Maalim Seif kuapishwa leo na Rais wa Zanzibar Dkt. Mwinyi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi kesho Disemba 8 atamuapisha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.

Hafla ya kumuapisha Maalim Seif itafanyika Ikulu Zanzibar.

Rais Mwinyi amemteua Maalim Seif Sharif Hamad ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, uteuzi ulioanza Disemba 6 mwaka huu.

Uteuzi huo umezingatia matakwa ya kifungu cha 9(3) cha katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

 
Eon5hfTUYAAYW9f.jpeg


kwako Mwalimu Kashasha
 
Atulie sasa ale mema ya nchi na kelele za uchaguzi ziishe.
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi kesho Disemba 8 atamuapisha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad...
Hongera sana Maalim Seif.....Imeisha hiyo....Jussa amesemaje kuhusu GNU?
 
Siasa za ZANZIBAR Watanganyika hamzifahamu tunakabiliana na magumu mengi na haya yote mnayafanya nyinyi Watanganyika kuingia ktk serikali kunafaida kubwa KWA ustawi wa Nchi yetu
 
Nchi inaenda ‘kuponywa’

Wale vijana wadogo waliouawa Pemba wakiamini wanapigania haki zao kama walivyoaminishwa na Maalim Seif Mungu awape pumziko jema. Familia walizopoteza ndugu zao, Mungu awape moyo, hii ni hali ngumu kwao.

Vipi Jusa na yale majeraha hajalamba teuzi ya kumpoza? Au bado yupo hospitali?
 
Atulie sasa ale mema ya nchi na kelele za uchaguzi ziishe.
Tunaingia serikalini huku Madai yetu yakiendelea
UHURU WA KUJIELEZA
UCHAGUZI HURU
WALIOHUSIKA NA VURUGU KIPINDI CHA UCHAGUZ WASHTAKIWE KWA MUJIBU WA SHERIA
 
Akipigwa mawe mtaani atatatetewa na haohao CCM aliokubali kuwa submissive kwao na aliowatumu huku akiongea kwa Tambo usitutishee usitufokeee.....!!!Pumbavu kabisa wanasiasa wa Tanzania.
Apigiwe mawe na Nani?
Nyie mnaongea tu hivi mnajua gharama za kuendesha chama?

Wangepata wapi hizo ela?
Ww unataka wenzako wasuse Sasa hivi uko kwenye Gari unaenda kazini kwako

Ili upate pesa za kuhudumia familia yako na watu wengine

Na ACT nao ni binadamu,
 
Safi sana Maalim na uongozi wa ACT pamoja na wanachama wa ACT mmefanya maamuzi mazuri sana kwa mustakbali wa wazanzibari.

Rais Dr. Hussein Mwinyi ni mtu hodari sana ba mwenye nia ya dhati ya kuleta maendeleo kwa wazanzibari, hivyo hakuna budi kumuunga mkono Mhe. Rais Dr. Hussein.

Endapo wazanzibari wote tutaungana kwa dhati na kwa dhamira ya pamoja basi naamini ndani ya miaka 5 znz itapaa kwa maendeleo.

Maalim seif huu ndio muda wako wa kuwatumikia wazanzibari na kuacha alama itakayo kumbukwa vizazi na vizazi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom