Maalim Seif: SUK ya 2010 - 2015 haikuwa na nia njema na raia wa Zanzibar. CCM walikubali ili kutimiza matakwa ya Kikatiba ila mioyo yao haikupenda

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,376
2,000
Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa ambaye pia ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema, Viongozi wa CCM ambao walishirikiana nao kuunda Serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar iliyoanza 2010 mpaka 2015 walifanya hivyo ili tu kutimiza matakwa ya kikatiba ila nyoyoni mwao hawakulitaka.

YOU MAY ALSO LIKE
WAZIRI AWESO ATAJA MIKAKATI YA SERIKALI KUMALIZA TATIZO LA MAJI DODOMA
14 HOURS AGO
WIZARA MPYA YAKUTANA NA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU
2 DAYS AGO
Maalim Seif ameyasema hayo huko Kizimkazi Mkunguni wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja alipokutana na Viongozi na Wanachama wa Chama cha ACT Wazalendo kutoka Mkoa wa Kati Unguja na Mkoa wa Kusini Unguja Kichama.

Maalim Seif ametoa kauli hio akijibu maswali baada ya kutoa fursa kwa Wanachama kuuliza nakutoa maoni yao ambapo wengi wa Wanachama walionesha hofu ya uwepo wa Serikali hii ya Umoja wa Kitaifa wakisema hapo kabla ilishakuwepo lakini faida yake haikuendelea kuonekana.

Maalim amewatoa hofu Wanachama hao kwa kuwaambia yakwamba;

“Kwa siku hizi 43 ambazo mimi nimeanza rasmi kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar nimeona wazi dhamira ya kweli ya Mh. Rais Mwinyi juu ya uwepo wa Serikali ya umoja wa Kitaifa, Kwani tunakaa pamoja, tunaongea, tunashauriana na tunaona yanatekelezwa, na hii ni ishara njema juu ya Umoja na Mashirikiano tunayoyataka Wazanzibari”.

Maalim Seif amesema Serikali kwa sasa inatakiwa
Kufanya marekebisho ya Katiba mpya ya Zanzibar ili tupate katiba mpya ambayo itaweza kurekebisha kasoro zilizopo.

Katika kuonesha umuhimu wa uwepo wa maboresho ya Katiba ya Zanzibar Maalim amesema;

“Tukipata Katiba mpya ya Zanzibar basi ndani yake tutapata Tume huru ya Uchaguzi lakini pia tutapata Majaji wa Mahakama walio huru na watakaotenda haki”.

Maalim ameendelea na msisitizo wake kwa Wazanzibari kwa kusema “Mimi ni M/kiti wa Chama cha ACT Wazalendo nikiwa katika shughuli za Chama, lakini mimi ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar hivyo nitahakikisha kila Mzanzibari anapata haki yake bila kuangalia itikadi ya Chama chake ikiwa tu ni Mzanzibari”.

Aidha, Maalim amesema huu ni muda wa kufanya siasa na kuboresha Chama chetu hivyo nilazima wote kwa pamoja tushirikiane kuanzia ngazi ya Tawi mpaka Taifa, kufanya majukumu ya kitaasisi sambamba na kuelekea Uchaguzi mkuu 2025, pamoja na hayo Maalim ameahidi kushuka katika matawi kuangalia utendaji.
 

Joselela

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
4,797
2,000
Wanasiasa ni watu wanafanya mambo kutimiza matakwa yao tu.

Kama ilikuwa hivyo kwanini hakuachia madaraka au kodi tamu sana.

Mzee ovyooo.
 

WAIKORU

JF-Expert Member
Dec 9, 2015
1,257
2,000
Usimwamini mwanasiasa. Hata jina lake akikwambia unapaswa kuuliza mtu wa jirani kama ni kweli.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom