LUKAZA
Senior Member
- Nov 30, 2010
- 140
- 70
Katika kipindi cha Funguka cha Azam two Malim Seifu akiri kuwa hakuna barua wala kielelezo chochote kuwa Lipumba amekubaliwa kujiuzulu na chama Cha CUF
Anakiri pia chama kina mgogoro Mkubwa ambao unasababishwa ba Lipumba na yeye Malim Seif
Na hii inaonesha wazi kuwa Seif ni Mfalme wa Chama kwa hiyo na yeye anachuki binafsi ya maamuzi yake kwa chochote anachokitaka ndo kiwe
Hata hivyo amekubali kuwa kesi ipo Mahakamani na pia pindi Lipumba akishinda wataheshimu maamuzi ya mahakama kuu.
Na Lipumba kuwa Mwenyekiti wake ila kama hata atakuwepo hatakuwa na mashirikiano nae katika chama
==========
Nukuu muhimu
Maalim Seif: Tulimuomba Prof Lipumba asijiuzulu lakini alikataa
Maalim Seif: Wakati huu ndio nimekuwa imara zaidi kuliko kipindi chote
Maalim Seif: 'Mtu akijiuzulu atumpi tena nafasi, katiba yetu hairuhusu hivyo'
Maalim Seif: Je ni wakati sasa kukaa pembeni? Tukishapata haki yetu na mimi kuwa rais, mengine yatafata uchaguzi ujao
Maalim Seif:
Maalim Seif: Hivi sasa dunia haikubali mtu kung'ang'ania madaraka hata kama umeshindwa, hili linaendelea kufuatiliwa
Maalim Seif: Mimi ni mtu wa misingi, hakuna sehemu Katiba inasema kurudia uchaguzi, ulirudiwa kwa misingi ipi?
Maalim Seif: Iwapo mahakama itakubaliana na hoja za msajili kuhusu Prof Lipumba, tutaheshimu maamuzi
Maalim Seif: Sijapata hata kufikiria kuunda chama wala kufikiria kujiunga na chama kingine
Maalim Seif: Katiba yetu inasema mtu akijiuzulu wadhifa wake, hana nafasi ya kurudi tena
Maalim Seif: 'Haiwezekani chama kimoja cha upinzani kuishinda CCM lakini UKAWA itasaidia'- Maalim Seif
Maalim Seif: 'Kama nilifanya kosa kutangaza matokeo kwa nini hawakunipeleka mahakamani?'
Maalim Seif: 'Lipumba alidhani akijiuzulu wengi watamfuata lakini haikuleta athari CUF, uchaguzi 2015 tulishinda majimbo 10 TZ bara'
Maalim Seif: 'Hatukubaliani na msajili wa vyama ndio maana tukaenda mahakamani, hawezi kutengua maamuzi ya vikao vya chama
Maalim Seif: 'Mtu anajiuzulu halafu anarudi unafikiri anarudi kwa mema'
Maalim Seif: 'Mkutano mkuu wa taifa ulifanyika tukasoma barua ya kujiuzulu kwa Lipumba na mkutano ukaidhinisha'
Kwa msaada wa Mitandao

Mkuu LUKAZA kuwa mkweli
Wote tunaangalia hapa kipindi cha FUNGUKA kati ya Maalim Seif na gwiji Thido Mhando.
Alichokisema Seif ni kuwa,barua ya Lipumba aliyoiandika kwa minajili ya kijiuzulu ipo,na aliiandika baada ya kuwa amebembelezwa sana asifanye hivyo.
Lipumba alifuatwa na Juma Duni na Maalim Seif usiku walikaa masaa kumuomba asiondoke,wakafuata wazee wa chama,akagoma,wakatumwa viongozi wa dini na wao Lipumba akawagomea.
Akakaa miezi tisa,na kwa muda wote huo hakukanyaga ofisini na alikabishi kila kitu.Ikaundwa kamati ya muda ya uongozi na Lipumba akawa kimyaa.Muda huo wote kwanini hakurudi?Kwa hiyo Seif anasema kukaa nje ya ofisi miezi tisa tena kwa kuandika barua kuwa umejiuzulu,inakuwaje urudi tena useme unautaka ule uenyekiti?
Kingine Seif anasema mpaka sasa Wahisani wa SMZ woote wamekata misaada,na pia kuna misaada kwenye serikali ya Muungano imekatwa na wahisani sbb ya "mgogoro" wa Znz.Hii hali ya uchumi kutikisika na serikali kusema haina lepe la pesa ni sbb ya mgogoro wa Znz,na njia pekee iliyobaki ni Serikali kumtumia Lipumba achukue chama halafu aje akubaliane na matokeo na kuitangazia dunia kuwa mgogoro umeisha wahisani walegeze kamba.
Kilichonishangaza tu na mimi,ni kuwa Seif anaamini atapewa urais wake wa Znz "aliodhurumiwa".Anasema hawezi kusema mambo yote hadharani,lakini yeye anaelewa hatua iliyofikia na anawaambia watu wa Znz kuwa waisubirie Serikali itakayoongozwa na CUF muda wowote.
Maalim Seif anasema Msajili ndio katikati ya mgogoro,anajua katiba ya CUF ruzuku lazima ifike kwa Katibu Mkuu,na mpaka sasa hakuna mahali ambapo msajili hamtambui Seif ambaye ndio "signatory" wa kwanza wa ruzuku ya chama.Siku moja kabla ya kupeleka pesa msajili akasimamia zoezi la kubadili "signatories" na kuingiza ruzuku kwenye akaunti ya Wilaya wakati kwenye kumbukumbu za msajili akaunti ya Taifa ipo.
Maalim Seif anasema "bwana Profesa" ana nguvu za dola nyuma yake.Anasema anasikitika sana mambo ambayo anayafanya Prof Lipumba,kuna mahali Prof alishirikiana na polisi kuvunja ofisi na kuingia kwa nguvu wakati polisi haohao wakatumika kumzuia Maalim Seif.
Anasema matibabu yake yote anayokwenda kutibiwa nje ya nchi kwa sasa hapati senti yoyote toka SMZ japo ana haki kikatiba ya kutibiwa na serikali.Seif anasema licha ya kuwa ana haki zake kikatiba kama Makamu wa Rais mstaafu juu ya kutibiwa,lakini hataki kuomba pesa ya matibabu serikalini sbb watamsimanga sana.Anaamua kujipigapiga mwenyewe na kujigharamia juu ya afya yake kila anapohitaji kufanya hivyo.
Anasema haki zake nyingine si HISANI bali zipo kisheria,kwa hiyo hata wanaosema Dr Shein amkatalie baadhi ya stahiki zake ni wapotofu,sababu anastahili mambo yote si upendeleo bali ni haki.
Seif anasema mpaka sasa ana haki ya posho kama Makamu wa Rais na ni kwa mujibu wa katiba,ana gari na dereva wake pamoja na ulinzi,japo na yeye amejiimarisha kwa ulinzi wake.
Na amemaliza kwa kusema,mda wowote tena mfupi toka sasa atakuwa Rais wa SMZ