Maalim Seif ni Mfadhilri wa TV Imani amesha wahihiza Waislam kuichangia kwa nguvu Zote!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maalim Seif ni Mfadhilri wa TV Imani amesha wahihiza Waislam kuichangia kwa nguvu Zote!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KING COBRA, Oct 13, 2012.

 1. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Maalim Seif, Shikh Ponda, Shikh Ali Basaleh ni wadau wa TV Imani ndio maana inatukana serikali na ukristo lakini haifungwi angalia hapa:
  [​IMG]Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akihutubia uwanja wa Taifa katika hafla ya kuchangisha kituo cha televisheni cha Imani.

  MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amewahimiza Waislamu nchini kote kujitokeza kwa wingi kuchangia uanzishwaji wa kituo cha televisheni kiitwacho Imani, kwa sababu televisheni hiyo itatoa mchango mkubwa kufuta dhana potofu dhidi ya Uislamu, na kutoa taaluma ya maadili mema ndani ya jamii.
  Alisema hayo leo alipokuwa akihutubia kwenye hafla ya kuchangia uanzishwaji wa televisheni hiyo, inayoanzishwa chini ya Jumuiya ya Islamic Foundation, ambayo pia inaendesha Redio Imani iliyopo mkoani Morogoro. Maalim Seif alisema vituo vingi vya televisheni hapa nchini mara nyingi huonesha vipindi vinavyokwenda kinyume na maadili mema ya jamii, jambo ambalo kwa kiasi kikubwa linachangia kuharibu maadili ya jamii na zaidi vijana na watoto wadogo.
  Makamu wa Kwanza wa Rais alisema mbali ya kujenga maadili mema kituo hicho cha televisheni pia kitaweza kufanya kazi kubwa ya kuwaelimisha wanajamii, juu ya mazuri na mchango wa Uislamu na kufuta dhana inayoenezwa na baadhi ya watu, dhana ambazo zinapotosha na kuipaka matope dini ya Kiislamu.
  “Waislamu jitokezeni kuchangia mambo ya kheri, kuanzishwa kwa televisheni hii ni jambo la kheri, wafanyakazi serikalini, Mashirika ya Umma na taasisi binafsi changieni, na wala msione haya kujuilikana nyinyi ni Waislamu, Uislamu ndio dini sahihi” alisisitiza Maalim Seif.
  Alieleza kuwa wapo waislamu wenye uwezo mkubwa na nafasi ya kuchangia mambo kama hayo yenye faida kwao na Waislamu wote, lakini kuna wengi miongoni mwao , licha ya kuwa na uwezo huo wamekuwa wagumu kutoa, na badala yake kujikita zaidi katika kuchangia mambo ya anasa.
  Katika hafla hiyo, Waislamu mbali mbali walijitokeza kuchangia ambapo, Makamu wa Kwanza wa Rais alichangia shilingi milioni mbili kwa ajili ya uanzishwaji wa kituo hicho cha televisheni. Akizungumza katika hafla hiyo, Sheikh Ali Basaleh alisema vyombo vingi vya habari nchini, vikiwemo vituo vya televisheni havina tabia ya kutangaza mambo mema yanayogusa Uislamu na Waislamu, na badala yake vyombo hivyo vimekuwa vikijikita zaidi kuripoti mambo mabaya dhidi ya Uislamu na kuyapa umuhimu mkubwa.
  Basaleh alieleza kwamba televisheni hiyo ya Kiislamu ikianza matangazo yake itasaidia kutangaza na kutoa taaluma juu ya mambo ya Uislamu, ikiwemo kufuta dhana hizo potofu zinazoupaka matope Uislamu. Mkurugenzi wa Islamic Foundation, Sheikh Arif Nahad alisema Waislamu wakiamua wanaweza, kwasababu hivi sasa wameamka baada ya miaka mingi ya kujiweka nyuma na kufunga mikono katika shughuli za kimaendeleo.
  Sheikh Nahad alieleza kuwa hakuna sababu televisheni hiyo ishindwe kuanza, na kwa kuwa jumuiya yake imeahidi itatekeleza hilo na kuwaahidi mamia ya watu waliohudhuria kuwa televisheni hiyo ipo njiani inakuja.
  Habari na Khamis Haji, Picha na Salmin Said (OMKR)
   
 2. Cheche Mtungi

  Cheche Mtungi JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,487
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  CUF=RADIO IMANI=IMANI TV=UAMSHO nk!
   
 3. N

  Nzinyangwa Member

  #3
  Oct 13, 2012
  Joined: Aug 27, 2008
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh!!!! Kwa hiyo wewe ulitaka waislamu wasichangie chombo chao!!!!! Hivi wanasiasa wengine wanaochangia michango mbalimbali makanisani nalo iwe ajabu?? au? kweli hampendi kuona uislamu unaendelea. Hivi hii thread ina hoja yenye kichwa kweli??? Kumbe udini ukuimvaa mtu hata akili yake inashindwa kufanya kazi!!!!!!
   
 4. Dogo1

  Dogo1 JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,102
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  ndg hawa wagalatia bure kabisa, wamesahau kuwa viongozi wengi wa serikali wamekuwa wakichangia harambee zinazoendeshwa na makanisa. Hatujawahi sikia yakijadiliwa hayo JF. Bado wanaJF walio wengi wanamawazo mgando.
   
 5. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,076
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280

  tatizo lako nini.. hapo..?

   
 6. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,076
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  cant wait TV iman kuwa on Air! ..

  wapo watakao nuna na kukasirika!
   
 7. G

  Gene Senior Member

  #7
  Oct 13, 2012
  Joined: May 2, 2012
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anahutubia wasiofikiri mara mbili..........
   
 8. mpemba mbishi

  mpemba mbishi JF-Expert Member

  #8
  Oct 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mara nyingi watu kuguswa kwa
  vitendo mbalimbali ambavyo
  vinafanywa na sisi Waislamu na
  pia vilivyotajwa katika Biblia.
  Matendo na Ujumbe huyo
  yatakuwa katika maeneo kadhaa katika Biblia, Taurat na Injiyl. Sisi
  tu pamoja katika ’Ibaadah na
  matendo ambayo yalikuwa
  yakifanywa na Manabii
  waliotangulia na Mitume. Na bila
  shaka dalili hizi ndo zinazidi kututhibitishia kuwa Uislamu ni
  dini ya hakki kutoka kwa Allaah
  na ni dini ya Mitume na Manabii
  wote waliotangulia. Kama
  ituakikishiavyo Qur-aan yenyewe
  kuwa: “Semeni nyinyi: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na
  yaletuliyo teremshiwa sisi, na
  yaliyo teremshwa kwa Ibrahim na
  Ismail na Is-haaq na Yaaquub na
  wajukuu zake, na waliyopewa
  Muusa na ’Iysa, na pia waliyo pewa Manabii wengine kutoka
  kwa Mola wao Mlezi;
  hatutafautishi baina ya yeyote
  katika hao, na sisi tumesilimu
  kwake.� Qur- aan 2:136 Hizi
  zifuatazo ni baadhi ya ’Ibaadah iliyokuwa ikifanywa na Mtume
  ‘Iysa (‘Alayhis Salaam):
  Waislamu Kufanya Harakati Fulani
  Katika Maombi. Harakati Za
  Maombi Mbalimbali Katika Biblia
  Kutoka kwa Yesu: “Basi, akaenda mbele kidogo,
  akaanguka kifudifudi, akasali:�
  (Biblia, Mathayo 26:39) Kutoka
  kwa Musa: “Kisha
  Musa akainama mbio
  kuelekea chini na kusali� (Kutoka 34:8
  Biblia) Kutoka kwa Musa na
  Haruni: “Musa na Haruni
  wakaenda kutoka katika
  Kanisa mbele ya mlango
  wa hema na wakapiga nyuso zao chini� (Biblia, kitabu
  cha Hesabu 20:06) Kutoka kwa
  Ibrahimu: “Kisha Ibrahimu
  akaanguka chini kwenye uso
  wake ...� (Biblia, Mwanzo 17:03)
  Kutoka kwa Yoshua: “Kisha Yoshua
  akaanguka chini kwenye
  ardhi juu ya uso wake na
  akainama ...� (Yoshua
  5:14 Biblia) Kutoka kwa Ezra na
  watu wake: “Na wakapiga magoti wakamwabudu Bwana
  kwa uso kwenye ardhi
  “ (Nehemia 8:06 Biblia)
  “Popote mnapokutana kufanya
  ibada nataka wanaume wasali,
  watu waliojitolea kweli na ambao wanaweza kuinua
  mikono yao wakisali bila hasira
  wala ubishi� (Biblia 1 Timotheo
  2:08) “Eliya akainama chini ya
  ardhi na akainamisha uso
  wake kati ya magoti yake� (Ya kwanza Wafalme 18:42 Biblia) “Na
  Bwana akasema na Musa,
  akamwambia:� Nenda mbali na
  mkutano huu, nami baada ya
  muda nitawaangamiza “. Kisha
  wakapiga magoti juu ya nyuso zao. “(Biblia ya nne Musa
  16:44-45) Waislamu Husalimiana
  Kwa Kusema “Assalamu
  ’Alaykum� , Maana Yake:
  “Amani Iwe Nanyi� – Yesu
  Alikuwa Akisalimiana Kwa Njia Hiyo Hiyo “Wanafunzi wote wawili
  walipokuwa
  wakiwaambia hayo, Yesu
  mwenyewe akasimama kati yao,
  akawaambia “Amani iwe juu
  yenu.! “(Biblia, Luka 24:36) “Mnapoingia nyumbani wasalimuni
  wenyeji wake kwa salamu ya
  amani� (Biblia Mathayo 10:12)
  Waislamu Mara Nyingi Hutumia
  Neno - “Inshaa- Allaah� Ambalo
  Maana Yake Ni - “Mungu Akipenda� - Maneno Haya Pia
  Tunapata Katika Biblia “Ninyi
  hamjui hata maisha yenu
  yatakavyokuwa kesho! Ninyi ni
  kama ukungu unaotokea kwa
  muda mfupi tu na kutoweka tena. Mngalipaswa kusema:
  “Bwana akitujalia tutaishi na
  tutafanya hiki au kile� (Yakobo
  4:14–15 Biblia) Kuomba Kutoka
  Asubuhi Mpaka Jioni - Waislamu,
  Kuswali Mara Tano Kwa Siku, Katika Biblia Tunasoma: “Kuanzia
  pale jua linapopambazuka mpaka
  pale linapozama jina la Bwana
  litukuzwe� (Zaburi 113:3 Biblia)
  Kuomba Kwa Nyakati Fulani Kwa
  Siku - Waislamu Huomba Kwa Nyakati Fulani “Siku moja, saa
  tisa alasiri, Petro na Yohane
  walikuwa wanakwenda Hekaluni,
  wakati wa sala� (Matendo
  03:01) “Mwanamke mjane kweli,
  asiye na mtu wa kumsaidia, amemwekea Mungu tumaini lake
  na huendelea kusali na
  kumwomba msaada usiku na
  mchana. (Timotheo 5:05)
  “Je, si Mungu basi yake kupata
  haki ya kuchaguliwa, wakati wao kupiga kelele kwa Mungu mchana
  na usiku? Je, hao wanapaswa
  kusubiri?� (Luka 18:07 Biblia)
  Waislamu Wanachukua Wudhuu
  (Kutawadha) Kabla Ya Kuswali.
  Biblia Inasema Yafuatayo “Na Musa na Haruni na wanawe
  baadaye akanawa mikono na
  miguu kwa maji kutoka humo.
  Mara nyingi walipokuwa wakenda
  ndani ya hema ya kukutania, au
  kuja mbele ya madhabahu, Walikuwa
  wakijiosha, kama Bwana
  alivyomwagiza Musa. (Kutoka
  40:31-32 Biblia) “Wale ambao
  hujitolea na kujisafisha kwa
  maombi katika bustani, wakiongozwa na mtu ambaye
  anasimama pale katikati ...�
  (Isaya 66:17 Biblia) Biblia Inataja
  Nyumba Ya Maombi, Hii Inakuwa
  Tafsiri Ndani Ya Kiarabu Na
  Kiswahili Masjid Ni Msikiti “Na akawaambia: Imeandikwa: Nyumba
  yangu itaitwa nyumba ya sala ...
  '(Mathayo 21:13 Biblia)
  “... Kwa maana nyumba
  yangu itaitwa nyumba ya
  sala kwa watu wote� . (Isaya 56:7 Biblia) “Na
  akawaambia:� Imeandikwa:
  Nyumba yangu itaitwa nyumba
  ya sala. Lakini ninyi mmeifanya
  kuwa pango la wanyang `anyi� .
  (Biblia St Mathayo 21:13) Waislamu Kufunga Mwezi Wa
  Ramadhaan Na Kuwatia Moyo
  Kufunga Kwa Hiari. Swawmu
  Imeandikwa Hata Katika Biblia
  “Akafunga siku arubaini mchana
  na usiku, naye hatimaye kuwa na njaa� (Mathayo 4:02 Biblia)
  “Heri wenye njaa na kiu ya
  kufanya atakavyo Mungu, maana
  watashibishwa� (Mathayo
  5:06 Biblia) “Mnapofunga, msiwe
  na huzuni kama wanafiki. Wao hukunja nyuso zao wapate
  kuonekana na watu kuwa
  wanafunga... ..� (Mathayo
  6:16-18 Biblia) Sehemu ya Luka
  ya Biblia unaweza kusoma kama
  ifuatavyo: “Mtu anaweza pia kufunga kwa hiari katika nyakati
  za Agano Jipya kwa kawaida juu
  ya Jumatatu na Alhamisi. Kwa
  kufanya hivyo kila wiki ilikuwa ni
  ishara ya maalumu ya
  uchamungu. (Biblia, Luka 18:12) Waislamu Kutoa Kwa Maskini
  (Swadaqah)- Upendo. Katika
  Biblia Tunasoma “Jihadharini
  msije mkafanya matendo yenu
  mema mbele ya watu kusudi
  mwonekane nao. La sivyo, Baba yenu aliye mbinguni hatawapeni
  tuzo. Basi, unapotoa sadaka,
  usijitangaze. Usifanye kama
  wanafiki wafanyavyo katika
  masinagogi na njiani ili watu
  wawasifu. Kweli nawaambieni, hao wamekwisha pata malipo yao.
  Lakini wewe unapotoa sadaka,
  mkono wako wa kushoto usijue
  mkono wa kulia umefanya nini.
  Toa sadaka yako kwa siri. Naye
  Baba yako aonaye yaliyofichika, atawapa thawabu. “(Mathayo
  6:1-4 Biblia) Waislamu Hawali
  Nguruwe, Damu, Au Wanyama
  Wafu. Biblia Pia Inakataza Hilo
  “Nguruwe msimle; ana kwato
  zilizogawanyika lakini hacheui; kwenu huyo ni najisi. Kwa sababu
  wanyama hao ni najisi msile
  nyama yao wala msiguse mizoga
  ya� (Biblia Walawi 11:7-8)
  Baadaye katika aya ya 21 ya
  sura hiyo tunasoma yafuatayo: “usile kitu kilichokufa chenyewe.
  “... Na wale wenye kula nguruwe
  na uchafu mwingine, ndiyo, pia
  panya, watapotea wote, asema
  Bwana� . (Isaya 66:17 Biblia)
  “Bali tuwapelekee barua kuwaambia wasile vyakula
  vilivyotiwa najisi kwa
  kutambikiwa sanamu za miungu;
  wajiepushe na uasherati; wasile
  mnyama yeyote aliyenyongwa,
  na wasinywe damu.� (Biblia Matendo 15:20) “Ni lazima tu
  subiri si kwa kula damu. Kwa
  sababu damu ni roho na roho
  usile na nyama. Unapaswa
  kumwaga kwenye ardhi kama
  maji “. (Kumbukumbu 12:23-24 Biblia) “Na kama mtu wa nyumba
  ya Israeli, au mmoja wa wageni
  ambao wanaishi kati yao,
  akinywa damu yoyote, nami
  nitaweka uso wangu dhidi yake
  ambae anakunywa damu na kumkatilia kwake mbali na watu
  wake� (Mambo ya Walawi 17:10
  Biblia) “Na hakuna damu yoyote
  mtayokunywa, ama kwa ndege
  au mifugo, bila kujali wapi mlipo.
  Kila mtu anaekunywa damu yoyote, huyo atakatiliwa mbali
  na watu wake “. (Walawi 7:26-27
  Biblia) Ni Haramu Kwa Waislamu
  Kunywa Pombe. Biblia Inatueleza
  Wazi Yafutayo “Uasherati na
  pombe lazima uondoshe akilini� (Hosea 4:11 Biblia) Je,
  wamesahau kwamba watu
  wabaya hawataurithi Utawala wa
  Mungu? Msidanganyike! Watu
  wanaoishi maisha ya uasherati,
  wanaoabudu sanamu, wazinzi, au walawiti. wevi, wachoyo, walevi,
  wasengenyaji,
  wanyang'anyi, hao wote
  hawatashiriki Utawala wa Mungu.
  (Biblia Kwanza Wakorintho
  6:9-10) Katika Uislamu ni haramu Riba. Biblia pia inakataza Riba
  “Unaweza kukopa fedha kwa ajili
  ya maskini yeyote kati yenu, kati
  ya watu wangu, hivyo ni lazima si
  kitendo dhidi yake kama walaji
  riba. Wala kuongeza juu yake faida yoyote� (Biblia, Kutoka
  22:25) “Usichukue faida yoyote
  ya ndugu yako, ama ya pesa au
  chakula au kitu kingine chochote
  ikawa umechukua riba� (Biblia,
  Kumbukumbu la Torati 23:19) “Na kama mnawakopesha wale
  tu mnaotumaini
  watawalipeni, je, mtapata tuzo
  gani? Hata wenye dhambi
  huwakopesha wenye dhambi
  wenzao ili warudishiwe kima kilekile!� . Biblia (Luka 06:34) “...
  faida na kuchukua riba - Je, ndo
  ataishi? Hapana, lazima wafe,
  lakini kwa sababu yeye kashiriki
  katika maovu hayo, atakuwa
  katika adhabu na kifo. damu yake atakuja juu yake “. (Biblia
  Ezekieli 18:13) Waislamu huchinja
  na kutoa Swadaqah ya kondoo
  mwanamke akijifungua. Hii pia
  imetajwa katika Biblia. “Na siku
  yake ya kujisafisha ikifika, ikiwa ni mvulana au binti, atachinja
  kondoo mwenye umri kwa
  sadaka ya kuteketezwa ...
  (Mambo ya Walawi 00:06 Biblia)
  Waislamu Hutahiriwa. Yesu Na
  Ibraahiym Na Manabii Wote Wa Israeli Walikuwa
  Wakitahiriwa? “Siku nane
  baadaye, wakati wa kumtahiri
  mtoto ulipofika, walimpa jina
  Yesu, jina ambalo alikuwa
  amepewa na malaika kabla hajachukuliwa mimba '(Biblia, Luka
  2:21) “Na Mungu akamwambia
  Abrahamu:� Utunze agano
  langu, wewe na uzao wako
  baada yako, na vizazi vyote. Na
  hili ndilo agano kati ya mimi na wewe na uzao wako baada yenu,
  ambaye mtazishika kila uume kati
  yenu kutahiriwa katika govi
  zenu, na hii itakuwa ni ishara ya
  agano kati ya mimi na wewe.
  Vizazi, kila mtoto wa kiume kati yenu atatahiriwa, wakati ni umri
  wa siku nane, kama walivyofanya
  mtumishi wa kuzaliwa katika
  nyumba yako na yeye ambaye
  kanunuliwa kwa fedha za kigeni
  kutoka kwa watu ambao si wa ukoo wako. Utahiriwa ni kwa
  mtumishi wenu na aliozaliwa
  katika nyumba
  yako na yule uliemnunua kwa
  fedha. Na ndiyo ahadi yangu
  katika mwili wako wazi kuwa agano la milele. Lakini mmoja wa
  watoto wa mataifa mengine mtu
  mmoja ambaye govi haijawahi
  kutahiriwa, naye atatengwa na
  watu wake. Yeye kavunjwa ahadi
  yangu. (Biblia, Mwanzo 9-14) “Na Ibrahimu alichukua mtoto
  wake Ismail na watumishi wake
  wote, mzaliwa wa nyumba yake
  na watu waliokuwa
  wamenunuliwa kwa fedha, kila
  uume kati ya watu wa Ibrahimu, na kutahiriwa siku hiyo govi yao
  ambayo Mungu alimwambia. Na
  Abrahimu alikuwa na miaka tisini
  na tisa. Wakati govi yake
  ilitahiriwa na mtoto wake Ismail
  alikuwa na umri wa miaka kumi na tatu wakati govi yake
  ilitahiriwa. Tarehe ya siku hiyo
  Ibrahimu katahiriwa, na mtoto
  wake Ismail. Na ya watu wote
  katika nyumba yake, mzaliwa wa
  watumishi wake wa nyumbani na wale ambao walikuwa
  wamenunuliwa
  kwa fedha kutoka mataifa ya
  nje, walikuwa wametahiriwa
  pamoja naye “. (Mwanzo
  17:23-27 Biblia) “Na Ibrahimu katahiriwa mtoto wake Isaka
  alipokuwa na umri wa siku nane,
  kama Mungu alivyomwamuru� .
  (Biblia, Mwanzo 21:04) Kuhusu
  kutahiri ipo katika biblia: “Agano
  la Kale liliteuliwa na Mungu kama ishara ya pekee kwa watu wa
  Israeli, na kama ukumbusho wa
  ahadi zao pamoja naye. (Kutoka
  17:09 a, 3 Mwanzo 0:03, Yohana
  7:22) Pamoja na kwamba mistari
  yote ya Wayahudi inashuhudia hivyo ikawa ni “moto� na utata
  suala ambalo lilisaidia kugawa
  watu baada ya kipindi cha Yesu.
  Kuoa Wake Wengi Katika Uislamu.
  Hata Katika Biblia Kumetajwa
  Kuoa Wake Wengi “Akichukua mke mwingine, basi asifanya
  upungufu wowote katika mlo wa
  zamani, mavazi au sheria za
  ndoa� . (Biblia, Kutoka 21:10)
  “Kama mtu ana wake wawili,
  mmoja anayempenda na mwingine ambaye hamuoni ...� (Biblia,
  Kumbukumbu la Torati 21:15)
  “Yeye alikuwa na wake
  wawili ...� (Biblia, Samuel 01:02)
  “Kwa hiyo, Daudi alifika huko
  pamoja na wake zake wawili ...� (Biblia ya Samuel 02:02) “Lakini
  wakati wa usiku aliamka na
  kuchukua wake wake wawili na
  watu wake wawili wahuduma na
  wanawe kumi na mmoja….�
  (Biblia, Mwanzo 32:22 Uislamu Unaamuru Wanaume Kufuga
  Ndevu: Tuangalie Biblia
  Inatwambiaje Kuhusu Suala Hili
  “Msikate pande yote ya nywele
  zenu ya vichwa, wala msikate
  pande ya ndevu zenu. (Biblia, Walawi 19:27) Katika Biblia
  imetajwa katika maeneo mengi,
  kwamba manabii na waumini
  walikuwa na ndevu. Tazama kwa
  mfano Ezra 9:03, Mambo ya
  Walawi 21:05, Nehemia 13:26 Najivunia Kuwa Muislam
   
 9. A

  ADK JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2012
  Joined: Jan 13, 2012
  Messages: 1,153
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  ndugu acheni kulalamika fanyeni yote lakini kumbukeni kuanzisha na shule zenye tija
   
 10. DULLAH B.

  DULLAH B. JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2012
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 674
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Acheni ubwege mbona kina Lowasa Pinda wanachangia makanisa mapesa mengi hamsemi? Akifanya muislam kuhusu dini yake mnaumia. Shame on u!
   
 11. s

  sir echa Member

  #11
  Oct 13, 2012
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tatizo sio muislam kuchangia dini yake, tatizo ni hicho chombo alichochangia kinahamasisha uchochezi na kinajenga chuki baina ya waislamu na wakristo jambo ambalo ni hatari kwa amani na usalama wa nchi yetu..
   
 12. Achahasira

  Achahasira JF-Expert Member

  #12
  Oct 13, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na vpi vyombo vyenu, maana Chuki kwako ni ukweli. unataka kusema waislam hawateswi nchii hii? alafu unajiits great thinker.

  hebu tuache ku reply ukiona huna lakusema. kaa kimya jifunze
   
 13. Pelham 1

  Pelham 1 JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2012
  Joined: Feb 29, 2012
  Messages: 521
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Mkuu kwani nyinyi si mna ATN mbona hatuongei ama sio ya Tv ya Wakristo?
  Swala la Imani kitu kingine kabisa Mkuu liache kama lilivyooo...
  Kila Mtu ana uhuru wa kuabudu nakuchangia dini yake
  Ndio maana akina Pinda,Lowassa, Mama Rwakatale n.k wanachangia nakusapot dini zao sembuse Mariam Seif!!.
  Serikali haina dini bt Waliondani ya serikali wana dini ndio maana wanapoteuliwa huapishwa kwa Imani ya dini zao.
  Acha tusapot na kuwekeza ktk dini yetu tukitegemea malipo kwa Mungu
  Ama ww unataka tusapoti nakuweza anasa.
  Naww pia waweza kuja kukeza Dini ya haki Islam
  Upo Mkuu.
  "Karibu sana"
   
 14. s

  salmar JF-Expert Member

  #14
  Oct 14, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 782
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Bro nakugongea like u truely wise man
   
 15. s

  salmar JF-Expert Member

  #15
  Oct 14, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 782
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Kweli mods sijui hawachuji habari zinazo postiwa humu nakumbuka miaka mitano nyuma jf it was realy ya ma great thinkers sio sasa jf imekua ya wasema chochote maana huyu mleta mada ni sawa na mnywa gongo wa kariakoo mm ningekua mod nisiingei publish huu utumbo asa maalim kuichangia tv imaan ndio imekuuma basi naserekali inayowapa exptn makanisa yakaingiza bbidhaa kwa majina ya kanisa alafu yakauzwa vp hapo mbona husemi. Naogop kusema mengi nisije nikapigwa ban bure
   
 16. kashengo

  kashengo JF-Expert Member

  #16
  Oct 14, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 2,648
  Likes Received: 464
  Trophy Points: 180
  umewahi kuitazama TV IMAAN? Au udini unakusumbua? Upuuzi hampendi maendeleo ya waislam na itaendelea maana wako hewani miezi miwili ijayo Digital
   
 17. kashengo

  kashengo JF-Expert Member

  #17
  Oct 14, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 2,648
  Likes Received: 464
  Trophy Points: 180
  Mleta Mada muongo na mnafiki,mfitini nani kamwambia Maalim Seif ni mfadhili wa Taasisi ya Islamic foundations? Yani milioni mbili kwenye harambee uwanja wa Taifa tayari ni MFADHILI?

  MLETA THREAD ana propagate Udini na tumeshachoshwa na mada za sampuli hizi hapa zomba come here meen
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #18
  Oct 14, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Hao wote uliowaandika wala hawahusiki na Imaan TV.
   
 19. Dogo1

  Dogo1 JF-Expert Member

  #19
  Oct 14, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,102
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Naungana na ww mia kwa mia mkuu JF kwa sasa haina mchango wa maana kwa jamii zaidi ya uchochezi. Vyombo husika vinapaswa kuingalia na kuchukua hatua stahiki. JF imekuwa kokoro, kila mwenye matusi ambayo amekosa sehemu ya kuyatolea bac anakimibilia JF!
   
 20. M

  Mariposa Member

  #20
  Oct 14, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yes! Umezungumza ya maana mkuu. Hem wape hao wenye chuki na uislamu, wasokwisha kuupaka matope na kuuita majina mabaya.
   
Loading...