Zanzibar 2020 Maalim Seif: Nikichaguliwa, wakulima wa karafuu, viungo watauza popote duniani

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
1600330136716.png

Mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema endapo atapata ridhaa ya kuongoza, atahakikisha wakulima wa viungo na karafuu wanakuwa huru kuuza mazao yao sehemu yoyote wanayotaka duniani.

Maalim Seif aliyaeleza hayo katika Kijiji cha Konde, Wilaya ya Micheweni, ikiwa ni mwendelezo wa kampeni kupitia chama hicho katika Kisiwa cha Pemba. Alisema kazi ya Serikali yake itakuwa ni kukusanya kodi ndogo ili kuwafanya wakulima wapate faida kubwa, waweze kuendeleza kazi yao hiyo kwa maendeleo ya nchi.

“Katika Serikali ya CCM imekuwa ikichukua faida kubwa kulikoni wakulima wenyewe, lakini Serikali ambayo nitaiongoza, nitahakikisha inachukua kodi ndogo na kuwafanyia mazingira ya kukuza kilimo chao,” alieleza Maalim Seif.

Alisema kazi kubwa ya Serikali yake ni kuwapatia mbinu na mazinggira wakulima wa karafuu pamoja na bidhaa za viungo ili iwe ni njia ya kukuza uchumi wa Wazanzibar.

“Tunataka kuwalea wakulima wetu wa bidhaa za viungo ili waweze kuitangaza Zanzibar katika masoko ya ulimwengu ili baadae wafanyabiashara za viungo waje Zanzibar kununua wenyewe,” alisema Maalim Seif.

Alisema katika Serikali ya CCM wakulima wa bidhaa za viungo wanaonekana kuchoka sana kutokana na kuandamwa na kodi kubwa za kila sehemu.

Maalim Seif alisema katika utawala wake atawashauri wakulima wa bidhaa za viungo kujikita zaidi kwenye bidhaa za viungo ambavyo vitaleta tija za haraka kwao na Serikali kwa ujumla.

Pia alisema kazi nyengine ya kufanya ni kuhakikisha Zanzibar inakuwa na mifugo bora na soko la uhakika. Alisema atahakikisha huduma zote za mifugo zinapatikana ili kile kinachozalishwa kinakuwa bora katika masoko yote.

“Tutahakikisha viwanda vya madawa na vyakula vina vyakula vya mifugo yote vinapatikana hapahapa kwetu ili iwe rahisi wafugaji kuwahudumia mifugo yao,” alieleza Maalim Seif.

Alisema wafugaji wengi wa kuku Visiwani Zanzibar wameacha kufanya kazi hiyo kutokana na upatikanaji na ughali wa madawa na vyakula.

Akizungumza mbele ya mgombea huyo, mfugaji wa kuku katika Kijiji cha Mtambile Mkoa wa Kusini, Pemba, Humud Muhammed Said, alisema kama ingalikuwa chakula cha kuku kinatengenezwa Zanzibar hata tija ingaliongezeka.

Alisema kwa mfano kwa siku yeye anahitaji matumizi ya gunia mbili na nusu ambayo moja ni Sh 55,000. “Angalia kwa mwezi nitahitaji ngapi, kwa maana hiyo hatuwezi kupata faida nzuri kutokana na ughali wa vyakula… kama yangalikuwa yanazalishwa Zanzibar bei hiyo haiwezi kufikia,” alieleza Said.

Alisema ukiachana na vyakula, kuna madawa ambayo nayo wanaagizia nje ambayo mara nyingine yanachelewa sana. Kufuatia malalamiko hayo, Maalim Seif alisema katika utawala wake atafanya mapinduzi katika sekta ya mifugo na kilimo cha viungo na karafuu kwa ujumla.

Mtanzania
 
Siku moja nilikwenda darajani kununua spices. Nikataka karafuu, basi jamaa ananambia usiitamke waziwazi ivo. Nikauliza kwanini. kanamabia kuwa hawaruhusiwi kuuza karafuu. Balaa... "Karafuu ni zangu mwenyewe nkiziuza naambiwa nafanya magendo"
 
Hii ndio sera iliyokuwa ikisubiriwa na wazanzibari.Wakati ambapo karafuu ilifanywa ni zao la taifa na watu wakawa wanazuiliwa kuuza wapendapo wametoa mwanya karafuu kulimwa maeneo mengine ya bara na sasa Zanzibar ina karafuu chache kuliko mkoa kama wa Tanga,wakulima wa karafuu wamelishika soko la Kenya ambako wapemba wengi wamekufa kwa miaka kadhaa wakifukuzana baharini na askari wa kmkm eti wasisafirishe nje ya nchi wanapopeleka Mombasa.

Karafuu ni kiungo muhimu sana cha chakula na ni dawa ya maradhi mengi ikitumiwa peke yake au ikichanganywa na mimea mingine,hivyo mahitaji yake sio kule ambako serikali ya mapinduzi ilikuwa ikipeleka pekee.Wakulima wanaweza wakauza Afrika ya kati na kaskazini ambako kote wanazijua au kuzisikia na wanazihitaji.
 
Maalim anafanya kampeni kutimiza wajibu tu ila yeye ndio mshindi mpaka sasa.
Ana sera nzuri na anastahiki kuwa raisi lakini afanye tu kampeni na Mwenyezi Mungu anashuhudia lakini kura keshaibiwa zamani tangu wakati wa kuandikisha watu na ugawaji wa majimbo.
 
Back
Top Bottom