Maalim Seif kuwasili jijini Dar es Salaam na boti akitokea Unguja

Miiku

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2014
Messages
3,704
Points
2,000

Miiku

JF-Expert Member
Joined Oct 8, 2014
3,704 2,000
Taarifa Muhimu:

Kesho saa 5 asubuhi Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad atawasili Dar es Salaam akitokea Unguja na Boat ya Azam Marine.

Wapenzi na WANACUF WOTE JIJINI DAR ES SALAAM asibaki mtu nyumbani tukiwa na sare za CHAMA twendeni tukampokee Katibu Mkuu wetu na baadae kuelekea ofisi za Wabunge Magomeni.

Upatapo taarifa hii mjulishe mwenzio. Wasioweza kuja Bandarini watusubiri Magomeni.

Maharagande
Naibu MKURUGENZI HABARI

15/3/2019

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pulchra Animo

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2016
Messages
733
Points
1,000

Pulchra Animo

JF-Expert Member
Joined Jun 16, 2016
733 1,000
Taarifa Muhimu:

Kesho saa 5 asubuhi Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad atawasili Dar es Salaam akitokea Unguja na Boat ya Azam Marine.

Wapenzi na WANACUF WOTE JIJINI DAR ES SALAAM asibaki mtu nyumbani tukiwa na sare za CHAMA twendeni tukampokee Katibu Mkuu wetu na baadae kuelekea ofisi za Wabunge Magomeni.

Upatapo taarifa hii mjulishe mwenzio. Wasioweza kuja Bandarini watusubiri Magomeni.

Maharagande
Naibu MKURUGENZI HABARI

15/3/2019

Sent using Jamii Forums mobile app
Wana CUF mnanishangaza mnapokubali kuendelea kutumiwa na watu kwa maslahi binafsi! Hivi CUF ina hazina ndogo kiasi hicho ya wanachama wenye uwezo wa kuongoza? Kama kweli uwepo wa CUF unategemea Lipumba au Maalim, basi hicho chama hakina sifa ya kuwa chama cha kisiasa (perpetual succession is highly doubtful). Tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe Tanzania, Maalim ndiye mara zote amekuwa mgombea wa CUF wa urais wa Zanzibar. Nadhani hii ni kampuni binafsi; waachieni wenye kampuni yao badala ya kuendelea kutumika kubariki maslahi yao binafsi!

Kama CUF ni ya wanachama, basi wanachama na waoneshe hivyo kwa kuwapiga chini Maalim na Lipumba!
 
Joined
Feb 8, 2018
Messages
37
Points
95
Joined Feb 8, 2018
37 95
Wameshakuambia kuwa "alipo tupo".
Hata umautini watakuwa nae.

Lipumba yeye kasema ni "ngunguri" yaani haondoki mtu.

CCM wanakuambia "ina wenyewe".

CDM wanaiita "SACCOS".

Usishangae hii yote ni sababu ya ulaji kupitia kuwapumbaza watu kupitia saikolojia ya siasa.

Tembo wanagombania nyasi.

Watawala wachache watawaliwa wengi.
Ndio kanuni ya survival is for the fitest.

Utaishi kwa shida kwa ajili ya kumnufaisha mwingine kwani wewe utakuwa soko la bidhaa za matajiri na chanzo cha kodi kwenda kwa utawala uliopo.

Ni utumwa na utwana uliostaarabika.

Ikiwezekana hata kupoteza maisha ya wachache wanaokaidi hii falsafa ya maisha.

Watatibiwa ughaibuni kwa gharana zako,wataenda kupunzika huko pia,hata uliodhani wanakupigania kuwa uko binadamu sawa na yeye ona sasa hata mke wake atatakiwa akajifungulie ughaibuni kwani haiamini hata ile hospitali aliyochangia kukujengea pale jimboni kwake.
Wana CUF mnanishangaza mnapokubali kuendelea kutumiwa na watu kwa maslahi binafsi! Hivi CUF ina hazina ndogo kiasi hicho ya wanachama wenye uwezo wa kuongoza? Kama kweli uwepo wa CUF unategemea Lipumba au Maalim, basi hicho chama hakina sifa ya kuwa chama cha kisiasa (perpetual succession is highly doubtful). Tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe Tanzania, Maalim ndiye mara zote amekuwa mgombea wa CUF wa urais wa Zanzibar. Nadhani hii ni kampuni binafsi; waachieni wenye kampuni yao badala ya kuendelea kutumika kubariki maslahi yao binafsi!

Kama CUF ni ya wanachama, basi wanachama na waoneshe hivyo kwa kuwapiga chini Maalim na Lipumba!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Forum statistics

Threads 1,378,912
Members 525,244
Posts 33,728,169
Top