Maalim Seif Hammad hajawahi kuongelewa vibaya si mtaani wala mitandaoni

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
50,961
2,000
1618340104469.png
Maalim ni mwanasiasia mkongwe Mwenyezi Mungu marehemu, hajawahi kusakamwa na kauli za wanachama wake wala wapinzani wake licha ya kuwa mwanasiasa wa muda mrefu. Tuna la kujifunza hapa.
 
IDEGENDA

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
3,742
2,000
Bavicha mnajaribu kupambana na marehemu Magufuli,

Badala ya mshughulikie mambo muhimu mmekalia ujinga.

2025 tukiwagonga tena manaanza kulalama
 
Bayyo

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,770
2,000
Mti wenye matunda ndo hupigwa mawe.

Kwa hiyo kinyume chake ni ukweli. Ni ukweli usiopingika kuwa Maalim Seif hawezi kushambuliwa mitandaoni kwa kuwa hakupewa nafasi ya madaraka yenye maamuzi yanayoathiri wananchi.

Siyo kwamba hakuwa na madhaifu kweye siasa za upinzani, hapana. Mfano udhaifu mkubwa ni kung'ang'ania madaraka kwa zaidi ya miaka 20, kwamba hakuna mtu mwingine angeweza kurithi nafasi yake?

Huo ni udhaifu, na ni kuonesha kuwa ndani ya upinzani hakuna demokrasia. Pia hizi siasa za upinzani Kutegemea mtu badala ya taasisi ndo inaathiri upinzani wa tz, ndo maana alipohamia ACT - Wazalendo, CUF ilififia sana Z'bar.

NB: Mfumo ujengwe kwenye taasisi, na siyo umaarufu wa mtu!
 
Nyendeke

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
1,531
2,000
Maalim alisimamia Misimamo yake thabiti bila kuyumbishwa na yeyote hata kama Misimamo hiyo ilikuwa inamfanya alale Njaa.., hivyo hakuwahi kuwa Mnafiki!

Sasa wengi wa Wanasiasa tulionao zama hizi wengi wao ni Wasaka fursa na bendera fuata Upepo kama wale aliowahi kuwaeleza Mwl Nyerere kwenye hotuba zake akatumia neno " Malaya Malaya..,"
 
Krav Maga

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
4,626
2,000
View attachment 1751239
Maalim ni mwanasiasia mkongwe Mwenyezi Mungu marehemu, hajawahi kusakamwa na kauli za wanachama wake wala wapinzani wake licha ya kuwa mwanasiasa wa muda mrefu. Tuna la kujifunza hapa.

Alikuwa na Ustaarabu wake halafu hakuwa Mshamba ( Mbwiga ) kama wengineo na aliijua vyema Siasa kuliko wengine waliokuwa wakijua sana Kuchanganya tu Kemikali Maabara.
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
84,011
2,000
Bavicha mnajaribu kupambana na marehemu Magufuli,

Badala ya mshughulikie mambo muhimu mmekalia ujinga.

2025 tukiwagonga tena manaanza kulalama
Kwanini Maalim Seif hajawahi kusimangwa tangu amefariki ? ukipata jibu la hili utajifunza jambo
 
Muuza viatu

JF-Expert Member
May 14, 2020
928
1,000
vipi MKAPA mbona hajawahi kuchukiwa kama MWENDAZAKE,je na yy hakua na Madaraka?
Mkapa alikufa akiwa hana mamlaka na ndio maana hakusemwa saaaaana lkn Pombe alikufa akiwa mamlakan kawaida sana kusemwa,na lait km Mkapa angekufa akiwa mamlakan kulingana na siasa za kipind kile cuf ya maalim na lipumb ikiwa moto jeshi LA polisi kuna askar aliitwa Mahita ingekua balaa maana cuf ilikua NGANGARI na Mahita na polis wake walikuwa NGUNGURI miksa vikapatikana visu ikasemekana cuf walikua na mpango wa kulianzisha na ukata ulikua umetamalak kwa kiwango kikubwa na ridandas ilibamba balaa ktk mashirika ya umma Mkapa km angekata moto kipind kile mzee pombe angesubir
 
Bayyo

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,770
2,000
vipi MKAPA mbona hajawahi kuchukiwa kama MWENDAZAKE,je na yy hakua na Madaraka?
Wewe umezaliwa lini? Inaonekana huelewi kabisa, MKAPA alipigwa hasa mawe. Hata mzee Ruksa, kachezea sana vitasa, Kikwete ndo usiseme alipewa jina DHAIFU.

Ukiwa kiongozi lazima kuna kundi ktk jamii itakuchukia kwa sababu huwezi kuwaridhisha wote kwa wakati moja. Wengine hufuata mkumbo wa kulaghaiwa na siasa chafu. Huo ndo ukweli
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
27,952
2,000
View attachment 1751239
Maalim ni mwanasiasia mkongwe Mwenyezi Mungu marehemu, hajawahi kusakamwa na kauli za wanachama wake wala wapinzani wake licha ya kuwa mwanasiasa wa muda mrefu. Tuna la kujifunza hapa.
Dada yagu umeandika jambo lenye nguvu na kutafakarisha sana. Hawa wa akina nchemba na Vuvuzela Lusinde sijui kama watapitia hapa wasome.

Wajiulize why Jiwe ansemwa vibaya and not Maalim? Jiwe atasemwe vibaya kwa liowatendea vibaya na akina nchemba wanaofaidi ukatili wake watamsifia
 
Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
947
1,000
Ni mgombea Uraisi pekee aliejitokeza barabarani kupinga matokeo ya uchaguzi Mkuu.
 
Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
50,961
2,000
Dada yagu umeandika jambo lenye nguvu na kutafakarisha sana. Hawa wa akina nchemba na Vuvuzela Lusinde sijui kama watapitia hapa wasome.

Wajiulize why Jiwe ansemwa vibaya and not Maalim? Jiwe atasemwe vibaya kwa liowatendea vibaya na akina nchemba wanaofaidi ukatili wake watamsifia
Viongozi wetu wa upinzani tuliwqchagua ili wapate mateso chini ya himaya ya mfalme Jiwe. Sugu akiwa jela mama yake aliugua kwa mawazo. Huku tunachangishana kumtibu Tundu Lissu, kule Mbowe alikula Christmas gerezani. Acha tu.
 
dos.2020

JF-Expert Member
Feb 17, 2009
4,357
2,000
Mti wenye matunda ndo hupigwa mawe.

Kwa hiyo kinyume chake ni ukweli. Ni ukweli usiopingika kuwa Maalim Seif hawezi kushambuliwa mitandaoni kwa kuwa hakupewa nafasi ya madaraka yenye maamuzi yanayoathiri wananchi.

Siyo kwamba hakuwa na madhaifu kweye siasa za upinzani, hapana. Mfano udhaifu mkubwa ni kung'ang'ania madaraka kwa zaidi ya miaka 20, kwamba hakuna mtu mwingine angeweza kurithi nafasi yake?

Huo ni udhaifu, na ni kuonesha kuwa ndani ya upinzani hakuna demokrasia. Pia hizi siasa za upinzani Kutegemea mtu badala ya taasisi ndo inaathiri upinzani wa tz, ndo maana alipohamia ACT - Wazalendo, CUF ilififia sana Z'bar.

NB: Mfumo ujengwe kwenye taasisi, na siyo umaarufu wa mtu!

aling'ang'ania nini na wapi? Hakulazimisha mtu kuungana nae kwenye harakati alizozianzisha, na ndio mana aliondok CUF akahamia ACT ila watu ndio wanaomfuata yeye, Kuna vyama karibu ya 20 TZ, hivi yeye kugombea uraisi kwenye chama kimoja ndio kazibia watu nafasi? hivyo vyama vyengine vipo kwa anayetaka angejikita huko.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom