Elections 2010 Maalim seif je ni ukomavu wakisiasa,? umeshinikizwa au ndo ustarabu?

mnyikungu

JF-Expert Member
Jul 26, 2009
1,960
2,464
Kwa waliowahi kufuatilia historia ya Seif na uchaguzi zanzibar nadhani watanisaidia kwa hili. Maalim seif ana historia ndefu sana na siasa za ZANZIBAR yaani toka enzi za mwalimu yeye ni mpinzai. kwa miaka yote ya uchaguzi zanzibar seif hushika nafasi ya pili na hajawahi kuyakubaki matokeo hata kidogo na siku zote huwa anakataa kuitambua serikali iliyoko madarakani kwa madai kwamba yeye ndiye huibuka mshindi.Safari hii nimeshangaa na kushtuka sana, kwa sababu seif kakubali kushidwa kilaini sana japo hotuba yake inaonyesha hajaridhika na matokeo. sasa najiuliza kwa nini seif hajagomea uchaguzi huu(japo sipendi afanye hivyo kama hamna sababu) kama alivyofanya miaka mingine?
1. amekomaa kisiasa
2. ameshinikizwa kukubali
3. au kweli anajali maslahi ya zanzibar
 
Seif itabidi aondolewe ktk CUF. Kuna habari kwamba kuna uwezakano wa Seif kujiuzulu ndani ya CUF. Watu wamepoteza maisha yao kwa sababu ya chama, leo anakuja kukiuza chama kwa sababu ya matakwa yake binafsi.
 
Nimemsikiliza Seif kwa makini. Anaonesha wazi hajaridhika na matokeo, ila kwa sababu ana uhakika wa kuingia serikalini kaamua kukubali yaishe. Cha kusubiri ni kama ataendelea kuwa na msimamo ule ule kuhusu siasa za znz.
 
Maalim ameridhika kwanza Mpemba mwenzake amechukua urais kitu ambacho kilikuwa ni ndoto kwao.Ndo maana kasema wasirushiane vijembe.Pili yaonekana ni furaha yake na hii imetokana na haya mambo kuwa yameshapangwa..kwa nilivyomuona maalim alikuja kukamilisha ratiba tu..katoa hotuba fupi yenye ujumbe mzito kwa mtu anaelewa siasa ya zanzibar
 
Kwa waliowahi kufuatilia historia ya Seif na uchaguzi zanzibar nadhani watanisaidia kwa hili. Maalim seif ana historia ndefu sana na siasa za ZANZIBAR yaani toka enzi za mwalimu yeye ni mpinzai. kwa miaka yote ya uchaguzi zanzibar seif hushika nafasi ya pili na hajawahi kuyakubaki matokeo hata kidogo na siku zote huwa anakataa kuitambua serikali iliyoko madarakani kwa madai kwamba yeye ndiye huibuka mshindi.Safari hii nimeshangaa na kushtuka sana, kwa sababu seif kakubali kushidwa kilaini sana japo hotuba yake inaonyesha hajaridhika na matokeo. sasa najiuliza kwa nini seif hajagomea uchaguzi huu(japo sipendi afanye hivyo kama hamna sababu) kama alivyofanya miaka mingine?
1. amekomaa kisiasa
2. ameshinikizwa kukubali
3. au kweli anajali maslahi ya zanzibar

jibu sahihi ni 2 yaani ameshinikizwa
 
Kama umemsikiliza hotuba yake iko wazi kwamba hakuridhika na mwenendo wa ZEC,ameonglea chombo hicho kukosa imani ya wananchi.Sasa ni vizuri akawepo katika serekali ili aweze kuondoa mfumo unaotumika na chama tawala kuwakandamiza wananchi nafikiri ni hatua nzuri na matumaini atafanya hivyo.
 
nimemsikiliza na ndio maana nikashangaa kukubali kilahisi vile ilhali hajalidhika
 
siasa za fujo zimepitwa na wakati, kukubali kwake matokeo, kumeepusha mambo fujo kuto tokea!

Ongera Maali Seif kwa kuonyesha ukomavu wa kisiasa.
 
Nadhani pia kesha lamba chumvi nyingi saaana, sasa iliyobakia ni kidogo bora kuimalizia kwa kuwagawia wajukuu busara. Hata majopgoo wakigombana hufikia wakati wakachoka na kuanza kutizamana. Hata jogoo wa ukweli akichoka huwa hawezi kuwika tena:tape:
 
Back
Top Bottom