kisanganyakiswata
JF-Expert Member
- Jan 28, 2014
- 1,294
- 543
Lala uote tenaHabari za chini ya carpet zinadai kuna mkakati mahsusi wa kiuchaguzi kati ya Chadema na ACT wazalendo ambapo baba wa upinzani maalim Seif anatarajiwa kugombea urais wa JMT.
Mh Mbowe anatajwa kuwa mgombea mwenza huku Zitto Kabwe akiandaliwa kuwa Waziri mkuu.
Godbless Lema naye anatajwa kuhamia jimbo la Hai ambako ni nyumbani kwao kugombea ubunge na akishinda anaweza kuteuliwa kuwa Waziri wa mambo ya ndani na Naibu Waziri mkuu kama ilivyokuwa kwa Augustini Lyatonga Mrema enzi za Mwinyi.
Safari hii bendera itakayopeperushwa ni ya ACT wazalendo.
Endeleeni kunywa mchuzi nyama mtazikuta chini
Maendeleo hayana vyama!
Sent using Jamii Forums mobile app