Maalim Seif: Siasa za mivutano zinaathiri ustawi wa Zanzibar

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
MAALIM Self Sharif Hamad, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ameeleza athari zinazotokana na siasa za mivutano.

Akiwa kwenye ziara yake katika Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba jana amesema, mivutano ya kisiasa imekuwa ikiathiri ustawi wa Zanzibar.

“Sisi sote tuna maslahi mapana na hatma ya Zanzibar, na kama maslahi yakiwa mazuri sote tutanufaika, na maslahi yakiwa mabaya basi sote tutaathirika, hivyo lazima tutambue sisi ni ndugu na Zanzibar ndio nyumbani kwetu, tusishiriki kuibomoa nyumba yetu,” amesema na kuongeza:

“Wazanzibari tumepewa neema kubwa ya umoja, hata lugha yetu ya kuwasiliana ni moja ya Kiswahili, na hata dini waliowengi wanaabudu dini sawa, hii inaonesha kwamba hili ni taifa lililoshikamana, na hii ni tunu ya Taifa.

“Kwa hiyo nawasihi sana Wananchi wenzangu, asitokee mtu wa nje akaleta chokochoko na kulichafua Taifa hili, kwani gharama ya kuirudisha amani itakuwa kubwa sana.”

Maalim Seif ambaye aligombea urais visiwani humo kupitia Chama cha ACT-Wazalendo amesema, suala la ushirikiano katika nchi haliepukiki na kwamba, Zanzibar inahitaji umoja na mshikamano.

“Mpaka sasa kuna Serikali ya Umoja wa Kitaifa, hii ni kuonesha kwamba maendeleo ya Zanzibar yataletwa na Wazanzibar wenyewe,” amesema.

Maalim Seif pia amezungumzia ushirikiano wa Serikali na Chama cha Wananchi (CUF) mwaka 2010-2015.

Mfano mzuri wa mshikamano niule uliodumu kati ya mwaka 2010 mpaka 2015 ndani ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa, ambapo maisha ya utulivu na hali ya amani katika nchi yalionekana wazi, ila baada ya uchaguzi wa mwaka 2015 mambo yaliyotokea tumeona wote namna hali ya amani na Usalama ilivyochafuka mpaka kufikia katika uchaguzi mkuu wa 2020.

“Uchaguzi huu umeacha majeraha makubwa kwa wananchi, na hii imetokea baada ya kutokuwepo mashirikiano,” amesema na kuonveza:

“…mbali na yote yaliyotokea, mimi Maalim Seif na mwenzangu Rais Husein Mwinyi, tumesafiana nia na lengo letu kwa sasa ni kujenga nchi hii, kuweka umoja na mshikamano na dhamira yetu kuu nikuipeleka nchi hii katika hatma njema kwa maslahi yetu na vizazi vyetu”.

Maalim Seif amesisitiza kwamba, suala la maendeleo litafikiwa ikiwa Katiba ya Zanzibar itafuatwa kikamilifu, na kuheshimiwa kwa kuhakikisha Wananchi wote wanapata haki sawa sambamba na kupiga vita rushwa na ubaguzi.

Katika kukazia suala la Maendeleo, Maalim Seif amewaelekea viongozi wa Serikali kwa kuwaambia kwamba, “Mafanikio ya Zanzibar yatakuja kwa kutenda haki sawa na uadilifu kwa Wananchi.”
 
Chanzo Cha yote hayo.
Ni tamaa ya madaraka ya magufuli.
Siwalaumu halima mdee wala Maalim Seif.
Mimi lawama zangu ni kwa Magufuli.
Yeye ndo MUHARIBIFU.
haya yanayotokea ni matokeo ya dhulma aliyoifanya
Kwani Halima James Mdee amefikaje bungeni na kuapishwa?

Siasa ni Uongo.

Na Uongo na Wizi ni mapacha wanaofanana!
 
Chanzo Cha yote hayo.
Ni tamaa ya madaraka ya magufuli.
Siwalaumu halima mdee Wala maalim seif.
Mimi lawama zangu Ni kwa magufuli.
Yeye ndo MUHARIBIFU.
haya yanayotokea Ni matokeo ya dhulma aliyoifanya
Kwani maalimu Seif na Halima Mdee hawana tamaa ya madaraka?
 
Hadi Maalim nae unadiriki kupiga mikwala ya kishamba?

Hivi huyo wa kuigawa Zanzibar anatokea nchi gani
 
MAALIM Self Sharif Hamad, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ameeleza athari zinazotokana na siasa za mivutano....
Mpaka sasa zanzibar yanayotembea ni maneno mdomoni tu MIAKA 5 ikimaliza itaongea Rais Mwinyi hasa alikusudia nini alikuwa na maana gani lengo lake ni nini.

Lakini kama maneno matamu namna hii kutoka kwa Maalim Seif na lada kwa Rais kuna swali mimi linaniumiza kichwa sana - Kwanini mwinyi aliingia madarakani kwa mtutu wa bunduki?
 
Back
Top Bottom