chadema kukataa Ukweli hali ya kuwa wanajuwa kuwa wameshindwa kihalali bila ya hilba yoyote ukweli Tume za za Tanzania(ZEC NA NEC) zinajitahidi kufanya uadilifu ila kinachokosekana ni uchu wamadaraka kwa viongozi wetu na si kuwapigania wananchi wao ila leo sitakwenda mbali sana ila hebu tumsome hii habari

MAKAMU wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amewathibitishia viongozi na wanachama wa chama cha CUF kuwa uchaguzi wa Zanzibar uliomalizika, ulikuwa safi na usio na ghilba.
Maalim Seif alisema hayo kwa nyakati tofauti, alipokuwa akizungumza na viongozi wa ngazi mbali mbali wa Chama hicho wa Wilaya za Mkoani, Chake Chake, Wete na Micheweni kisiwani Pemba.
Alisema kutokana na hali hiyo na imani aliyonayo kwa Mwenyezi Mungu kuwa humpa yule amtakae, na kwamba hakujaaliwa malengo aliyonayo ya kuiongoza Serikali ya Zanzibar iliyo katika mfumo wa Umoja wa Kimataifa.
Maalim Seif alisema, Jeshi la Polisi, kwa mara ya kwanza katika uchaguzi, limefuata maadili ya kazi zake bila ya upendeleo, kinyume na ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.
Makamu huyo wa Kwanza wa Rais, alisema ana imani na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein kwa kuonyesha nia njema kwa kutekeleza vyema kivitendo matakwa ya katiba kwa kugawa kwa uwiano mzuri Wizara za Serikali yake.
Maalim Seif, aliwataka Wazanzibari kudumisha amani na mshikamano kwa kuweka mbele uzalendo wa utaifa na kuelezea imani yake ya kukua kwa maendeleo nchini kutokana na kuwepo kwa maridhiano.
Aidha aliwataka wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka CUF, kwenda katika Mabaraza hilo la kutunga sheria na kuwajibika ipasavyo ili kufikia lengo na matarajio ya wananchi.
Katibu huyo alliwaonya Wawakilishi hao kuwa yeyote atakaeshindwa kutoa hoja au kushindwa kuuliza maswali ya msingi katika vikao vitatu atalazimika kujieleza, pamoja na kuagiza kutumiwa taarifa zao Ofisini kwake.
Nae Makamo Mwenyekiti wa CUF, Machano Khamis, aliwataka viongozi hao kuhakikisha vijana wote wasio na vyeti vya kuzaliwa, wanaandaa utaratibu wa kuvipata, sambamba na kitambulisho cha Mzanzibari, ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mkuu wa 2015.
Mapema katika salamu zao, Mawaziri waliotokea chama hicho walisema wanathamini sana dhamana walizokabidhiwa, hivyo watatumia uwezo wao wote katika kuwahudumia wananchi bila ubaguzi.
Kwa upande wake Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Abdillah Jihad Hassan, aliwathibitishia viongozi hao kuwa ndani ya kipindi cha miezi sita, Sauti ya Tanzania Zanzibar na Televisheni ya Zanzibar, vitasikika na kuonekana kwa usahihi kisiwani humo, sambamba na gazeti la Zanzibar Leo kufika kwa wakati.

Je kama toka uko nyuma angekuwa anakubali ukweli kama huu wananchi wangekimbia zanzibar na kwenda shimoni wazanzibar wangekuwa wapi toka wakati ule ila poa ndo tushapita zama zile sasa tunataka na kina CHADEMA watoke huko waliko wakubali matoke waache njaa ya kutaka kuwaulisha wanachi kwa ajili ya kujishibisha wao. waache udini

waslamu waachiwe wawe na mahakama yao ya KADHI ya nini kuwazuia
 
Uchu tu wa madaraka amepata sasa, alivyopewa kuzungumza yake machache b'da ya kutangazwa mshindi wa urais Zanzibar alilalamikia tume, ss hv anasifia Uchaguzi ulikuwa hauna tatizo. Mmmmmh!!!
 
Kwa hiyo, Maalim, angetokea mpinzani mwingine akasema kuwa uchaguzi haukuwa huru wala wa haki ungemuelezeaje? Yale madai ya Tume Huru ya Uchaguzi yamemalizwa na wewe kuteuliwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais ( ambaye hawezi kukaimu nafasi ya Rais akiwa hayupo)??
 
MAALIM SEIF: Uchaguzi wa Zanzibar ulikua safi hauna GHILBA

Ndio huu ndio ukweli usionashaka kwa Watanzania kuambiwa ukweli na kuacha zile zama za Kina Chadema kukataa Ukweli hali ya kuwa wanajuwa kuwa wameshindwa kihalali bila ya hilba yoyote ukweli Tume za za Tanzania(ZEC NA NEC) zinajitahidi kufanya uadilifu ila kinachokosekana ni uchu wamadaraka kwa viongozi wetu na si kuwapigania wananchi wao ila leo sitakwenda mbali sana ila hebu tumsome hii habari

MAKAMU wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amewathibitishia viongozi na wanachama wa chama cha CUF kuwa uchaguzi wa Zanzibar uliomalizika, ulikuwa safi na usio na ghilba.
Maalim Seif alisema hayo kwa nyakati tofauti, alipokuwa akizungumza na viongozi wa ngazi mbali mbali wa Chama hicho wa Wilaya za Mkoani, Chake Chake, Wete na Micheweni kisiwani Pemba.
Alisema kutokana na hali hiyo na imani aliyonayo kwa Mwenyezi Mungu kuwa humpa yule amtakae, na kwamba hakujaaliwa malengo aliyonayo ya kuiongoza Serikali ya Zanzibar iliyo katika mfumo wa Umoja wa Kimataifa.
Maalim Seif alisema, Jeshi la Polisi, kwa mara ya kwanza katika uchaguzi, limefuata maadili ya kazi zake bila ya upendeleo, kinyume na ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.
Makamu huyo wa Kwanza wa Rais, alisema ana imani na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein kwa kuonyesha nia njema kwa kutekeleza vyema kivitendo matakwa ya katiba kwa kugawa kwa uwiano mzuri Wizara za Serikali yake.
Maalim Seif, aliwataka Wazanzibari kudumisha amani na mshikamano kwa kuweka mbele uzalendo wa utaifa na kuelezea imani yake ya kukua kwa maendeleo nchini kutokana na kuwepo kwa maridhiano.
Aidha aliwataka wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka CUF, kwenda katika Mabaraza hilo la kutunga sheria na kuwajibika ipasavyo ili kufikia lengo na matarajio ya wananchi.
Katibu huyo alliwaonya Wawakilishi hao kuwa yeyote atakaeshindwa kutoa hoja au kushindwa kuuliza maswali ya msingi katika vikao vitatu atalazimika kujieleza, pamoja na kuagiza kutumiwa taarifa zao Ofisini kwake.
Nae Makamo Mwenyekiti wa CUF, Machano Khamis, aliwataka viongozi hao kuhakikisha vijana wote wasio na vyeti vya kuzaliwa, wanaandaa utaratibu wa kuvipata, sambamba na kitambulisho cha Mzanzibari, ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mkuu wa 2015.
Mapema katika salamu zao, Mawaziri waliotokea chama hicho walisema wanathamini sana dhamana walizokabidhiwa, hivyo watatumia uwezo wao wote katika kuwahudumia wananchi bila ubaguzi.
Kwa upande wake Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Abdillah Jihad Hassan, aliwathibitishia viongozi hao kuwa ndani ya kipindi cha miezi sita, Sauti ya Tanzania Zanzibar na Televisheni ya Zanzibar, vitasikika na kuonekana kwa usahihi kisiwani humo, sambamba na gazeti la Zanzibar Leo kufika kwa wakati.

Je kama toka uko nyuma angekuwa anakubali ukweli kama huu wananchi wangekimbia zanzibar na kwenda shimoni wazanzibar wangekuwa wapi toka wakati ule ila poa ndo tushapita zama zile sasa tunataka na kina CHADEMA watoke huko waliko wakubali matoke waache njaa ya kutaka kuwaulisha wanachi kwa ajili ya kujishibisha wao. waache udini

waslamu waachiwe wawe na mahakama yao ya KADHI ya nini kuwazuia
Ufafanuzi kidogo hapo kwenye bold mkuu,
Ni lini CDM waliwaulisha watanzania na wapi, data please, na kama huna data ni upupuuuuu, Katika mada hii what is the connection with mahakama wa kadhi? what is the connection kati ya ZEC na NEC? Je wajua kuwa mwenyekiti wa CUF Lipumba alisema kulikuwa na kasoro katika uchaguzi siku ile matokeo yalipotangazwa? If so who is right mwenyekiti wa chama au Katibu? Nisaidie tu kuelewa mkuu
 
wanaJF na hasa kama wewe si CCM au mpenzi wa CCM usipoteze muda wako kusikiliza propaganda za CCM.

Ukisoma thread utaona kuwa mleta mada ni CCM ambaye anapenda sana kuona wapinzani wanaacha kuishughulikia CCM na serikali zake badala yake wanajiingiza katika kutuhumiana, kudharauliana. kurushiana madongo.

Kama mchangiaji mmoja alivyouliza kuna uhusiano gani kati ya mada na mahakama ya kadhi. Mleta mada anajaribu kulikoroga ili litibue hisia nzito. Kama haitoparaganya mawazo yako ukaanza kumu-attack Seif,
na CUF . basi atakupata katika udini.

Jawabu mjibuni, asante mkuu kwa taarifa tu, halafu aende akachukuwe ujumbe mwengine kutoka kwa waliomtuma atuletee.

Iwe ni kweli Seif amesema hivyo kama huyu mleta mada anavyotuambia. Sisi tulimsikia Seif akisema kulikuwa na kasoro nyingi ila alikubali yaishe. CCM sasa hivi wanatafuta kila mwanya waharibu makubaliano ya GNU kama vile walivyoharibu miafaka ya mwanzo.

Kwa hiyo, hata kama Seif amesema uchaguzi ulikuwa mzuri, huru, wa haki, haukuwa na kasoro yoyote basi kwa watu weledi wa siasa watajuwa ni lugha ya kidiplomasia tu. Anajuwa CCM watachokonoa popote, kila kona, watatafuta kila sababu ili GNU isisimame, ianguke chini, isifanye kazi vile ilivyokusudiwa halafu wailaumu CUF. Halafu wao waendelee kupeta!!!

LUKAZA katafute jungu jengine ,mkuu ,utuletee . Hili tumelishitukia.
Unataka wapinzani waanze kurushiana madongo!! Unataka wakiristo wavurugane na waislamu kwa maslahi ya CCM. Heko mkuu.

AU ni nini madhumuni ya mada yako. Tufafanulie ujumbe wako! Au unataka kutwambia kuwa tayari mumemtia mfukoni Seif ?
Wacha kujifurahisha na malengo yako machafu! Usifanye kazi ya Shetani.
Ipeni nafasi GNU ifanye kazi, wazanzibari wapate afueni. Tukiona inafaa huko tunaweza kuiokoa Tanzania (na maafa) siku za usoni.
Hiyo model ,ikifaulu huko, itawezekana kujaribiwa na Tanganyika au kwako ni bora watu wafe ila CCM iendelee kutawala?

LUKAZA; Mkuu aste aste!
 
Labda ilikuwa moja ya ''masharti'' ya kupewa umakamu wa Rais - kwamba baada ya muda lazima aje mbele ma kusifia kwamba uchaguzi ulikuwa swafi. Sawa sawa!?

CUF kwishnehi. watakuja na mpya gani tena 2015 wakati na wao ni part of the failed system? CCM wamelamba dume hapa. Huu muafaka sio ''win-win'' bali ni ''win-lose'' na CCM ndo wamemchapa bao CUF
 
Mkuu.
Tuchukulie kuwa hali ya Zanzibar kiuchumi iki-improve, wananchi wakapata kazi, maisha yakawa afueni kwa wakaazi wa huko. Jee huoni hapo ni kuwa CUF watakuwa wamewapiga bao CCM? Wananchi watajuwa kuwa CCM ndiyo ilikuwa inawaadhibu bila ya sababu za msingi. So next election, mpiga kura atajuwa nani anastahiki kupewa kura.
Ninavyoamini ni kuwa CCM watajaribu kuuchakachuwa muafaka na GNU ili waliolala wasiamke.
kuna sehemu hapa JF imeletwa mada kuwa kuna improvement tayari katika mahospitali, Wizara ya afya wamekabidhiwa CUF.

katika hii mada ya LUKAZA kuna waziri wa habari ameahidi kuwa katika miezi 6 wakaazi wa Pemba watapata matangazo ya TV na redio bila matatizo, wizara hii ipo chini ya CUF. Kama CCM hawata-sabotage uendeshaji wa GNU basi CUF have nothing to loose, but to gain.
Hata CCM wa zanzibar watajitahidi walete improvement ili na wao wasiachwe nyuma na CUF. Ultimately, atakaefaidika itakuwa ni wananchi wote na itakuwa ni win-win kwa CCM na CUF.
Tuwaombee dua, GNU ifanikiwe na hiyo itakuwa chachu kwa CCM bara and may be tutapata GNU kwa Tanzania yote.

Kwa ambaye hajui GNU inafanya kazi vipi, afanye utafiti kwanza kabla ya kukurupuka na kumwaga upupu humu, (I mean siyo GNU African style!) Sehemu nyingi duniani wanatumia huu mfumo na una mafanikio mazuri. usiniambie nikupe mifano, google, mkuu!

Hata kule Zanzibar walipeleka watu wao kutoka CCM na CUF kwenda Ujerumani na Uingereza kujifunza vipi GNU, Serikali ya mseto/ serikali shirikishi inafanya kazi. Kama walifuzu mafunzo yao basi tutegemee mafanikio huko Zanzibar.
Let us be optimistic!
 
"Maalim Seif alimpongeza Dk. Sheni kwa kupata ushindi huo na alimsifu kuwa ana uwezo, uzoefu na mahaba ya kuiongoza nchi yake. Alisema ushindi wa Dk. Shein ni uametokana na uamuzi wa wazanzibari.

Alisema tume ya uchaguzi ya Zanzibar imefanya kazi nzuri kwa kuwa uchaguzi ulikuwa haki na huru, lakini alimuomba mwenyekiti wa tume kurekebisha kasoro za baadhi ya maofisa wake wanaokiuta taratibu za uchaguzi.

Maalim Seif alisema mwenyekiti wa tume na maofisa wake wa ngazi ya juu wanafanya kazi nzuri, lakini baadhi ya maofisa wa chini ndio wamekuwa wakileta dosari. Alimpongeza Dk. Shein kwa kumkubatia na kumuomba awaeleze wafuasi wa CCM wasiwabeze wenzao wa CUF kwa kuwa ushindi wake ni ushindi wa wazaznibari wote. Alisema uchaguzi ulikuwa huru iklinganishwa na uchaguzi uliopita.

Kwa upande rais mteule Dk. Shein alimsifu Maalim Seif kwa hotuba yake fupi lakini yenye maneno mazito na kwamba amemtia moyo sana katika kuwatumikia wazanzibari."

..............................................................................................................................................................................
"I do not have sympathy for politicians at all because when the politician wants your vote, he can promise all sorts of things which are sometimes unrealistic, just to convince you to vote for him. But when the time of accountability comes, they then turn (around) to tell you their promises were not legally binding." - Andrew Edwin Arthur
 
Bwana LUKAZA hivi Wewe ni Mtanzania au umetoka kenya maana nashindwa kukujadili pamoja na mada zote naomba uwasiliane na Nonda akusaidie kidogo kama sio kibaraka wa CCM
 
Bwana LUKAZA hivi Wewe ni Mtanzania au umetoka kenya maana nashindwa kukujadili pamoja na mada zote naomba uwasiliane na Nonda akusaidie kidogo kama sio kibaraka wa CCM

Mkuu
Hapa kwa muundo wa tungo( sentensi) basi ,inaweza kusemwa kuwa umetumia tungo tata.umeua ndege wawili kwa jiwe moja. Yaani unatuhumu, au umeweka dhana kuwa mmoja kati yetu ni kibaraka wa CCM. Kama uliiweka kwa kukusudia basi imekaa kiufundi.

Nothing serious! Kwa mtu mwengine ingeweza kuwa ndiyo umewafungulia ..... Let the dogs out!

Nimefarajika kusoma ; katika post yako nyengine, kuwa unaamini naweza kuwa mwalimu.
ukweli mimi ni mtu mdogo sana, yaani ni mtu wa kawaida tu, ila ni mpenzi wa siasa, nafuatilia sana mijadala ya siasa na si mwanachama wa chama chochote cha siasa Tanzania. Ni mtanzania though!
 
Back
Top Bottom