wagagagigi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2014
- 890
- 983
Toa tathmini ya maneno ya Maalim Seifu kwenye kwenye hii video
Anazidi kupagawa, Nyerere angeimalizaje Zenji, vile visiwa binadamu anavimalizaje, mzee anazeeka vibaya huku anajichongea kaburi lake la siasa. Kama maua yanavyochanua na kunyauka ndivo inavomtokea Maalim. Bahati mbaya ananyauka na kisirani.
Na Kafanikiwa kweli!
1984 Alitumika huyo huyo Seif kumfanyia Fitna Al marhuum Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi aliekuwa anakaribia kukata Minyororo ya Nyerere kwa Zanzibar lakin Seif Sharif Hamad akasimama kidete kuwa Upande wa Tanganyika kupinga Serikal 3 na tangu hapo Wazanzibar hawaaminiani kwa kuwa huamini kwny Mikakat Yao kuna uwezekano Vi Seif Sharif kadhaa vikawepo.
1964 Zanzibar Empire ilijiunga na Tanganyika.
2016 Zanzibar Minicipal Rais Wake anachaguliwa Dodoma na Wajumbe wa NEC kutoka Mbambabay , Nshamba Muleba, n.k. Seif ndio anabeba Msalaba huu asijifanye Sungura kumtupia Nyerere.
Naukumbuka wakati wa utawala wa Aboud Jumbe ,huyu raisi alikuwa dikteta kwelikweli,Wazanzibari tulikuwa sote tunavaa nguo za aina moja kwa jina "vitenge maalumu",kula kwa kadi "ration",kununua mkate wa boflo inabidi uamke saa tisa alfajiri ukae foleni mkate unapa saa mbili asubuhi,sembe la njano kwa ugari.wazanzibari walianza kula ugari wakati wa utawala wa Jumbe
Kama kweli Maalim kafanya hayo aliyoyafanya kumzuia Jumbe asitoke kwenye muungano basi maalim alifanya jambo la maana sana kwani huyu jamaa sijui angelitupeleka wapi,Maalim aliinusuru Zanzibar isiangamie kama anavyojitahidi hivi sasa.