Maalim Seif na balozi wa Uingereza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maalim Seif na balozi wa Uingereza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by salmar, Oct 14, 2012.

 1. s

  salmar JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 782
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Zanzibar na Uingereza zinakusudia kuendeleza mahusiano katika nyanja mbali mbali za kiuchumi kwa maslahi ya pande hizo mbili.

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ameeleza hayo huko Ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar alipokuwa na mazungumzo na balozi wa Uingereza nchini Tanzania bibi Diane Loise Corner.

  Amesema katika ziara yake ya hivi karibuni nchini Uingereza Maalim Seif amesema Zanzibar imeweza kugundua maeneo tofauti ambayo nchi hizo mbili zinaweza kushirikiana katika kukuza uchumi wake.

  Amesema ziara yake hiyo imempa matumaini makubwa kwamba Zanzibar inaweza kunufaika kutokana na uhusiano wake wa muda mrefu na Uingereza.

  Kwa upande wake balozi wa Uingereza nchini Tanzania bibi Diane Corner amesema nchi yake imefurahishwa na hali ya amani inayoendelea Zanzibar , na kwamba iko tayari kutoa mashirikiano katika kuendeleza uchumi wa Zanzibar .

  Ameahidi kuwa Uingereza ambayo ni rafiki wa muda mrefu wa Zanzibar itaendelea kukuza mahusiano hayo kwa lengo la kuisaidia Zanzabar kuendeleza uchumi wake. My take. Hivi tokea lini mabeberu na wezi wakawa na marafiki wa kudumu
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2014
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,567
  Likes Received: 18,313
  Trophy Points: 280
  Salmar, ni wewe huyu?!.
  Pasco
   
 3. s

  salmar JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2014
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 782
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Naam boss pasco za siku tele boss
   
Loading...