Maalim Seif Sharif Hamad atangaza kuihama CUF na kujiunga na ACT-Wazalendo

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,577
6,582
427a3cf6-1404-4a3b-be6f-1e1665c83f6c.jpg


Caption:

1. Eddy Riyami

2. Mansoor Himid

3. Ismail Jussa

4. Maalim Seif

5. Zitto Kabwe

Vicheko hivi tuvichukulieje?

======
UPDATE:

MAALIM SEIF ATANGAZA KUJIUNGA NA ACT-WAZALENDO

58015832-04E1-40A6-811B-66DDACC93FC2.jpeg


Mwanasiasa mkongwe na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF ametangaza kukihama chama hicho na kuhamia ACT Wazalendo.

Maalim Seif ametangaza uamuzi huo mchana wa leo, Machi 18, 2019.

Wamachama wa CUF wanaomuunga mkono Maalim Seif walianza kubadili tangi za ofisi za chama hicho saa chache kabla ya kiongozi wao kutangaza kuhama.

Aidha kwenye matawi mengine ya CUF bendera ya chama hicho imeshushwa na kupandishwa ya ACT Wazalendo



47DAB7CC-76A4-418B-9AF8-B06E6453140C.jpeg




=====

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad leo Jumatatu Machi 18, 2019 ametangaza yeye, viongozi, pamoja na wafuasi wanaomuunga mkono kuhamia Chama cha ACT- Wazalendo.

Maalim Seif ametangaza uamuzi huo zikiwa zimepita saa chache tangu Mahakama Kuu ya Tanzania kuhalalisha uenyekiti wa Profesa Ibrahim Lipumba ndani ya CUF hali iliyomweka kando Maalim Seif.

Akizungumza na waandishi wa habari mchana wa leo Jumatatu katika ofisi za wabunge wa CUF Magomeni jijini Dar es Salaam, Maalim Seif amesema mapambano ya kisiasa lazima yaendelee.

“Mimi na wenzangu, tumetafakari kwa kina juu ya uamuzi wa kesi ulivyokwenda, tumeona kutafuta jukwaa jingine la kulitumia kuwa ni ACT- Wazalendo,” amesema Maalim Seif.

“Nawatangazia Watanzania wote na wanachama wote waliokuwa wanatuunga mkono mimi na wenzangu, tunajiunga na ACT- Wazalendo, tunawaomba wote wajiunge ili kuendeleza kazi kubwa tuliyokuwa tumeianza,” amesema.

Maalim Seif amewashukuru wale wote waliojitolea nyumba zao kwa ajili ya ofisi za CUF na kuomba waendelee kufanya hivyo wakiwa ACT- Wazalendo.

“Mapambano ya kujenga demokrasia sio kazi ya lele mama, tumefanya kazi kubwa hadi hapa tulipofikia,” amesema .

Amesema tukio hili ni historia mpya kote Zanzibar na Bara, “Umma haujawahi kushindwa kokote duniani, ndiyo historia inaonyesha, hatuna wasiwasi kuwa umma wa Watanzania nao utashinda.”

Kuhusu kuhama na nyadhifa zake, Maalim Seif amesema wanahamia huko pasi na masharti wala vyeo na wanakwenda kama wanachama wa kawaida na ikiwa watapewa vyeo watavichukua au la.

Akizungumzia nafasi ya wabunge amesema ni wana CUF, wengi wanawaunga mkono wao, “Tumewaachia wenyewe, kama watahama sasa au baadaye ni wenyewe, uamuzi wataamua wenyewe.”
 
Taarifa Inasema Maalim Seif Sharif Hamad atazungumza na wandishi wa habari mchana wa leo

----------

UPDATES FROM HIGH COURT DAR ES SALAAM:

Tarehe 18 March, 2019
----------

Mahakama Kuu mbele ya Jaji Benhajj Masoud, imeliondoa (Struck Out) shauri Namba 23/2016 lililokuwa linahoji Uhalali wa Lipumba ndani ya Chama cha CUF. Kwa hoja za kiufundi (Legal Technicality) aidha, Jaji ameeleza kuwa Msajili alikuwa na Mamlaka ya kufanya kile alichokifanya kumrejesha Lipumba ndani ya CUF.

PRESS CONFERENCE:

Maalim Seif Sharif Hamad atazungumza na Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini katika Mkutano utakaofanyika Leo tarehe 18/3/2019 katika Ukumbi wa Wabunge wa CUF uliopo Magomeni –Dar es Salaam.
Muda: Saa 8:00 mchana .

Nyote Mnakaribishwa.

Imetolewa leo Tarehe 18/3/2019 na;

MBARALA MAHARAGANDE


======

MAALIM SEIF ATANGAZA KUJIUNGA NA ACT-WAZALENDO

Mwanasiasa mkongwe na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF ametangaza kukihama chama hicho na kuhamia ACT Wazalendo

Maalim Seif ametangaza uamuzi huo mchana huu

Wamachama wa CUF wanaomuunga mkono Maalim Seif walianza kubadili tangi za ofisi za chama hicho saa chache kabla ya kiongozi wao kutangaza kuhama

Aidha kwenye matawi mengine ya CUF bendera ya chama hicho imeshushwa na kupandishwa ya ACT Wazalendo
 
Wazanzibari tunasubiri kauli ya kiongozi wetu mpendwa maalim seif sharif hamad. Atakapo amua kujiunga na chama chochote na viongozi wetu kwa ujumla nasi tupo nyuma.

Lipumba tutaonana 2020, uchaguzi Ndio utathibitisha ni nani kauwa chama na nani kaimarisha vyama.

Cuf ni watu na si sefu, kwa maana, maalim ni moja wa cuf hivyo atakako elekea nasi tupo, endelea na ujinga wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

33 Reactions
Reply
Back
Top Bottom