Maalim Seif tulikuambia achana na Lowassa, hukusikia!

Umeandika kwa uzandiki na kwa mtindo wa kizombi japo una hoja nzuri, umeiweka kijinga jinga kabisa, na unafiki wa mizimu kama CCM. Ningechangia vizuri ila nia yako ni ya mizimu hivyo kabisa. Kwenda zako uko siku nyingine andika vizuri bila kulamba ugoro sawa.
Wewe ndiyo unatakiwa kwenda huko kwa sababu sijakuita kwenye thread yangu.

Ni uamuzi wako kuchangia au kutochangia.

Karibu sana!
 
Masopyakindi,
Unapeleka pole sipo.
Wa kupewa mkono wa taazia ni CCM Zanzibar ambao walishindwa uchaguzi.

Hili la Maalim Seif kugombea urais unanishangaza.
Kwani uchaguzi ulikuwa wa nini?

Anaetaka kwa pupa si CUF.

CUF juu ya madhila yote ambayo sote tunayajua wanachama wake wamebaki
watulivu.

Nasoma ushauri wako wa miaka 20 nacheka peke yangu.
Karume alisema uchaguzi baada ya miaka 50.

Hakika mdomo haumkatai bwana wake.
Kuna mambo utayapata Afrika katika dunia nzima.

Nakuwekea picha ambayo siku Karume alisema uchaguzi baada ya miaka 50.

2016%2B-%2B1

Abeid Amani Karume akizungumza na David Martin kushoto ni Ali Nabwa na
huyo binti ni Bi. Nasra Mohammed mtangazaji Radio Zanzibar katika mazungumzo
haya ndipo Karume aliposema: ''No election in Zanzibar, Ok, election in Zanzibar
after 50 years.''
Mohammed Said, naona kwa njia nyingine unakubaliana na maono ya Mzee Karume na ya kwangu vile vile.
Ingawaje kwa shingo upande.
Mafanikio makubwa ya CUF ni ile kuweza kuingia GNU baada ya sokomoko la siku nyingi la kisiasa huko visiwani.
Hilo halina ubishi.
Si unajua jinsi siasa za Zanzibar zilivyoanza kupoa baada ya mapinduzi!
Kwanza lilikuwepo MB, Baraza la Mapinduzi.
Mtu akiwa MBM, kule visiwani alikuwa akiogopewa kama kamungu kadogo.
Sasa hivi BM ni kama taasisi tu ya Wazanzibari waliopundua nchi mwaka 1964.
Likaingia Baraza la Wawakilishi, na hili lilichukua muda kuzoeleka ili siasa ziekeweke kewa ni ushirikiano.
Hilo likapita na kukubaliwa.
Ikaingia GNU, na hili nalo lilikuwa lipewe muda likomae, lieleweke kwa Wazanzibari, na kwa hakika ilikuwa sehemu nzuri wazanzibari wamefika katika maelewano.

Sasa tumchambue Maalim.
Yeye kagombana na KILA KIONGOZI wa Zanzibar toka awe mwanasiasa.
Ukianzia usaliti wake kwa Mahmoud Jume, kwa Abdul Wakil, Salmin Amour, hadi kuishia sasa kwa Shein Mohammed, yeye kauma meno tu!

Angeishia GNU , ili awape wengine nafasi ya maelewano, Zanzibar ingeendelea mbele kisiasa.
Sasa wamerudi nyuma na GNU iko mashakani.
Maalim alioa katika hili.
 
Serikali Haramu ya Zanzibar (SHZ) kwa sasa haina fedha na inasemekana kila siku inamhimiza Magufuli awasaidie angalau wavuke miaka mitano,hadi sasa haijaweza kulipa mishahara kikamilifu ,tayari hela ya mafuta ya kutia kwenye gari zao za serikali zimeanza kukisiwa na masharti kibao ,sasa ukame wa hela umeanza kuinyatia serikali hio ,wengine wameanza kutumia hela za mifukoni mwao wakitegemea miradi ambayo nayo si muda itaanza kunywea.
Porojo tupu!

Sorry.
 
Mfianchi,
Hili jambo liko wazi sana na limashajadiliwa huko nyuma.
Maalim hakujitangaza.

Matokeo yalikuwa yashatoka.

Tatizo ni kuwa Maalim alikuwa ameshinda tena kama vile
alivyoshinda 2010.
Hapana tulisikia kwa masikio yetu Maalimu akijitangaza DW wakati tume haijatangaza hayo matokeo.Hayo matokeo unayosema yalikuwa yametoka yalitangazwa na nani? nadhani tuanzie hapo na hizo takwimu kuwa Maalimu seifu alishinda zimetoka wapi.
 
Kwa hali ya sasa Zanzibar hili swali halina mantiki!

Swali ambalo linatakiwa ni kufahamika ni hatima ya maisha ya CUF nje ya uongozi.

Nini hatima ya Maalim Seif baada ya kupokea ushauri wa Lowassa na kuufanyia kazi?
Okey. Kwa hiyo kama wewe ungemshauri nini Seif kwa mfano.. Hana kosa lolote coz hata kama angeshiriki ule uchaguzi wa marudio asingeshinda! Usimlaumu bure
 
Wasioijua Zanzibar na wazanzibari, ndio siku zote na ndio fikra zao pia, , cuf zanzibar imo ndani ya mioyo ya watu , ulioambatana na uzalendo, , kama cuf itakufa zanzibar basi na Zanzibar pia itakufa, , ama M/Lowasa alipata mapenzi ya dhati Kwa watanzania kwa muda mdogo tu kupitia ukawa kwa tkt ya chadema, si dhani kama ni msanii wa siasa awe na mapenzi kama hayo kwa mda mdogo, ,nguvu ya ukawa pia tumeiyona ni wabunge wangapi wamepatikana na meya kitu. Kilichokuwa hakijawahi tokea. ... mwenye macho. ......
 
MsemaUkweli,
CUF haipo nje ya uongozi.

CUF ndiyo chagua la Wazanzibari na wanaitazama CUF kwa sura
hiyo.

CUF inatawala nyoyo za Wazanzibari.
Angalia Maalim Seif anavyopokewa na wananchi.

Fananisha.
Utapata jibu.

Ingia hapa:
Mohamed Said: MAALIM SEIF KATIKA SALA YA IJUMAA MSIKITI WA MSUMBIJI
Mzee Mohamed Said

Umeanza kuleta hoja kama za vijana wa CHADEMA waliokuwa wanatuambua Dk. Slaa ni Rais wao wa mioyoni lakini hao hao leo wanaongoza kumtukana Dk. Slaa baada ya Lowassa kuingia CHADEMA.

Jenga hoja zenye msingi wa uhalisia. Acha propaganda ambazo haziwezi kubadilisha ukweli wa hali ya kisiasa Zanzibar.

Nasikia kwa sasa kuna marumbano makali yanaendelea ndani ya CUF kuhusu uamuzi wa CUF kususia Uchaguzi ambao umepelekea kupoteza majimbo yote ya Zanzibar.
 
Mzee Mohamed Said

Umeanza kuleta hoja kama za vijana wa CHADEMA waliokuwa wanatuambua Dk. Slaa ni Rais wao wa mioyoni lakini hao hao leo wanaongoza kumtukana Dk. Slaa baada ya Lowassa kuingia CHADEMA.

Jenga hoja zenye msingi wa uhalisia. Acha propaganda ambazo haziwezi kubadilisha ukweli wa hali ya kisiasa Zanzibar.

Nasikia kwa sasa kuna marumbano makali yanaendelea ndani ya CUF kuhusu uamuzi wa CUF kususia Uchaguzi ambao umepelekea kupoteza majimbo yote ya Zanzibar.
MsemaUkweli,
Nimekueleza kuwa ukitaka kunifananisha mimi na watu wengine
utatabika sana.

Unasema umesikia kuwa kuna mjadala wa kupoteza majimbo?
Majimbo yapi yaliyopotezwa?

Msomi makini anafanya kazi na utafiti kwenye ''facts.''
Msomi makini hashughulishwi na ''hearsay.''

Zingatia hili ikiwa unataka mimi na wewe tufanye mjadala.
 
Mkuu Mohamed Said
Hoja siyo kushinda au kushindwa uchaguzi, hoja yangu ni CUF kujikuta iko nje ya utawala wa Zanzibar kuanzia madiwani mpaka Rais kutokana na ushauri kutoka kwa Lowassa.
MsemaUkweli,
Umempenda sana Lowassa.
Mimi siwezi kuzungumza habari za Lowassa hadi niwe na taarifa kamili.

Hili la kujikuta nje ya utawala linanistaajabisha jinsi lilivyokukaa kooni.
Uchaguzi si ulifanyika na CUF wakashinda uchaguzi CCM ikafuta?

Sasa CUF watakuwaje katika utawala wakati CCM hawakubali kushindwa?
Labda nikusaidie tujitoe katika huu mkwamo wa ''CUF nje ya utawala.''

Ni hivi.
Mapambano yamechukua sura nyingine.

Moja ya sifa za ''political scientist'' ni kuwa na uwezo wa ''prediction,''
yaani awe na uwezo wa kufanya utabiri.

Utabiri wangu mimi ni huu.

Siasa za Zanzibar zinaingia ''level,'' ya kuwatazama viongozi waliojiweka
madarakani katika sura ambayo (naogopa kulisema neno lenyewe)...

Hii itachukua sura ya Wazanzibar kupigania kitu kikubwa zaidi na halitakuwa
tena suala la kuingia katika Bunge na Baraza la Uwakilishi.

Ni jambo kubwa kupita hili.
Wazanzibari watakuwa wanaigania uhuru wa nchi yao.

Ukiwa unaweza hebu soma historia ya Vidkun Quisling.
Utaelewa ninalokueleza.
 
Kwa taarifa za chinichini Serikali ya Zanzibar haijawalipa mishahara wafanya kazi wake huu ni mwezi wa tatu mbali ya miezi mingine iliyorukwa ,ila wameambiwa watulie kimya kama wanaonyolewa na atakaeleta fyoko anafukuzwa kazi kama ni ubunge au uwakilishi atausikia kwenye matangazo.

Kwa Serikali Ya Mapinduzi Zanzibar sasa viongozi wake wanafanya kazi ya kujitolea ,kazi bila ya mishahara na wananchi wameshaweka wazi hawaendi kulipa umeme wala maji.

Mbona wanasogeza bahari wajenge jiji la maana? Manake wako level nyingine sasa
 
Hapana tulisikia kwa masikio yetu Maalimu akijitangaza DW wakati tume haijatangaza hayo matokeo.Hayo matokeo unayosema yalikuwa yametoka yalitangazwa na nani? nadhani tuanzie hapo na hizo takwimu kuwa Maalimu seifu alishinda zimetoka wapi.
Mfianchi,
Nilikosea Dr. Sheni ndiye alishinda uchaguzi na hicho ndicho kisa
cha kufuta uchaguzi.

Hata uchaguzi wa 2010 Shein alishinda.
 
MsemaKweli,
Ikiwa utamleta Lowassa katika siasa za Zanzibar tutahangaishana.

Nimekueleza kuwa CUF ukifananisha na CCM Zanzibar, CCM haifui
dafu.

CCM ni chama dhaifu kilichochukua sura ya siasa kama zilivyokuwa
Haiti ya Papa Doc wakitawala kwa kupitia Ton Ton Macoute.

Ingia hapa:
Mohamed Said: COMPARE AND CONTRAST BETWEEN TON TON MACOUTE IN PAPA DOC's HAITI AND THE ZOMBIES IN ZANZIBAR
Mohamed Said
Msingi wa hoja yangu siyo udhaifu au uimara wa CUF kabla ya Uchaguzi Mkuu.

Hoja yangu ni maisha ya CUF baada ya Uchaguzi uliofanyika tarehe 20 Machi 2016

CUF inafutika katika uso wa siasa za Zanzibar kwa sababu ya ushauri wa Lowassa.
 
Mohammed Said, naona kwa njia nyingine unakubaliana na maono ya Mzee Karume na ya kwangu vile vile.
Ingawaje kwa shingo upande.
Mafanikio makubwa ya CUF ni ile kuweza kuingia GNU baada ya sokomoko la siku nyingi la kisiasa huko visiwani.
Hilo halina ubishi.
Si unajua jinsi siasa za Zanzibar zilivyoanza kupoa baada ya mapinduzi!
Kwanza lilikuwepo MB, Baraza la Mapinduzi.
Mtu akiwa MBM, kule visiwani alikuwa akiogopewa kama kamungu kadogo.
Sasa hivi BM ni kama taasisi tu ya Wazanzibari waliopundua nchi mwaka 1964.
Likaingia Baraza la Wawakilishi, na hili lilichukua muda kuzoeleka ili siasa ziekeweke kewa ni ushirikiano.
Hilo likapita na kukubaliwa.
Ikaingia GNU, na hili nalo lilikuwa lipewe muda likomae, lieleweke kwa Wazanzibari, na kwa hakika ilikuwa sehemu nzuri wazanzibari wamefika katika maelewano.

Sasa tumchambue Maalim.
Yeye kagombana na KILA KIONGOZI wa Zanzibar toka awe mwanasiasa.
Ukianzia usaliti wake kwa Mahmoud Jume, kwa Abdul Wakil, Salmin Amour, hadi kuishia sasa kwa Shein Mohammed, yeye kauma meno tu!

Angeishia GNU , ili awape wengine nafasi ya maelewano, Zanzibar ingeendelea mbele kisiasa.
Sasa wamerudi nyuma na GNU iko mashakani.
Maalim alioa katika hili.
Masopakyindi,
Napata shida sana kukuelewa.
 
Kama CUF Zanzibar mlidhani CHADEMA ya Lowassa itaweza kuwasaidia wakati wa shinda mtakuwa hamkufanya homework yenu vizuri au mlikuwa ni wale wasiosikia la mkuu...

CHADEMA ya Lowassa ni bomu linaloua ajenda za vyama vya upinzani nchini softly.

Lowassa aliingia CHADEMA kwa usanii wa kuja na wabunge 50 wa CCM, wenyeviti wa mikoa wa CCM zaidi ya 22, Wenyeviti wa wilaya zaidi ya 80 na wakuu wa wilaya lakini baada ya kuondoka CCM, alifuata na genge la wachumia tumbo wachache wasiozidi kumi ambao wengine wameanza kurudi CCM.

Lowassa aliua ndani ya CHADEMA ajenda ya kupambana na ufisadi na pia akaua ajenda ya kumsimamisha Dk. Slaa kuwa mgombea Urais wa Tanzania. CHADEMA ya Lowassa amekuwa CCM ya zamani ambayo ilikuwa ya kisanii na haikutaka kabisa kusikia ajenda za ufisadi na rushwa.

Maalim Seif, Watu wenye fikra pana walikuwa wanakuchora wakati unafunga safari za kutoka Zanzibar kwenda Mikocheni kwenye ofisi ya Lowassa ili kupata ushauri wa kisiasa.

Hukufahamu kama Lowassa ana shahada ya Usanii kutoka UDSM ambayo CCM waliishtukia na kumtosa katika uteuzi wa Mgombea Urais wa Tanzania.

Makelele ya CUF Zanzibar kuhusu CHADEMA ni kielelezo cha political frustration and beating a dead horse baada ya kuwekeza fikra zao kwa Lowassa ambaye kama kawaida yake amewaacha wamezama kwenye tope la kisiasa kama ilivyotokea kwa wapambe wengine wa Lowassa ambao miongoni mwao wameanza kurudi CCM.

CHADEMA iliyokuwa ikitoa misaada na ushauri wa dhati ni ile iliyokuwa chini ya Dk. Slaa.

Kutegemea CHADEMA ya Lowassa kukupa msaada kama wewe ni mpinzani ni sawa na kutegemea CCM ikupe msaada wa kisiasa!

Lowassa atawasaidia nini wakati fikra zake na marafiki zake bado ni CCM. Aliwatumia tu kwa manufaa yake binafsi ya kufika Ikulu na sasa anaiangalia CUF kama CCM Zanzibar wanavyoiangalia.

Nchi zinazotoa vikwazo vya kiuchumi ni nchi za Magharibi ambazo zinaamini CUF ina elements za Islamic fundamentalism. Kwa sasa huwezi kusikia tena kelele za nchi za Magharibi.

Hamkufahamu hata neno ‘’mahaba kwa Lowassa’’ lilianzishwa na viongozi wa CCM kutoka Zanzibar ambao kwao siasa siyo za kiitikadi bali ni siasa za kibaguzi kati ya Mwarabu na Mwafrika/mtu mweusi.

Ushauri wa kisanii aliokupa Lowassa wa kususia uchaguzi wa Zanzibar kwa kigezo kuwa atakusaidia katika kuzishawishi nchi wahisani ili waweke vikwazo vya kiuchumi kwa viongozi wa Zanzibar ili kunishinikiza madai yako lakini kwa sasa amekuacha umezama kwenye tope. Hakuna cha kikwazo cha kiuchumi wala CUF Zanzibar kuongoza Zanzibar.

Kama ilivyo tabia ya watanzania wengi, kwa sasa wameanza kuisahau CUF Zanzibar.

Mwandishi nguli wa Kibrazil aitwaye Paulo Coelho aliwahi kusema “People never learn anything by being told, they have to find out for themselves.”

Maalim Seif aliudharau msemo usemao, ''If you can't get what you want, just take what you get''.

Maalim Seif have learned the hard way!

CUF Zanzibar is dying slowly.

maalim_lowassa.jpg
umeandika kuhusu Maalim Seif lakini umetaja lowassa mwanzo mwisho , hivi uamuzi wa kususia uchaguzi wa kizushi wa 20 march ulikuwa wa Lowasa au baraza la uongozi wa CUF? hivi wewe masikini wa kutupwa wa fedha na akili ndio wa kumshauri Maalim Seif ? nimekudharau sana mkuu , lazima muwe na adabu kwa maamuzi ya vyama vya siasa yanayotokana na vikao halali , hapa JF si mahali pa kuandika ili ujifurahishe .
 
Fik

fikra pans in wizi was kura mchana kweupe. Jambo muhimu la kujua no kuwa CCM majambazi hayataondoka kupitia sanduku la kura. Lowasa alishinda wakaiba Maalim Seif alishinda wakaiba sasa ni suala la kujipanga namna kuua hawa panya
Yeah, Lowassa alishinda wakaiba! My left foot!

Mgombea ambaye hata kuongea dakika tano ilikuwa kama ni adhabu halafu kwa fikra zako kiduchu unadhani anaweza kushinda.

Alichokiweza Lowassa wakati wa kampeni ni kuwashikia fikra baadhi ya vijana na wakaamini kama atashinda nafasi ya Urais wa Tanzania.
 
Wakati mwingine unajitoa ufahamu na kusahau kilichotokea Zanzibar,uvunjaji wa Katiba uliotukuka,mbona hilo halizungumziwi wako wapi wasomi na wanasheria wetu? ingekuwa busara tujikite kwenye hilo suala kwanza kwa midahalo na mihadhara ili umma utambue tunahitaji kuheshimu Katiba wakati wote sababu Katiba ndio msingi wa kila kitu.
 
Kweli mkuu Lowass ameinajisi CDM na UKAWA kwa ujumula,yaani sasa hivi inashangaza CDM na vijana wake ndiyo wamegeuka watetezi wa mafisadi,yaani wamepteza kabisa moral authority ya kukemea ufisadi..Duh leo hadi akina msigwa wanalilia safari za nje ya nchi kwenda kuangalia nyumba za mabarozi..huku majimboni kwao kukiwa na shida ya madawati.
 
Back
Top Bottom