Maalim seif kuunguruma London | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maalim seif kuunguruma London

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by X-PASTER, Feb 7, 2010.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Feb 7, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,649
  Likes Received: 117
  Trophy Points: 160
  As received:

  MKUTANO WA HADHARA
  MAALIM SEIF SHARIF KUNGURUMA LONDON

  Jumuiya ya wazanzibari UK (ZAWA) inafuraha kuwaalika mkutano wa hadhara utakaohutubiwa na Katibu Mkuu CUF-Taifa Maalim SEIF SHARIFF HAMAD.

  Wazanzibari wote, wake kwa waume, waliopo UK na nchi za jirani wanakaribishwa kuhudhuria. Huu ni mkutano wa kihistoria na wa kwanza kufanyika London baada ya makubaliano yaliyofikiwa baina ya CUF na CCM Zanzibar.

  Kwa vile London ina umuhimu mkubwa katika siasa za Zanzibar tunamshukuru Maalim Seif kututunukia ziara yake kama Wazanzibari wa mwanzo Ulimwenguni kuhutubiwa baada ya maridhiano kupitishwa.

  SIKU NA PAHALA
  Jumamosi ya tarehe 13/02/2010

  Ukumbi wa Durning Hall

  ADDRESS:
  Earlham Grove,
  Forest Gate
  London,
  E7 9AB ,
  (Nyuma ya Mangala Solicitor.

  Kwa maelekezo zaidi ya pahala piga simu No: 02085363800

  UFIKAJI/USAFIRI
  Bus: 25, 86, 58
  Train. Forest Gate station (British rail)

  WAKATI: Saa saba na nusu mchana (1.30PM)

  WAHUSIKA: Kwa maelezo zaidi piga simu No:
  07957654192, 07960355753,
  07508016265, 0783180339
   
 2. a

  alibaba Senior Member

  #2
  Feb 7, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 185
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  XP,
  Wasio Wanzanzibari je hawastahili kuhudhuria?? labda niliweke swali vingine Mtanzania bara/Mtanganyika ana haki ya kuhudhuria??
   
 3. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #3
  Feb 7, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,649
  Likes Received: 117
  Trophy Points: 160
  Taarifa niliyoletewa mimi mwisho wa tangazo limeandikwa neno:

  ………..NYOTE MNAKARIBISHWA………

  Hii inaonyesha kuwa mkutano ni wa kila Mtanzania, ila msisitizo umewekwa kwa Wazanzibar kwa vile yale makubaliano yaliyofikiwa baina ya CUF na CCM kule Zanzibar, ni kwa Wazanzibar.

  Ila kwa taarifa zaidi piga hizo namba simu hapo juu.

  Thanks.
   
 4. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #4
  Feb 7, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,765
  Likes Received: 1,028
  Trophy Points: 280
  Tunamwombea Aungurume vizuri na mafanikio ya kuunguruma.
   
 5. n

  nyetisana New Member

  #5
  Feb 7, 2010
  Joined: Feb 7, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunajiandaa kuja kusikiliza huo Muungurumo.
   
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  Feb 7, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,772
  Likes Received: 4,916
  Trophy Points: 280
  Mufanye Murudi Nyumbani Muache kujiripuwa Kusema Nyinyi Ni Wasomali Wakati Nyinyi ni Wazanzibar Njooni Mujenge Nchi yetu jamani

  Mkuu X-PASTER Kumbe Wewe Uko London?
   
 7. B

  Bull JF-Expert Member

  #7
  Feb 8, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Sidhani kila anaeishi London kajilipua, wako tafauti na pia wanweza kujenga nchi wakiwa London, US na kwengineko sio lazima kurudi Tanzania ndio unaweza kujenga nchi. Hivi wako wangapi hapa Tanzania na kazi zao kubomoa nchi?
   
 8. B

  Bumbwini Member

  #8
  Feb 8, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  tutahudhuria mkuu xp,wala usijali napia ni kwa watanzania wooote mnaruhusiwa kuhudhuria,shime tujitokeze kwa wingi bila kukosa.
   
 9. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #9
  Feb 9, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,649
  Likes Received: 117
  Trophy Points: 160
  Eeh! Mambo ya mkutano na Usomali wapi na wapi, alafu tena kujiripua...!? Daha! haya yetu macho!
   
 10. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #10
  Feb 9, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 43,164
  Likes Received: 27,143
  Trophy Points: 280
  Atakuwa anazungumzia nini?? i mean agenda?
   
 11. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #11
  Feb 9, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,649
  Likes Received: 117
  Trophy Points: 160
  Ajenda nadhani ni muwafaka kati ya CUF na CCM Zanzibar, ila ukiudhuria itakuwa bora zaidi.
   
 12. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #12
  Feb 9, 2010
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Agenda
  1.CCM ni chama bora ndo maana nikaamua kuungana nacho
  2.Chagua CCM kwa wabara kwani Zanzibar bado tuko kwenye mazungumzo ya k usogeza mbele uchaguzi
  3.Nikichaguliwa kuwa makamu wa Rais mtarudi nyumbani kwani ninaandaa mipango ya kuibadilisha Zanzibar ionekane kama ulaya vile nikishirikiana na Mh.Rais niliyemtambua Amani A.Karume,kwa hiyo mjiandae kurudi nyumbani
  4.Mengineyo
   
 13. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #13
  Feb 9, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Basi watu wa uhamiaji wa kija kwenye mkutano huo wa wazenj,watawakuta wasomali...he he he
   
 14. Peasant

  Peasant JF-Expert Member

  #14
  Feb 9, 2010
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 3,949
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mmmh! Acha hizo mkuu, mbona haipo kwenye hilo tangazo?! Jaribu kuwa mkweli, wamealikwa Wazenji, huu ni mkutano wa Wazanzibari, haitakuwa busara kwa Wabara kuhudhuria katika mazingira kama haya.
   
 15. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #15
  Feb 9, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Aje aongee point sio kuunguruma tuuuuuu
   
 16. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #16
  Feb 9, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  miaka ya 99-00 jijini London,kulikuwa na Mzanzibar anaomba omba pale East Ham underground station,yuko wapi siku hizi?aliharibu sifa ya wazenj!nafikiri alikuwa amejilipua
   
 17. J

  Jekyll+Hyde Member

  #17
  Feb 9, 2010
  Joined: Jul 23, 2009
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jumuiya ya wazanzibari UK (ZAWA) = CUF ???

  Jumuiya ya Watanzania/Watanganyika UK (TA UK) = CCM???
  Nauliza tu, maana naanza kupata hisia na mtazamo tofauti wa hizi Jumuiya ama ni wawakilishi wa vyama vya kisiasa ughaibuni?

  Kumbe Wazanzibari sio Watanzania? au ndio kubagua wa kutoka Tanzania bara, je hao wazanzibari wanahold passport za Uraia gani?
  Tanzania Bara na Tanzania Visiwani ingekaa vizuri kidogo katika tangazo lenu
   
 18. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #18
  Feb 12, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,649
  Likes Received: 117
  Trophy Points: 160
  Wanzazibar wao bado wanao utaifa wao, ila Watanganyika utaifa tulisha uunganisha kwenye Muungano.

  Kila mtu anakaribishwa kwenye huo mkutano.

  Kwa taarifa zaidi piga simu hapo juu.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...