Wanabodi;
Kuweka kumbukumbu sawa,ikumbukwe katika chaguzi zote za uchaguzi mkuu za mwaka 1995,2000,2005,2010 na 2015 CHADEMA hawakusimamisha mgombea urais kwa upande wa Zanzibar na walitangaza dhahiri kumuunga mkono Maalim Seif katika chaguzi zote hizo.
CHADEMA walisisitiza kuwa kura za wanachama ,wapenzi na washabiki wao ziende kwa Maalim Seif.
Nakumbuka mwaka 2005 kwenye uchaguzi mkuu CHADEMA walimsimamisha Freeman Mbowe kugombea urais kwa upande wa Tanzania Bara.Mbowe alisafiri hadi Zanzibar kwenda kumnadi Maalim Seif hususani kwenye siku za uzinduzi na ufungaji wa kampeni za urais za CUF.
Ilihitaji roho ngumu kwa Mbowe kuacha kuendelea na kampeni zake za Urais huku Tanzania Bara na kwenda Zanzibar kumsapoti Maalim Seif.
Nakumbuka vilevile kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 wakati CHADEMA kikiwa bado chama kichanga kilitangaza waziwazi kushirikiana na CUF kwenye baadhi ya majimbo ya uchaguzi ambapo kwa yale majimbo ambayo Chadema haikusimamisha wagombea walitangaza kwamba kura za wanachama na wapenzi wa CHADEMA ziende kwa wagombea wa CUF.
Vilevile kwenye chaguzi za serikali za mitaa CHADEMA walikuwa wakisisitiza kuwa sehemu ambazo hakuna mgombea wa CHADEMA basi kura zote ziende kwa wagombea wa CUF.
Haihitaji kuwa na PhD kujua ni jinsi gani Chadema kimekuwa kikimsapoti kwa hali na mali Maalim Seif Shariff Hamad katika harakati zake za kisiasa huko Tanzania Visiwani.
Kwa mshangao wa wengi Maalim Seif amehamia ACT chama ambacho hakina hata miaka mitano ya uhai wake,chama ambacho hakijawahi kumsapoti kwa aina yoyote(kumbuka AcT hawakuwepo kwenye mwamvuli wa UKAWA).
Hii ndio yathibitisha kauli ya wahenga "shukrani ya punda mateke"
TIME WILL TELL