Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,495
- 9,275
Mwenyekiti wa chama cha ACT-Wazalendo Maalim Seif Hamad amesema amesikitishwa na hotuba ya kufungwa kwa Bunge la 11 iliyotolewana Rais John Magufuli leo Juni 16,2020 kwakua aliacha mambo ya msingi ambayo yanaliliwa na wananchi wa Tanzania
Akizungumza na wa mkutano wa chama cha ACT-Wazalendo mkoani Tanga, Maalim Seif amesema Rais ameongea vitu vingi lakini amesahau maswala ya msingi kama demokrasia, haki za binadamu pamoja na swala zima la tume huru ya uchaguzi
“Nimeisikia hotuba ya Rais John Magufuli ya kulifunga Bunge leo Juni 16, 2020 nasikitika sana amekwepa kuyazungumzia mambo matatu muhimu yanayolikumba Taifa letu Demokrasia na Haki za Binadamu, Tume Huru ya Uchaguzi na Uchumi imara kwa kila Mtanzania.” amesema
Ikumbukwe kuwa mapema leo Juni 16, 2020 Rais Magufuli alihutubia bunge la jamhuri ya Muungano kwa mara ya mwisho ikiwa ni kiashirilia cha kufikia ukomo kwa wabunge wote na kufungua njia za kuanza kwa uchaguzi wa madiwani , wabunge na rais mapema mwenzi Oktoba 2020