Maalim Seif kugombea tena Ukatibu Mkuu CUF, Achukua Fomu Ijumaa Mei 23rd, 2014

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,869
1,225


Friday, May 23, 2014

Maalim Seif kugombea tena Ukatibu Mkuu CUF, Achukua Fomu leoKatibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akichukua fomu ya kugombea tena nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama hicho katika ofisi kuu za CUF Wilaya ya Magharibi Kilimahewa Zanzibar. Anayemkabidhi ni Kaimu Katibu wa CUF Wilaya ya Magharibi Ussi Juma Hassan.
Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akionyesha fomu ya kugombea tena nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama hicho katika ofisi kuu za CUF Wilaya ya Magharibi Kilimahewa Zanzibar.
Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na wanachama waliojitokeza kumsindikiza wakati wa kuchukua fomu hiyo. katika ofisi kuu za CUF Wilaya ya Magharibi Kilimahewa Zanzibar.


Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na waandashi wa habari katika ofisi kuu za CUF Wilaya ya Magharibi Kilimahewa Zanzibar, baada ya kuchukua fomu ya kugombea tena nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama hicho (Picha na Salmin Said, OMKR)

Na Hassan Hamad OMKR

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, leo amechukua fomu ya kugombea tena nafasi ya Katibu Mkuu wa Chama hicho.

Maalim Seif amechukua fomu hiyo katika Ofisi za CUF zilizopo Kilimahewa Wilaya ya Magharibi Unguja, na kusindikizwa na viongozi na wanachama kadhaa wakati akichukua fomu hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu hiyo Mhe. Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesema ameamua kuchukua fomu hiyo ili aendelee kuwatumikia wanachama na kufikia malengo ya chama waliyojiwekea.

Amefahamisha kuwa pia ameshawishika kuchukua fomu hiyo baada ya kujitokeza kauli za kutaka kuzorotesha serikali ya umoja wa kitaifa.
Amesema akiwa kiongozi wa Chama ataendelea kuwatumikia wanachama na wananchi hadi pale chama kitakapotimiza malengo yake.

Maalim Seif amesema kwa kipindi kirefu alikua hajaamua iwapo agombee tena nafasi hiyo, na ndio maana hapo awali aliwahi kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa nafasi ambayo tayari ameondoa jina lake kufuatia uamuzi wake wa kugombea tena nafasi ya Katibu Mkuu.

Chama hicho tayari kimekamilisha uchaguzi wa chama ngazi za Matawi na Majimbo, na hatua inayofuata ni uchaguzi ngazi ya Wilaya.

Akizungumzia kuhusu tetesi za kuzorota kwa serikali ya umoja wa kitaifa Mhe. Maalim Seif amesema serikali hiyo itaendelea kuwepo kwa vile imekuwepo kwa matakwa ya wananchi walio wengi, na kwamba hawako tayari kurudi walikotoka.

Ameongeza kuwa katika kipindi cha uongozi wake akiwa Katibu Mkuu wa Chama hicho kilikabiliwa na changamoto kadhaa zikiwemo za upungufu wa rasilimali, lakini akasema wamejitahidi kakabiliana nazo kuona kuwa haziathiri ustawi wa chama hicho.

Kuhusu tetesi za kuwepo mgogoro kati ya chama hicho na mbunge wa Jimbo la Wawi Mhe.Hamad Rashid, Maalim Seif amesema Hamad Rashid hawamtambui kwa vile sio mwanachama wa chama hicho.

"Wala sisi hatusumbui kwa sababu sio mwanachama wetu, yeye ni mbunge wa mahakama na wala sio wa CUF", alisisitiza Maalim Seif.

Pamoja na mambo mengine Mhe. Maalim Seif amesema CUF ni chama kinachofuata misingi ya kidemokrasia, hivyo mwanachama yeyote anayaona ana sifa kugombea nafasi yoyote ikiwemo ya Katibu Mkuu yuko huru kuchukua fomu na kugombea nafasi hiyo.

Maalim Seif anatarajiwa kurejesha fomu hiyo tarehe 30/05/2014, ambapo tarehe ya mwisho ya kurejesha fomu ni tarehe 10/06/2014.source: ZanzibarNews
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom