mnyikungu
JF-Expert Member
- Jul 26, 2009
- 1,960
- 2,464
Kwa waliowahi kufuatilia historia ya Seif na uchaguzi zanzibar nadhani watanisaidia kwa hili. Maalim seif ana historia ndefu sana na siasa za ZANZIBAR yaani toka enzi za mwalimu yeye ni mpinzai. kwa miaka yote ya uchaguzi zanzibar seif hushika nafasi ya pili na hajawahi kuyakubaki matokeo hata kidogo na siku zote huwa anakataa kuitambua serikali iliyoko madarakani kwa madai kwamba yeye ndiye huibuka mshindi.Safari hii nimeshangaa na kushtuka sana, kwa sababu seif kakubali kushidwa kilaini sana japo hotuba yake inaonyesha hajaridhika na matokeo. sasa najiuliza kwa nini seif hajagomea uchaguzi huu(japo sipendi afanye hivyo kama hamna sababu) kama alivyofanya miaka mingine?
1. amekomaa kisiasa
2. ameshinikizwa kukubali
3. au kweli anajali maslahi ya zanzibar
1. amekomaa kisiasa
2. ameshinikizwa kukubali
3. au kweli anajali maslahi ya zanzibar